KERO Responded Inakuwaje gharama ya kutengeneza 'kidude' cha kuwekea umeme wa LUKU ni bei kubwa hivi?

KERO Responded Inakuwaje gharama ya kutengeneza 'kidude' cha kuwekea umeme wa LUKU ni bei kubwa hivi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Habari, ndugu mteja.

Tafadhali fahamu kuwa kuna aina mbili za rimoti: Rimoti ya njia moja (single phase): Shilingi 80,000/= na Rimoti ya njia tatu (three phase): Shilingi 120,000/=.

Malipo ya rimoti hufanyika kupitia namba ya malipo (Control Number) utakayopewa na TANESCO.

Asante. ^FL
Bado ghali sana

Ova
 
Acheni janjajanjaa
Maada inayolalamikiwa hapa ni kwanini remote ikiharibika mum tope mtanganyika mwenzenu 150000?.

Akikomaa wale mafundi wenu watake rushwa ili bei ipungue.
Ndugu mteja,

Tumekujibu hivyo kwa kuzingatia ujumbe wako kwamba ulikumbana na changamoto katika mojawapo ya ofisi zetu. Ndiyo maana tumekuomba utupatie taarifa zaidi ili tuweze kufuatilia na kukusaidia ipasavyo.

Kuhusu rimoti, gharama zake ni rasmi na ni sawa katika ofisi zote za TANESCO. Malipo hufanyika kupitia namba ya malipo (Control Number). Iwapo umekutana na tofauti yoyote ya gharama, tafadhali tujulishe ili suala hilo liweze kufanyiwa ufuatiliaji na hatua stahiki zichukuliwe.

Asante. ^FL
 
Ila ni kweli unakubali kuwa mnalipisha wateja wenu kitita cha laki na 50 ya kitanzania kwa ajili ya kurekebisha kile kiremote cha plastic? Ambacho matumizi yake ni kubonyeza namba tu serious?
Inashangazaa mnooo mnooo. Hii nchi utapeli uanzia kwa waliotakiwa kuzuia utapeli
 
ndo maana tunawahujumu tunatumia umeme bure mwaka wa 7 huu
Wizi sio sifa wala ujasiri bali ni kurudishana nyuma na kuumiza wengine kama huyu mleta mada.

Muhimu kujua ni kwamba wizi wa umeme uliofanya ni gharama ambayo Tanesco wanaifidia kwa kuongeza bei kwa huduma nyingine ili labda kukwepa kuongeza bei ya umeme.
 
Habari, ndugu mteja, pamoja na wadau wengine.

Tafadhali fahamu kuwa hairuhusiwi kwa mteja kufungua au kuifanyia mita marekebisho mwenyewe, kwani kufanya hivyo ni kinyume na taratibu na kunaweza kusababisha changamoto wakati wa ukaguzi wa mita na wataalamu wetu. Hivyo, tunakuomba uzingatie tahadhari hii kwa usalama na kuepuka usumbufu usio wa lazima.

Iwapo mita yako ina changamoto yoyote, tafadhali toa taarifa mara moja ili wataalamu wetu waweze kukusaidia. Unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba 180, ambayo ni bure kwa huduma kwa wateja, au kupitia jukwaa hili na kurasa zetu nyingine za mitandao ya kijamii.

Asante. ^FL
Ila nyie kututapeli 150000 zetu ni fresh kabisaa yaani
 
Ndugu mteja,

Tumekujibu hivyo kwa kuzingatia ujumbe wako kwamba ulikumbana na changamoto katika mojawapo ya ofisi zetu. Ndiyo maana tumekuomba utupatie taarifa zaidi ili tuweze kufuatilia na kukusaidia ipasavyo.

Kuhusu rimoti, gharama zake ni rasmi na ni sawa katika ofisi zote za TANESCO. Malipo hufanyika kupitia namba ya malipo (Control Number). Iwapo umekutana na tofauti yoyote ya gharama, tafadhali tujulishe ili suala hilo liweze kufanyiwa ufuatiliaji na hatua stahiki zichukuliwe.

Asante. ^FL
Hiyohiyoo 150000 ndio naipinga kua ni utapeli na kama ni sheria na taratibu, basi nazo ni za kitapeli
 
Hujajibu gharama elekezi za matengenezo/marekebisho ya remote
Ndugu mteja.

