Inawezekana Jaribio la Kumuua Lissu lilimkasirisha sana Mungu

Inawezekana Jaribio la Kumuua Lissu lilimkasirisha sana Mungu

Namba 1 kipindi cha Lissu- Deportivo la Corunia ilifanya yake

Namba mbili kipindi cha Lissu- Alijawa na huruma akaenda kumsalimia Lissu nairobi Mungu akampa Urais

Katibu Mkuu kiongozi kipindi cha Lissu- Huyu ndo anasimamia shughuli za Tiss nae deportivo la corunia ilifanya yake

Kipilimba na Musalika- DG na DDG TISS- hawa wote hawapo kwenye nafasi zao

Mambosasa- Huyu alizuia maombi juu ya Lissu sasa haijulikani kama kastaafu au la

Balozi sokoine- Huyu aliondolewa ubalozi ubelgiji baada ya kwenda hospitali kumsalimia Lissu. Leo ni Katibu Mkuu mambo ya nje cheo kikubwa kuliko balozi

Kalemani ambae inasemwa alikuwa jirani wa Lissu na alihusika kutoa cctv camera za tukio la Lissu nae sio waziri tena

Job Ndugai- Huyu alizuia pesa za matibabu za Lissu na kuzuia mshahara wa Lissu, Kwa yanayoendelea sasa CCM inaonekana hata mwezi machi hakanyagi akiwa Spika. Katiba inasema spika akipata uspika kutokana na kuwa mbunge akipoteza ubunge anapoteza uspika. Je, CCM watamvua uanachama hivyo kukosa ubunge na uspika? Tusubiri

Waliotenda wema kwa Lissu, Mungu kawabariki, waliotenda ubaya kawaadhibu! Sasa Je jaribio la kumuua Lissu lilimkasirisha sana Mungu?

Mwisho Naona Lissu akirejea Mama Samia atamteua kuwa Mbunge ili kumfuta machozi!
Tuendelee kutafakari matendo makuu ya Mungu
 
Mwenzako kaweka hoja ya kufikirika wewe unamwita mpumbavu?. Mpumbavu Hana muda wa kufikiri Jambo la kufikirisha Kama hili. Hoja hujibiwa kwa hoja na sio matusi.
We km unaona alichoongea huyo kina make sense sina haja kukujibu Mungu ashughulike na petty issue za wachumia matumbo .
 
Umejiuliza kwanini hali imekuwa hivyo? is it by chance? Mwenzako amewaza kwa kutumia akili.

Anayewaza kwa kutumia akili hawezi KUJA na andiko kama hilo au hata KUKUBALIANA tu na andiko kama hilo. Vinginevyo, kuwaza kwa kutumia akili kungekuwa completely meaningless!

Katika Isa 55:8-9 SUV imeandikwa: Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
 
Swali gumu hapa ni kuwa gari la Lissu lililoshambuliwa lilikuwa left or right handed?

Kama ni magari yetu haya ambayo bos hukaa kushoto, iweke Lissu aliumia mguu wa kulia badala ya kushoto ili hali dereva wake hakuumia?

Wajuvi wa mambo hebu andikeni kwa vina nipate kuelewa.

Povu si busara wapendwa.
Wewe unauliza "wajuvi wa mambo" wa wapi? Humu JF?

Nakushauri upeleke maswali haya polisi ambao ndiyo wenye dhamana ya kuchunguza na kutoa ripoti ya jinai kama hii...

Ni ajabu sana kuwa, polisi hadi leo hawataki kufanya kazi yao huku nao wakigeuka kuwa wambea na wazushi...

Si ajabu na wewe ni miongoni mwao...!!
 
Shetani alishapewa hukumu ya milele anacho subiria Ni wafuasi wake wanao tenda dhambi ili wakatupwe wote motoni milele. Ndio maana shetani Ni mshitaki wetu mbele za Mungu, ili apate watu wengi wa kuungua naye na kupata mateso pamoja naye. Yule tayari alishakifa maana yupo kuzimu anaposubiria watenda dhambi wanaokufa ili wakateseke naye.

Utakuwa hujui ukichoandika!
 
