Inawezekana Jaribio la Kumuua Lissu lilimkasirisha sana Mungu

Inawezekana Jaribio la Kumuua Lissu lilimkasirisha sana Mungu

Kijana hata kama una njaa, jaribu kutumia njia nyingine nzuri ya kujipatia riziki ya halali. Acha kumuhusisha Mungu na upuuzi wako. Ila kama wachawi na waganga wa kienyeji nao hujifanya kumtanguliza mungu ktk ushenzi wao, basi sishangai kwa mleta mada kumuhusisha ktk upuuzi wake. Najua katibu mkuu atakutumia bando na buku 5 ya kula, lkn huko ulipo utaendelea kuteseka, kwa kosa la kuuza utu wako sababu ya njaa yako.
Lakini Mimi naona alichokiandika kina mantiki hata Kama ukweli unaweza kuwa sio asilimia Mia. Hakuna uhusiano Kati alichoandika na njaa, mtu mwenye njaa hawezi kuwa na akili ya kuandika Mambo mazito Kama hayo. Ila yote yaliyotokea mpaka awamu ya tano ikatoka Ni karma ya Lissu. Na karma ya Lissu itaitesa Sana serikali mpaka itubu.
 
Lissu hajawahi kuwa na njaa, hadharani alimkejeli Magufuli kuhusu kumteua, alimwambia kuwa yeye sio kama wale wa majalani

Lissu kujiamini kwake hakuna ulinganifu nchi hii so hawezi kukubali uteuzi wa Samia.
Ukitaka kumtendea wema Lissu tena haki kwa taifa lako. Tawala kwa misingi ya sheria haki na amani. Ukiweza hilo utamtuliza Lissu. Teuzi kwake hazina maana kama hutimizi misingi hiyo.
 
Kijana hata kama una njaa, jaribu kutumia njia nyingine nzuri ya kujipatia riziki ya halali. Acha kumuhusisha Mungu na upuuzi wako. Ila kama wachawi na waganga wa kienyeji nao hujifanya kumtanguliza mungu ktk ushenzi wao, basi sishangai kwa mleta mada kumuhusisha ktk upuuzi wake. Najua katibu mkuu atakutumia bando na buku 5 ya kula, lkn huko ulipo utaendelea kuteseka, kwa kosa la kuuza utu wako sababu ya njaa yako.
Hivi leo umepata cha mchana kweli?
 
Hapa ndipo uwezo wako wa kufikiria unapoishia? Sio bure; huu ni ugonjwa!

Mungu angekuwa anafanya mambo yake kwa style hii ya kibinadamu, basi hapa duniani asingekuwepo kiumbe yeyote aitwaye shetani; angekuwa ameshamalizana naye kitambo sana!
Umejiuliza kwanini hali imekuwa hivyo? is it by chance? Mwenzako amewaza kwa kutumia akili.
 
kwahiyo tusubiri majibu ya Chacha Wangwe kupitia zile kesi zilizopo mahakamani?
Hata wewe unajua ukweli kuhusu kifo Cha chacha wangwe. Yule kijana aliyekuwa na chacha wangwe kwenye gari unajua alipo Sasa?. Na Ni Nani alimpa msamaha akatoka jela?. Aliyetoa msamaha wa kutoka jela kwa yule dogo aliyekuwa na chacha wangwe kwenye gari ni Rais Kikwete.
 
Lakini Mimi naona alichokiandika kina mantiki hata Kama ukweli unaweza kuwa sio asilimia Mia. Hakuna uhusiano Kati alichoandika na njaa, mtu mwenye njaa hawezi kuwa na akili ya kuandika Mambo mazito Kama hayo. Ila yote yaliyotokea mpaka awamu ya tano ikatoka Ni karma ya Lissu. Na karma ya Lissu itaitesa Sana serikali mpaka itubu.
Nitakuwa wa mwisho kutoamini huo mtiririko wa matukio.

Is it by chance?
 