Hali ya rimoti na chanzo cha changamoto hubainishwa baada ya kukaguliwa na wataalamu wetu. Hivyo, ni muhimu fundi wetu kufanya ukaguzi na kutoa mwongozo kulingana na hali halisi ya rimoti.

Asante. ^FL
 
Habari, ndugu mteja.

Tumeeleza kuwa tumepokea ujumbe wake kama maoni kwa sababu mabadiliko ya aina hii si jambo la mtu mmoja, bali ni mchakato unaohusisha wadau mbalimbali.

Katika mchakato huo, maoni na mapendekezo kutoka kwa umma huwasilishwa kwa idara husika ili yachukuliwe na kuzingatiwa katika mchakato wa kufanya maamuzi na kuboresha huduma.

Asante. ^FL
Acheni wizi wenu pumbavu, ndio maana nilimchamba mfanyakazi wenu alivyoleta utapeli wake wa wazi wazi, na mkome kabisaa, pesa tunafuta kwa jasho, hatuziokoti. Wapuuzi nyie, mmekalia njaa tu.
 
Hii nchi sijuh uhuni itaisha lini?

Hv hili shirika ni huduma gani wanayoitoa kwa mwananchi hadi akajihisi fahari?
 
Habari, ndugu mteja.

Pole sana kwa changamoto hii. Tafadhali tambua kuwa tumepokea ujumbe wako na tumewasilisha maoni na mapendekezo yako kwa idara husika, ili yazingatiwe katika maboresho endelevu ya huduma zetu.

Asante. ^FL
Wewe uliyewekwa na TANESCO kujibu/kufafanua hoja za humu jamvini unapwaya.
Hukupaswa kuandika kuwa hoja umeichukua na kuipeleka idara husika ili yafanyiwe kazi.

Ulitakiwa kwanza, Kwa niaba ya shirika, umpatie mteja suluhisho la tatizo lake, period.
 
TANESCO hizo gharama ni kubwa mno na ni za kumkomoa mwananchi, haiwezekani remote tu ya kawaida ikawa gharama kubwa kiasi hicho. Huu ni ufisadi wa waziwazi
Habari, ndugu mteja.

Tunaelewa mtazamo wako kuhusu gharama za rimoti. Tafadhali fahamu kuwa gharama hizo ni viwango rasmi na ni sawa katika ofisi zetu zote. Hata hivyo, tumepokea maoni yako na tutayawasilisha kwa idara husika kwa ajili ya kuzingatiwa.

Asante. ^FL
 
Ndugu mteja tafadhali ambatanisha namba Yako ya Meter na Eneo husika ili tuweze fika kukushughulikia kikamilifu.
Asante.
451282.jpg
 
Habari, ndugu mteja.

Tunaelewa mtazamo wako kuhusu gharama za rimoti. Tafadhali fahamu kuwa gharama hizo ni viwango rasmi na ni sawa katika ofisi zetu zote. Hata hivyo, tumepokea maoni yako na tutayawasilisha kwa idara husika kwa ajili ya kuzingatiwa.

Asante. ^FL
Yani remote mpya 80,000 kwa 120,000 halafu matengenezo mnamlipisha mtu 150,000 serious?
 
Wizi sio sifa wala ujasiri bali ni kurudishana nyuma na kuumiza wengine kama huyu mleta mada.

Muhimu kujua ni kwamba wizi wa umeme uliofanya ni gharama ambayo Tanesco wanaifidia kwa kuongeza bei kwa huduma nyingine ili labda kukwepa kuongeza bei ya umeme.
Jibu ni moja tu mkuu Kila anaepata nafasi ya kubutua sehemu na abutue tu huruma sio malezi😡hata hao wanasiasa wanapiga ufisadi kwa sababu wapo kwenye nafasi ya kuzipiga pesa sasa wewe mlala hoi tetea na huku Kodi zinapanda Kila siku na mbunge wako anapata posho Kila wiki.

NB; Rushwa inakuwa mbaya kama haujashiriki ila kama ukishirikishwa kwenye Rushwa lazima uitetee kwa nguvu zoteeeee🙏
 
Back
Top Bottom