Kijana hata kama una njaa, jaribu kutumia njia nyingine nzuri ya kujipatia riziki ya halali. Acha kumuhusisha Mungu na upuuzi wako. Ila kama wachawi na waganga wa kienyeji nao hujifanya kumtanguliza mungu ktk ushenzi wao, basi sishangai kwa mleta mada kumuhusisha ktk upuuzi wake. Najua katibu mkuu atakutumia bando na buku 5 ya kula, lkn huko ulipo utaendelea kuteseka, kwa kosa la kuuza utu wako sababu ya njaa yako.
Nje ya mada hii
 
Hivi wewe unamjua Mungu kweli? Unadhani Mungu ni kama mwanadamu kiasi kwamba kuna matukio huwa yanamshitukiza bila yeye kujua?
Kwa taarifa yako Mungu ni "All knowing", anajua mambo yote hata kabla hayajatokea, kwa hiyo hakuna kitu chochote kinachoweza kutokea na kumrusha roho!
Halafu kwa nini ashitushwe na tukio la lisu peke yake, yeye ni nani? Naye si binadamu wa kawaida tu kama wengine; mdhambi tu kama wewe na watu wengine walivyo?!
Msimuingize Mungu kwenye mambo yenu ya kipuuzipuuzi.
Adam na Eva walipokula tunda la kati Mungu alikasirika na kuwafukuza, kwanini alikasirika wakati alikuwa anajua hilo?
 
Ni yeye
ELIAH_NGASE%F0%9F%85%B0_on_Instagram%3A_%E2%80%9CNiyeye!!!!%E2%80%9D%22_.jpg
 
HAPANA!!.... MUNGU YEHOVA si exclusive kwa kiasi hicho na kwa namna yoyote....

Yeye ndiye aliyesema kwa kila mtu "USIUE..."

Kwa kifupi sana ni kuwa, mtu yeyote kumuua mtu mwenzake is exclusively a BIG SIN....

However, na bahati njema ni kuwa, this sin is also forgivable just like any other sin...

Labda tunachoweza kukubaliana ni hiki, na ndivyo afanyavyo BWANA MUNGU siku zote...

Kwamba, ALITAKA na ANATAKA na ATAENDELEA kulitumia tukio hilo kwa ajili ya kutufundisha na hususani kuwafundisha somo mahususi watawala na wenye mamlaka wa serikali za kidunia (Tanzania) kitu fulani...

Kwa hiyo, Bwana Mungu Yehova aliruhusu risasi 16 ziingie ktk mwili wa huyu ndugu LAKINI Mungu aliifunga roho ya mauti ili kumfanya mtu huyu awe ZANA YA KUFUNDISHIA...!

Unfortunately, baadhi yao ni wajinga na wenye mioyo migumu kujifunza na kuelewa ili wajue yawapasayo kufanya na namna ya kuendelea mbele...

That's why wengine wanajifunza in a hard & costly way...

Mathalani, hayati John P. Magufuli moja ya kosa lililogharimu maisha yake hata kifo ni hili....

Huyu Paul Makonda naye kwa hakika kabisa ataishia pabaya zaidi kuliko alipo sasa kama hatapata akili ya kutubu na kuomba msamaha kwa muumba wake...
Hivi mwanadamu anapojipa kazi ya uungu hujikuta nae ni Mungu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namba 1 kipindi cha Lissu- Deportivo la Corunia ilifanya yake

Namba mbili kipindi cha Lissu- Alijawa na huruma akaenda kumsalimia Lissu nairobi Mungu akampa Urais

Katibu Mkuu kiongozi kipindi cha Lissu- Huyu ndo anasimamia shughuli za Tiss nae deportivo la corunia ilifanya yake

Kipilimba na Musalika- DG na DDG TISS- hawa wote hawapo kwenye nafasi zao

Mambosasa- Huyu alizuia maombi juu ya Lissu sasa haijulikani kama kastaafu au la

Balozi sokoine- Huyu aliondolewa ubalozi ubelgiji baada ya kwenda hospitali kumsalimia Lissu. Leo ni Katibu Mkuu mambo ya nje cheo kikubwa kuliko balozi

Kalemani ambae inasemwa alikuwa jirani wa Lissu na alihusika kutoa cctv camera za tukio la Lissu nae sio waziri tena

Job Ndugai- Huyu alizuia pesa za matibabu za Lissu na kuzuia mshahara wa Lissu, Kwa yanayoendelea sasa CCM inaonekana hata mwezi machi hakanyagi akiwa Spika. Katiba inasema spika akipata uspika kutokana na kuwa mbunge akipoteza ubunge anapoteza uspika. Je, CCM watamvua uanachama hivyo kukosa ubunge na uspika? Tusubiri

Waliotenda wema kwa Lissu, Mungu kawabariki, waliotenda ubaya kawaadhibu! Sasa Je jaribio la kumuua Lissu lilimkasirisha sana Mungu?

