KERO Responded Inakuwaje gharama ya kutengeneza 'kidude' cha kuwekea umeme wa LUKU ni bei kubwa hivi?

KERO Responded Inakuwaje gharama ya kutengeneza 'kidude' cha kuwekea umeme wa LUKU ni bei kubwa hivi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Toeni jibu na sio kuishia kupokea tu , haya mambo alikuwa anayapambania sana mwendazake sahivi viongozi wa juu hawana kauli mnaaumua kufanya mnavyojua kukandamiza wananchi.

R.I.P Magu
Habari, ndugu mteja.

Tumeeleza kuwa tumepokea ujumbe wake kama maoni kwa sababu mabadiliko ya aina hii si jambo la mtu mmoja, bali ni mchakato unaohusisha wadau mbalimbali.

Katika mchakato huo, maoni na mapendekezo kutoka kwa umma huwasilishwa kwa idara husika ili yachukuliwe na kuzingatiwa katika mchakato wa kufanya maamuzi na kuboresha huduma.

Asante. ^FL
 
Ila ni kweli unakubali kuwa mnalipisha wateja wenu kitita cha laki na 50 ya kitanzania kwa ajili ya kurekebisha kile kiremote cha plastic? Ambacho matumizi yake ni kubonyeza namba tu serious?
 
Mnachofanya ni utapeli wa wazi wazi.

Haiwezekani gharama ya kutekebisha hiyo remote ilingane na gharama ya kuweka umeme kwenye nyumba mpya.

Kitengo chenu cha Matengenezo pale chama - msasani ni kikundi cha kukusanya fedha za Watanganyika masikini
Habari, ndugu mteja.

Pole sana kwa changamoto hii. Tafadhali fahamu kuwa gharama ya rimoti kutoka TANESCO ni sawa katika ofisi zetu zote.

Iwapo ulikumbana na jambo la tofauti, tafadhali tujulishe ili tuweze kukusaidia zaidi.

Asante. ^FL
 
Ukifungua kava ya mita unaweza ingiza namba za LUKU bila rimoti, je umewahi kujaribu? Ikitokea umekosa/umechelewa kupata pesa ya kutengeneza rimoti unaweza ingiza umeme wako hapo.
kama mita yake ipo juu ya nguzo ni shida. Pia kufungua kava sio kesi ya wizi kweli maana makava si wanayafungaga kwa lakiri?
 
Wanatakiwa kutoa kidude kingine, ni kazi yao tanesco, huduma kwa wateja. Nenda kamuone meneja wa sehemu husika.
Habari, ndugu mteja.

Ni kweli, huwa tunafanya hivyo. Ndiyo maana inapojitokeza changamoto kwenye rimoti, ni muhimu ikaguliwe na wataalamu wetu ili kubaini tatizo na kutoa msaada stahiki.

Asante. ^FL
 
Habari, ndugu mteja.

Pole sana kwa changamoto hii. Tafadhali fahamu kuwa gharama ya rimoti kutoka TANESCO ni sawa katika ofisi zetu zote.

Iwapo ulikumbana na jambo la tofauti, tafadhali tujulishe ili tuweze kukusaidia zaidi.

Asante. ^FL
Nililipishwa 150000, ambayo mimi naamini kua ni utapeli wa serikali juu ya raia wake.
 
Habari, ndugu mteja.

Pole sana kwa changamoto hii. Tafadhali fahamu kuwa gharama ya rimoti kutoka TANESCO ni sawa katika ofisi zetu zote.

Iwapo ulikumbana na jambo la tofauti, tafadhali tujulishe ili tuweze kukusaidia zaidi.

Asante. ^FL
Gharama yake elekezi mpya ni shingapi?

Na taratibu na bei elekezi ya kutengeneza ni shingapi?
 
Hili jibu lenu limekaa kinyumbu sana na ndo maana tunawahujumu tunatumia umeme bure mwaka wa 7 huu🥹🥹eti mnajibu kabisa ni MAPENDEKEZO? Hivi nyie watumishi manyumbu huko ofisini mnazeekea ujinga badala mstaafu, ndo maana shirika linajiendesha kwa hasara kwa sababu na halitapata faida
Habari, ndugu mteja, na pole kwa mtazamo huo.

Tumejibu hivyo kwa sababu mabadiliko ya bei si uamuzi wa mtu mmoja, bali ni mchakato unaohusisha wadau mbalimbali na kuzingatia mambo muhimu.

Katika michakato kama hii, maoni kutoka kwa umma ni miongoni mwa mambo yanayozingatiwa. Ndiyo maana tunayapokea na kuyawasilisha kwa idara husika kwa ajili ya kuzingatiwa katika michakato ya kufanya maamuzi.

Ndugu wateja, tunawahakikishia kuwa maoni yenu tunayapokea na kuyafanyia kazi, kwani ni sehemu muhimu ya taarifa zinazotusaidia kuboresha huduma zetu.

Asante. ^FL
 
Habari, ndugu mteja.

Pole sana kwa changamoto hii. Tafadhali tambua kuwa tumepokea ujumbe wako na tumewasilisha maoni na mapendekezo yako kwa idara husika, ili yazingatiwe katika maboresho endelevu ya huduma zetu.

Asante. ^FL
Sasa semeni ni kweli hiyo remote ni 150000 au mnamhifadhi huyo hamnazo wenu?
Mimi niliambiwa ni 70000 na nililipa nikapewa kipya.
TOENI UFAFANUZI BEI HALISI YA REMOTE NI BEI GANI?
cc Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom