Inasikitisha sana, kuna mtu ameomba kazi ya trainee akiwa na miaka 35

Mzeebaba ungetaja na kitengo unachofanyia kazi Mkuu ili tukuelewe vizuri.. Kama uyo Boss wako ni Baba ako endelea kushangaa ila kama na wew umeajiriwa hapo basi jua possibility ya wew kuja kumshangaza mwingine ni kubwa..just focus on your plate!
Safi sana
 
Maisha ni safari ndefu Sana Muombee tu apate kazi.
 
Serikalini wakitoa matangazo ya kuomba ajira mwisho 45, 35 unaanzisha uzi kweli.
 
Life kila mtu na mda wake mie nilienda driving school na miaka 25 nikiwa na majonzi kuwa nimechelewa kujua kuendesha gari mana kitaa watoto wa kishua walikua wanaendesha magari wakiwa na miaka 17 huko...

Aminj mzee kufika pale namkuta jamaa ana miaka 47 yupo driving school ndio kaagiza gari yake ya kwanza na yupo very happy kwa hyo achievement toka siku hyo nikakubali life halina kuchelewa na usiishi kwa kujilinganisha na wengine...
 
Aisee!

Nakumbuka miaka hiyo ulipo kuwa pale jalalani (udsm) ukisoma electrial engineering wakala kichwa ukaja kuibukia kwenye economics!

Then ukasota sana kwenye ajira ..ukaenda TRA wakakula kichwa mwishoe ukaja ibukia kwenye ajira za serikali huko kigoma huko!

Leo umekuja unashangaa mtu kuomba ajira akiwa na miaka 35! Kweli dunia inakimbia kwa kasi!
 
Siku zote wale wanaopitia shida au mazingira Magumu,wakifanikiwa kidogo tu ndo huanza kuwa kama huyu!! Ukijaribu kuchunguza hata wale tuliokulia mazingira ya kimaskini au yenye changamoto kubwa,tukija kufanikiwa mbeleni HUKO huwa tunakuwa na dharau sana hasa sisi wadada na wanawake!! Ulimbukeni unakuwa mkubwa kuliko Hekima✍️
 
Mimi mwenyewe nina miaka 36,lkn ramani ya maisha bado haijasoma, naendelea kumuomba MUNGU anisaidie niweze kufanikiwa hata km ni kwa kuchelewa.Mshukuru MUNGU wewe uliyefanikiwa mapema.
 
We unashangaa mwenye 35!!?
Nchi ngumu hii,mie Nina 51 na Bado nagombsnia ajira na watoto wa 90s,sasa ngoja nifikishe abiria bunju,harafu naenda kwenye usaili!!?mfuruki alikuwa na 70+na bsdo alikuwa utumishi! Mkuchika hata mgongo unaanza kupinda lakini Bado yupo serikalini
 
Mpe ukweli ili ajifunze.
 
Nikiwa kidato cha kwanza shule ya sekondari Malangali Iringa kuna mshkaji alikuwa smart sana kichwani ila aliishia form 1 tu, tunapofungua shule ile Januari hakurudi tena kuendelea kidato cha 2 sababu ya kukosa ada, na ada ilikuwa ni shilingi elfu 70 tu, kwao ilikuwa ni Mbozi, Mbeya anaitwa Elia jina la pili nimelisahau. Nilisikitika sana.
 

Ipo mifano mingi mkuu, Hwadmaster wa shule niliyosoma O-Level alikuwa mtu mzuri sana...alikuwa anatoa fursa ya kuwaacha warejee masomo wale waliokuwa wanakosa ada...

Kuna wengine walikuwa wanapewa vibarua nyakati za likizo kama kukata nyasi, kuhudumia ng'ombe wa shule n.k halafu wanalipwa ujira kidogo...
 
Mtoa mada sijui una hali gan huko ulipo, kwa comments hizi za wadau nahisi umejiona bwege Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…