KERO Responded Inakuwaje gharama ya kutengeneza 'kidude' cha kuwekea umeme wa LUKU ni bei kubwa hivi?

KERO Responded Inakuwaje gharama ya kutengeneza 'kidude' cha kuwekea umeme wa LUKU ni bei kubwa hivi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mtoa mada ni mjinga, hujui njia za mkato, CIU zinapatikkana tele ni wewe na ujanja wako tu
Inakuwaje jamaa awe mjinga kisa hajui njia ya mkato, n sawa na kumuona mtu sio mtenda maovu na kusema huyu n mjinga kisa hafanyi hayo maovu.
 
Acha kujibu kama ROBOT, eleza ni kwanini mnachaji 150,000 kwa matengenezo ya remote tu? Huo sio UTAPELI wa mchana kweupe? Jibu hilo.
Habari, ndugu mteja.

Kama tulivyofafanua awali, upangaji wa bei hufuata mchakato unaohusisha wadau mbalimbali na hauamuliwi na mtu mmoja au taasisi moja pekee. Katika mchakato huo, mambo mbalimbali huzingatiwa, yakiwemo mazingira ya kiuchumi, kisera, kijamii na kisheria.

Vivyo hivyo, pale kunapokuwa na mapendekezo ya kufanya mabadiliko ya bei, taratibu na mifumo husika hufuatwa kabla ya maamuzi kufanyika.

Hivyo, tunapokea na kuthamini maoni yako, pamoja na ya wateja wengine, kwani ni sehemu muhimu ya mrejesho unaoweza kusaidia wadau husika katika tathmini na maboresho ya huduma.

Asante. ^HN
 
Mwenyewe nimetoka kulipa juzi 80k tshs baada ya kukimbizana nao sana vifaa vyenyewe vibovu kintumika tu kuingiza umeme ila mabatton muda wowote yanagoma mara kutu mara kijizime, huu ni wizi wa wazi
 
Hili shirika ni la kipumbavu mno mwezi wa 8 wamekuja kijijini kwetu wakatuunganishia umeme na wakatuwekea unit 10 za ofa ila wakatuahidi kabla ya wiki moja watatutumia control number ili tulipie 27000.....chakushangaza hadi leo hawajatutumia hizo namba na umeme umeshaisha na kwahali hiyo hauwezi kununua umeme kwahiyo tupo Gizani tu... huwa tunajiuliza hivi kuna aliewalazimisha mutuletee umeme?
 
Hizo unit 10 huwa sio za ofa ungeuliza vizuri na kila mita mpya huwa zinawekwa ukizitumia unazilipa! Acha kulalamika fuata utaratibu!
 
Attachments

  • PXL_20261006_043028058.RAW-01.jpg
    PXL_20261006_043028058.RAW-01.jpg
    291.9 KB · Views: 7
  • PXL_20261006_042834071.RAW-01.jpg
    PXL_20261006_042834071.RAW-01.jpg
    294.2 KB · Views: 8
TANESCO kwa hio picha hapo post #217 nimekiharibu au kimeharibika,remedy yake ni nini?
Habari XYZ987.

Asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali jaribu zoezi lifuatalo kwa usaidizi, nunua betri mpya kisha weka kwenye rimoti yako ya kuingizia umeme na chomeka kwenye soketi ndani kwako kisha ingiza 755204 ok kisha ingiza mita namba bila namba mbili za mwanzo(43) kisha bonyeza OK, halafu ingiza token zako.

Iwapo utakua umeshalifanya zoezi hili hapo awali tafadhali tupatie namba ya taarifa kwaajili ya msaada zaidi.^RS
 
Back
Top Bottom