umenikumbusha jambo muhimu sana, Emagence Agents wenu uwa anadai remote ikiwa mbovu au ikiwa haipo kipindi wanabadirisha main meter wanakataa kukupatia charge ya remote ya meter mpya waliyofunga kwa kisingizio remote ya mwanzo ilikuwa mbovu sana huu nao ni wizi na njaa, mimi nakumbuka walitaka elfu 5 nikawakatalia na wakaondoka na hile charge cha remote ya meter mpya waliyobadirisha, Binafsi nikaona sio kesi kwasababu inafanana na ya simu mbaka now natumia charge ya simu.
Pia kuhusu umiliki huo huo unauongelea hapa kifaa hicho kikiaribika yaani remote ya meter na ukiipeleka kwa fundi mtaani kwako inakuwa ni kosa na unaweza kuangushiwa kesi kubwa sana la uhujumu Uchumi, sasa hii imekaaje kama mwenye umiliki hayuko na haki ya matengenezo ya kifaa chake anachomiliki kwa kisingizio anaweza kuifanyia modification, mwisho unapewa kesi kisha hapo hapo amjaweka utaratibu wa matengenezo nyinyi wenyewe, hivi hamuoni kana kwamba huu ni ubadhirifu..?
Mimi natoa ushauri wangu wa moja kwa moja kwamba, "Gharama za Matengenezo ziondolewe au zipungue kwa kiwango kinachokidhi la sivyo mmiliki wa kifaa hicho ambae ni mteja awe na haki ya kutengeneza kokote atakako, Kwa fundi yeyote na ni mahali popote ilimradi tu kipone" Pia Remote nyingi zinakufa si kwa phisical Issues ambazo mteja anaweza kusababisha bali kwa Software glitch or Network connectivity kati ya Remote na Main meter.
Mfumo wa utawala na Usimamizi wa Tanensco unapaswa kuangaliwa kwa kina, maana unaweza kuumiza haki za watu, kucheleweshwa kwa maendeleo ya watu wanaotumia nisharti ya umeme, na kuzalisha rushwa hasa kwa maafisa wa Tanesco kutaka pesa kwa kisingizio kisichokuwa na kichwa wala miguu.
Kumbuka:
Remote nyingi zinakufa si kwa phisical Issues ambazo mteja anaweza kusababisha bali kwa Software glitch or Network connectivity kati ya Remote na Main meter.