KERO Responded Inakuwaje gharama ya kutengeneza 'kidude' cha kuwekea umeme wa LUKU ni bei kubwa hivi?

KERO Responded Inakuwaje gharama ya kutengeneza 'kidude' cha kuwekea umeme wa LUKU ni bei kubwa hivi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kinachotakiwa ni mfumo mpya wa umeme kuingia direct unaponunua bila kujaza namba.
Ndugu mteja, tayari tumeanzisha huduma hii kupitia kampeni ya mita janja, ambapo mteja anaponunua umeme, tokeni huingizwa moja kwa moja kwenye mita.

Kwa sasa, kampeni hii inaendelea, na wateja wanabadilishiwa mita bila malipo na kwa hiari. Endapo eneo lako litafikiwa, utajulishwa.

Aidha, unaweza kutembelea ofisi ya TANESCO iliyo karibu nawe kwa msaada na mwongozo zaidi.

Asante. ^FL
 
Habari, ndugu mteja.

Pole sana kwa changamoto hii. Tafadhali tambua kuwa tumepokea ujumbe wako na tumewasilisha maoni na mapendekezo yako kwa idara husika, ili yazingatiwe katika maboresho endelevu ya huduma zetu.

Asante. ^FL
Iweje matengenezo yawa gharana? Yupo mtu ataweza kiharibu makusudi? Mteja arekebishiwe bure au apewe mashine nyingine! Me waliniambia 90k nyambaaaf...
 
Kuchukulia tatizo la watu wawili kwa umma wote nafikiri sio sawa.

Angalia iadi ya wachangiaji humu ambao wanachangamoto hiyo, je ni wote wazembe/waliwapa watoto kuchezea?

Kuna maelekezo rasmi kwamba kifaa hicho kitatumika kwa muda gani? Hufikiri kuw huenda, vinamaliza muda wa matumizi?
Uko sahihi mkuu. Watu wachache hawawezi kufanya wotee tuumie
 
Sasa semeni ni kweli hiyo remote ni 150000 au mnamhifadhi huyo hamnazo wenu?
Mimi niliambiwa ni 70000 na nililipa nikapewa kipya.
TOENI UFAFANUZI BEI HALISI YA REMOTE NI BEI GANI?
cc Pascal Mayalla
Wewe uliambiwa ni 70,000 mimi nimepiga simu ijumaa wakaniambia 80,000 kupata kipya na mwingine kaambiwa kurekebisha ni 150,000.

Shirika moja majibu tofauti, kuna wizi hapo!
 
Yah! Hao TANESCO wanatakiwa wahamie huku.

Mana si wengine hivyo vidude baadhi ya namba hazibonyezeki halafu mtihani uliopo ukinunua umeme wanakupa namba za kuweka 20.

Yaani mtu unahangaika nazo mpaka basi na ilivyo ukiwa unahangaika kuweka namba ikichukua sekunde kadhaa haijaandika zile namba ulizohangaika nazo mwanzo zinajifuta unaanza upya.

Mie pia nashauri waende na teknolojia tukinunua umeme basi unaingia moja kwa moja.
Habari Shadeeya, asante kwa kuwasiliana nasi,

Tayari tumeanzisha huduma hii kupitia kampeni ya mita janja, ambapo mteja anaponunua umeme, tokeni huingizwa moja kwa moja kwenye mita.

Kwa sasa, kampeni hii inaendelea, na wateja wanabadilishiwa mita bila malipo na kwa hiari. Endapo eneo lako litafikiwa, utajulishwa.

Aidha, unaweza kutembelea ofisi ya TANESCO iliyo karibu nawe kwa msaada na mwongozo zaidi.

Asante. ^FL
 
Sio wao (watu) nadhani wanatumia lile dubwana (AI) kuandika hivyo.
Nimeona majibu nikajua tu hayo ni Auto reply.

Sasa mshirika mkubwa kama huo hata customer services zinakuwa ngumu si bora tu wakae pembeni mkoloni mweupe aingie kazini?
 
Habari, ndugu mteja.

Tumeeleza kuwa tumepokea ujumbe wake kama maoni kwa sababu mabadiliko ya aina hii si jambo la mtu mmoja, bali ni mchakato unaohusisha wadau mbalimbali.

Katika mchakato huo, maoni na mapendekezo kutoka kwa umma huwasilishwa kwa idara husika ili yachukuliwe na kuzingatiwa katika mchakato wa kufanya maamuzi na kuboresha huduma.

Asante. ^FL
Hovyo kabisa!

Kwa hiyo mjikusanye conference room wiki nzima mkiokota posho just kujadili kama bei ya ku-repair hizo remote ipunguzwe au isipunguzwe?hilo si jambo la kuamua mkurugenzi tu hilo ndani ya sekunde mambo yanabadilika?
 
Back
Top Bottom