Inasikitisha sana, kuna mtu ameomba kazi ya trainee akiwa na miaka 35

Perry nakumbuka enzi zile ulivyojiunga na UDSM hatukulala humu.

Anyway, hongera kwa kupata ajira.
Hata mimi nakumbuka sana

Anaonekana ni jamaa ni majivuno na dharau

Yeye kufanikiwa kwa njia rahisi anahisi wengine ni vilaza (hatujui yeye kafanikiwi kivipi)

Aache kujifanya kama haijui Tz

Watu wana elimu safi tu still wan struggle hadi leo wapate ajira inayoeleweka yeye anashangaa kana kwamba kaja Tz jana.

Yeye kamshangaa jamaa wa miaka 35 ,mimi nimemshangaa yeye!!![emoji15]
 
Naona watu mmenielewa vibaya
Iko hivi,mimi sijadharau mtu,kilichonishangaza ni hii kuona mtu wa 35 years anaomba kazi ya Trainee,kwangu ni kitu kigeni kwa sababu nimezoea kuona watu wanaoomba hizi nafasi za kuwa Trainee ni vijana wadogo wa chini ya miaka 30.
Anyway jamaa kahudhuria usaili na tumeonana, I hope Mungu atamsaidia.
 
Bado unaendelea kuandika utumbo tu
 
Hahahahaha jamaa anadhani tumemsahau na tambo zake za udsm
 
Inasikitisha kwasababu wewe una kazi tayari....ila kiuhalisia ni suala la kawaida hapa nchini
Huo si ukawaida. Stop normalizing matatizo yaonekane ni normal. That not normal

Thats is state ya ajira nchini ilivyo enda chini.
 
Naona wana wamekushambulia sana kwa hii post yako mkuu. Sasa ili kuwaonyesha kuwa we unaelewa situation ya mwana basi msaidie huyo mwana apate internship na ikiwezekana mpambanie apate ajira kabisa.
Hilo ndio la msingi sio kushangaa
 
Watanzania tuna matatizo sana.kwa hiyo kitu kama ni kigeni kwangu siruhusiwi kushangaa,kisa nitaonekana nadharau watu?
Bado unaendelea kuandika utumbo bora unyamaze tu, kwahiyo ukija huku uswahilin kwetu ukaona watu wanakula ugali kwa dagaa kila siku wiki nzima utakuja hapa kuanzisha uzi kisa kwenu mlo mmoja tu una mboga saba?
 
Bado unaendelea kuandika utumbo bora unyamaze tu, kwahiyo ukija huku uswahilin kwetu ukaona watu wanakula ugali kwa dagaa kila siku wiki nzima utakuja hapa kuanzisha uzi kisa kwenu mlo mmoja tu una mboga saba?
Ndio maana ukienda ulaya nao wanashangaa inawezekana vipi sisi waafrika tunanaishi under 1 dollar kwa siku.
Kwa hiyo tusifundishane maisha,kitu kilicho strange kwangu kinaweza kikawa ni cha kawaida kwa mtu mwingine and vice versa.
Hakuna mahali nimeonyesha kumdharau mtu hapa kwenye huu uzi kama mnavyojaribu kuonyesha.
 
Wapi nimemuoffend mtu yeyote hapa kwenye huu uzi nionyeshe?
Muhimu msaidie huyo jamaa apate kazi kama upo kwenye position ya kuweza kumsaidia,na hilo tu ndio litakalo msaidia huyo jamaa kwenye maisha yake.
 
Mungu kamuandikia kila mtu njia yake

Usisikitike

Mnaweza wote mkatangulia kaburini na mkamuacha anaendelea na maisha yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…