Ila kuna namna Wanaume mnapenda sana matatizo

Nyie subirini kurogwa tu...🤣
 
Aisee...! Kijana anakuja na hawara bila kificho hadi nyumbani na wote mnafahamu hilo na mnamkenulia meno sababu eti anavuta bangi..!?
Aisee kuna koo ni za hovyo sana yaani kabisa hamjui ya kwamba atakujatia ukoo aibu na wote muonekane ni majuha, hivi watu wazima kabisa mnawezaje kuendelea kuchangishana na kukaa vikao vya kupanga harusi ya kijana asiyejielewa.

Natamani huyo kijana mnikopeshe huku kwenye ukoo wetu naapa kwa miungu na mizimu ya mababu angeacha huo upumbavu.
 
Maumivu ya moyo baada ya kuachwa yanazidi msiba...

Wanawake wakiwa wahanga wakuu

Visasi na malipizi ya kuua kwa nguvu za Giza ila hata wanaomlilia Mungu nao anawalipia kisasi...
Hii ya Mungu kulipa kisasi haipo. Yaani uvunje sheria za Mungu wa kweli, alafu unexpect Mungu alipe kisasi kisa mtu kaachwa bila ndoa, hivi mnamjua kweli Mungu Mtakatifu?
Sheria pekee ni atavuna alichokipanda na pia sheria ya generation curse.

Ila kwa upande wa nguvu za giza ndo inawezekana.
 
Huyu uncle ni mtata mno,. Kwanza wanaweza wakamwambia wengine huko akahisi ni sisi aanze kutunyanyasa 😃😀
Hahahaha

Kaeni kwa kujitahahalisha, siku akiwa anawaangalia kwa jicho la upande upande huku kakunja sura mjue kashasanuliwa😂😂😂
 
Ingewezekana tungekupatia tu bure hili jamaa wala sio hadi kukopa,.

Ameshasemwa sana sio na mama yake ( bibi ),. Dada zake na kaka zake lakini hakuna anayemsikia kwanza anasema hataki kufatiliwa maisha yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…