Mwisho Naona Lissu akirejea Mama Samia atamteua kuwa Mbunge ili kumfuta machozi!
Naunga mkono hoja, yaani ni kweli kabisa.
 
Ukiwa chukizo mbele za Mungu anakuondoa na mifano ipo mingi. Kasome pia mapigo ya wa misri, sodoma na Gomorrah etc. Pia Kuna Moto wa milele kwa watenda dhambi. Haiwezekani Kuna raia wameuawa kwenye nchi na haijulikani wapo wapi mpaka leo Halafu uniambie Mungu anafurahia. Mungu hutoa adhabu mwenyewe kwa njia ambazo mwanadamu hawezi kuijua, mpaka atafakari kwa kina.

Pia punguza ukali wa maneno mkuu. Mto mada amejaribu kuvuta events mbalimbali na kizioanisha na tukio la kupigwa risasi Lissu. Mtoa mada hajatukana mtu, wewe umekimbilia kumtukana bila kujibu hoja. Kuna Jambo Mtume Mwingira alilisema ya kwamba Lissu Ni mshindi, nilikuja kudhibitisha kwenye uchaguzi wa 2020, baada kuiba uchaguzi Urais haukudumu hata miezi mitatu ukafikia kikomo. Ili Jambo lilinifanya niogope Sana.

bible msiisome kama kitini cha marejesho ya vikoba.

kizazi cha nuhu,ruttu,Mungu amefanya mambi yale na baada ya hapo kuahidi kutorudia tena kuteketeza viumbe wake kwa sababu ya dhambi aina yoyote tu,isipokuwa siku ya ufufuo.

maneno yenye ukali yanasaidia kumrudisha mtu kwenye misingi ya kawaida ya kufikiri na kutenda,kuibiwa uchaguzi ccm haijaanza 2020 labda kama umezaliwa mwaka huo.
 
Acha kuongopea watu kwa maslahi ya kisiasa. Kifo Ni Moja ya adhabu za Mungu. Mungu alimwambia Adam ukila tunda la mti was katikati Hakika utakufa. Na baada ya Adam kula lile tunda Mungu alimwambia Adam ya kwamba mavumbini ulitoka na mavumbini utarudi. Mungu aliwaadhibu kwa kifo sodomah na ghomorrah, Mungu aliwaadhibu wazaliwa wa Kwanza katika misri kupitia kifo, etc. Kifo Ni Moja ya adhabu anayotumia Mungu ukifanya machukizo yaliyozidi.

kwahiyo wewe usiye nwovu unatarajia kuishi miaka mingapi ndugu yetu roho mtakatifu[emoji23][emoji23]

mnapenda kuiparamia bible kama mti wa mpera na mmevaa madela huku hamjavaa chupi.
 
Angesifia the gvrnt of green party tungesema kweli ana njaa lakin Lissu is neither in the ruling party nor in the government nani wa kumlipa?
 
Swali gumu hapa ni kuwa gari la Lissu lililoshambuliwa lilikuwa left or right handed?

Kama ni magari yetu haya ambayo bos hukaa kushoto, iweke Lissu aliumia mguu wa kulia badala ya kushoto ili hali dereva wake hakuumia?

Wajuvi wa mambo hebu andikeni kwa vina nipate kuelewa.

Povu si busara wapendwa.
Basi assume alijipiga mwenyewe hizo risasi
 
Kijana hata kama una njaa, jaribu kutumia njia nyingine nzuri ya kujipatia riziki ya halali. Acha kumuhusisha Mungu na upuuzi wako. Ila kama wachawi na waganga wa kienyeji nao hujifanya kumtanguliza mungu ktk ushenzi wao, basi sishangai kwa mleta mada kumuhusisha ktk upuuzi wake. Najua katibu mkuu atakutumia bando na buku 5 ya kula, lkn huko ulipo utaendelea kuteseka, kwa kosa la kuuza utu wako sababu ya njaa yako.
Unataka kusema kupigwa risasi Lissu Nitendo la kidini na kiimani kwenu?
Utakuwa unasali nyumba za mashetani wewe na damu za watu kwako/kwenu ni kiburudisho!!
All I can say is GTH (Go To H...)
 
Kuuwa mtu kisa kakukosoa ni kiwango cha chini sana cha kufikiri.
Killing haiwezi kuwa suluhisho la mda mrefu.
Unawaua watu kisha nawe unakufa mnaenda kutana huko.
 
Back
Top Bottom