Huo uwanja ni wa serikali na wasimamizi ni serikali wala sio Yanga,...Yanga ni mwenyeji kiitifaki tu lakini hana mamlaka yoyote na huo uwanja. Linapokuja swala Simba na Yanga watanzania wengi hua wanakosa akili na busara kabsa sijui kwanini?! Hivi kweli kwa hali tu ya kawaida Yanga wanaweza kuwazuia Simba ama timu yoyote kuingia hapo kwa Mkapa?! Kwa mamlaka gani waliyonayo sasa?! Wote Simba na Yanga wataingia hapo kwa ruksa ya serikali na serikali ndo imeweka wasimamizi wa huo uwanja muda wote in case of anything. Hata kama Serikali watakabidhi uwanja wa timu mwenyeji lakini sio kwa 100% lazima nao wawepo kuangalia matumizi sahihi ya mali yao ndo maana unaona gari ya polisi ambayo ndo serikali yenyewe ndo wameweka kizuizi mlangoni hapo kwamba hakuna kuingia mtu, si Yanga wala Simba. Tuache mihemko na ushabiki maandazi, miaka ijayo hizi Simba na Yanga zitasababisha Baba, Mama, mtoto na house girl wote kufanana akili😅😅😅😅
 
Yani Makolo mnaweweseka sanaa,usiku huu badala wachezaji wapumzike wawe na fitness kesho yake mnazunguka zunguka zunguka tu usiku kama wachawi.
Ngojeni kesho zile 5 zitarudi tena
 
Yani Makolo mnaweweseka sanaa,usiku huu badala wachezaji wapumzike wawe na fitness kesho yake mnazunguka zunguka zunguka tu usiku kama wachawi.
Ngojeni kesho zile 5 zitarudi tena
It's a shame to see mental health patient like this all because of Simba vs yanga...
 
wemekamatwa usiku baada ya timu ya simba kuzuiliwa kuingia uwanjani.
 

Attachments

  • wachawi.jpg
    68.1 KB · Views: 1
Naunga mkono hoja .Simba wachawi sana , uwanja wenyewe umezoeleka utadhani timu kutoka Tunisia ndio inacheza Derby
 
kwani zinasema lazima wafanyie mazoea hapo

wawe wapole kesho watapigwa swafiiiiii haina haja ya mauza uza
Hapo umeongea kishabiki mkuu , inabidi ungesema fact kwanini wakafanye mazoezi sehemu nyingine
 
Wanatafuta pa kutokea,ila kipigo kipo palepale,ila saizi wamepata kisingizio.......ni Kanuni sawa ila sijawahi kuona au kusikia timu ambayo ni mgeni kwenda kwenye uwanja wa mazoezi kwa derby yetu ya Kariakoo
 
Sizani kama mechi za watani kama zina utaratibu huu na sijawahi kuona hiki kitu kwenye mechi watani hata moja sijawahi tokea nianze kufuatilia mpira. Mara nyingi wanyumbani ndiye anaye kabidhiwa uwanja.
Mkuu nafikiri wanafuata miongozo ya FIFA na CAF sio ya Watani wa Jadi.

Ni vyema tukajadili miongozo ya FIFA inasemaje.
 
Ikifikia hivi Sheria inasemaje ,, nani anapewa adhabu kwa kuwazuia timu kufanya mazoezi kama Sheria inavyojulikana kila mahali kwamba siku Moja kabla timu mgeni anakuja kufanya mazoezi kwenye uwanja utakaotumika kwa mechi husika.
Siku moja ndani ya muda gani? Na hii nayo ni muhimu kueleweshawana.
 
Mkuu nafikiri wanafuata miongozo ya FIFA na CAF sio ya Watani wa Jadi.

Ni vyema tukajadili miongozo ya FIFA inasemaje.
Wanaifuata leo ,vip round ya kwanza au FIFA haikuwepo? Mechi zetu huku hasa za Derby timu ya ugenini hutokeaga kambini huko anapo pajua yy siku ya mechi.
 
Mimi nauliza tu swali kwanini simba walitaka kufanya mazoezi usiku? Timu mgeni anaruhusiwa kufanya mazoezi muda huo? Tumezoea mazoezi huwa ni jioni sijui kama kanuni inaruhusu mpaka usiku
 
Wanaifuata leo ,vip round ya kwanza au FIFA haikuwepo?
Mkuu tujadili uhalisia sio hisia. Kufanya kosa wakati uliopita hakuhalalishi kufanya kosa sasa.

Tunaweza kujadili uhalisia?
 
Mkuu tujadili uhalisia sio hisia. Kufanya kosa wakati uliopita hakuhalalishi kufanya kosa sasa.

Tunaweza kujadili uhalisia?
Uhalisia si ndio huu kwenye mechi zetu zote za Derby au unataka uhalisia gani?, tatizo lako unafanisha kabumbu na Socer.

Uhalisia kwamba kwenye mechi zote za Derby timu ya ugenini huingia kwenye uwanja siku ya mechi kutoka kwenye kambi anayo ijua yy, sasa sijajua unataka uhalisia gani wakati Derby zetu zipo hivyo.
 
Leta ushahidi wa picha na video...na je Sheria za mpira wa miguu zinasemaje kwa timu kufanya mazoezi siku Moja kabla ya mechi..jibu kama mtu mwenye akili na msomi...
Nafikiri sheria ya kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi iko wazi kabisa. Cha kuwekana sawa hapa ni muda gani hasa? Maana ukisema tu siku moja kabla ya mechi vipi mwingine akifika saa tano usiku, naye yuko sahihi?

Kuna mmoja kati ya Simba au Yanga hayupo sahihi.
 
Kuloga kumebuma tutakula kichapo kizuri 🤣
 
Mimi nauliza tu swali kwanini simba walitaka kufanya mazoezi usiku? Timu mgeni anaruhusiwa kufanya mazoezi muda huo? Tumezoea mazoezi huwa ni jioni sijui kama kanuni inaruhusu mpaka usiku
Mbona mechi zinachezwa usiku?
Kwa mujibu wa kanuni ni kuwa timu mgeni anatakiwa kufanya mazoezi ya mwisho siku moja kabla ya mchezo kwenye uwanja ambao mechi itachezwa hiyo mechi ,na muda wa kufanya mazoezi ushabiane na muda ambao mechi husika itaanza.
Mechi ya kesho inaanza saa 7:15 simba wamefika uwanjani 7:00 sasa hapo kosa la simba liko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…