Inasikitisha sana. Kwanini Azam Media inaendekeza udini namna hii?

Inaonekana ndugu we nyimbo za daimond ali kiba harmonize mboso dully sykes mwana FA mzee yusuph hauziskilizi kabisa
 
Waacheni waitimize imani shirki na non Muslim Mo alikataa hadi tu pale utakapoona huwezi na ukishirikiana nae ni kiunafiki tu unapokuwa dhaifu na ukiimarika unaondosha dini imeruhusu hivyo... Even Egypt iliingia makubaliano na Israel baada ya kushindwa vita
 
Ungemshauri Mzee Bakhresa tangu hizo enzi anajitafuta ingekuwa bora. Vinginevyo huu ushauri wako ni wa kupuuzwa.
 
Kwanza Mzee Bahressa mwenyewe ni mtu peace sana. Hana upendeleo hata kidogo. Tatizo ni hao/family/ndugu waliopewa dhamana ya kusimamia biashara zake.

Binafsi sipendezwi na aina yeyote ya ukabila, udini, itikadi au ukanda na ndio maana hata kipindi cha Mengi nilishakosoa sana tu.


Pia tunatakiwa kuiga mfano wa Mama yetu jinsi asivyokuwa na upendeleo, anachojali ni weledi , utendaji na uadilifu wa mtu. Kwanini tusifuate mfano huu wa Mama.
 
Inaonekana ndugu we nyimbo za daimond ali kiba harmonize mboso dully sykes mwana FA mzee yusuph hauziskilizi kabisa
Muulize Diamond ni nani aliyemuingiza studio wakati wa nyimbo yake ya Nenda Kamuambie
 
Bila kusahau clouds waachane na ukabila

Wasafi waachane na u sodoma na gomora
 
Hii nchi kuna haja ya kupitisha sheria mtu akitaja udini na ukabila peleka mahamani kuna watu wanaitakia hii nchi mabaya. Hizi tabia siku za karibuni zimekuwa shida sana kwa bahati mbaya serikali wamekalia kimya tu, haya ni mambo tunahitaji kuyakemea kwa nguvu zote hata kama tunatofautiana kwenye mambo mengine ya msingi sio shida lakini tusilete visababu vya udini wala ukabila.
 
Binaadamu ni viumbe wa ajabu sana ,huo udini umetoka wapi , mimi natumia dstv na channel za kikristo ni nyingi na hardly kupata za kiislamu, ila sioni kwamba ni udini au tatizo, acheni chuki yule ni mfanya biashara , hawezi kufanya kitu ambacho kwake kitaharibu biashara yake, ni wivu na chuki tu vinawasumbua
 
Exactly kuna watu wajinga sana
 
True, but learn to mind your own business!

Kwenye mashirika ya ki Catholic hawaajiri nje ya M catholic, leave alone U Kristo, tena lazima awe mshirika wa kutimiza taratibu zote.

Mimi ni Mkristo kabisa, ila wakristo nafikiri ni wabaguzi zaidi....

 
Matatizo siku zote hayawezi kutatuliwa kwa njia hii ya ubabe na vitisho. Isipokuwa kwa kutenda haki na pia kufanya mambo kwa usawa.
 
Anzisha media yako ,madai Yako ni yakipuuzi hayana msingi wowote eti "anaweka channel zisizo za dini yake kwa shingo upande" unaweza kuweka ushahidi wowote au picha ya aliweka channel hizo channel hulu shingo ikiwa upande ?
atuonyeshe hiyo shingo upande 🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…