Namba 1 kipindi cha Lissu- Deportivo la Corunia ilifanya yake

Namba mbili kipindi cha Lissu- Alijawa na huruma akaenda kumsalimia Lissu nairobi Mungu akampa Urais

Katibu Mkuu kiongozi kipindi cha Lissu- Huyu ndo anasimamia shughuli za Tiss nae deportivo la corunia ilifanya yake

Kipilimba na Musalika- DG na DDG TISS- hawa wote hawapo kwenye nafasi zao

Mambosasa- Huyu alizuia maombi juu ya Lissu sasa haijulikani kama kastaafu au la

Balozi sokoine- Huyu aliondolewa ubalozi ubelgiji baada ya kwenda hospitali kumsalimia Lissu. Leo ni Katibu Mkuu mambo ya nje cheo kikubwa kuliko balozi

Kalemani ambae inasemwa alikuwa jirani wa Lissu na alihusika kutoa cctv camera za tukio la Lissu nae sio waziri tena

Job Ndugai- Huyu alizuia pesa za matibabu za Lissu na kuzuia mshahara wa Lissu, Kwa yanayoendelea sasa CCM inaonekana hata mwezi machi hakanyagi akiwa Spika. Katiba inasema spika akipata uspika kutokana na kuwa mbunge akipoteza ubunge anapoteza uspika. Je, CCM watamvua uanachama hivyo kukosa ubunge na uspika? Tusubiri

Waliotenda wema kwa Lissu, Mungu kawabariki, waliotenda ubaya kawaadhibu! Sasa Je jaribio la kumuua Lissu lilimkasirisha sana Mungu?

Mwisho Naona Lissu akirejea Mama Samia atamteua kuwa Mbunge ili kumfuta machozi!
Kubwa la maadui, bedui, nduli, naye kafa kifo cha aibu
 
kwahiyo Mungu akikasirika anaua watu!!!!

[emoji16][emoji16][emoji16]kutompenda magufuli na utawala wake haimaanishi mtumie micundu kufikiri.
Ukiwa chukizo mbele za Mungu anakuondoa na mifano ipo mingi. Kasome pia mapigo ya wa misri, sodoma na Gomorrah etc. Pia Kuna Moto wa milele kwa watenda dhambi. Haiwezekani Kuna raia wameuawa kwenye nchi na haijulikani wapo wapi mpaka leo Halafu uniambie Mungu anafurahia. Mungu hutoa adhabu mwenyewe kwa njia ambazo mwanadamu hawezi kuijua, mpaka atafakari kwa kina.

Pia punguza ukali wa maneno mkuu. Mto mada amejaribu kuvuta events mbalimbali na kizioanisha na tukio la kupigwa risasi Lissu. Mtoa mada hajatukana mtu, wewe umekimbilia kumtukana bila kujibu hoja. Kuna Jambo Mtume Mwingira alilisema ya kwamba Lissu Ni mshindi, nilikuja kudhibitisha kwenye uchaguzi wa 2020, baada kuiba uchaguzi Urais haukudumu hata miezi mitatu ukafikia kikomo. Ili Jambo lilinifanya niogope Sana.
 
Aliomba katiba ya chama ifuatwe. Mwenyekiti akae madarakani kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano kama ilivyokuwa kwa wenyeviti wengine. Kauli ambayo ilimchukiza mwenyekigoda wa chama na kuamua kumshughulikia ili asije kujitokeza mungine wa kutaka demokrasia ya kweli ndani ya chama. Sasa huenda kesi hizi ni mwanzo tu wa yale mengi yaliofanywa na mwenyekigo huyo. Tusubiri.
Mtajitahidi Sana kumuhusisha Mwenyekiti na Mambo ya ajabu. Ndani ya moyo wako unajua Nani alihusika kwenye mauaji ya Chacha wangwe. Yule kijana alikamatwa akapewa traffic case, baadae akatolewa kwa msamaha wa Rais. Tatizo Ni kwamba raia haturumiani tuna abudu vyama kupita kiasi, ebu weka Mambo ya vyama pembeni uangalie uhalisia wa Mambo, siku Moja litatokea kwako watu watasema huyo sio wa chama chetu wacha ahangaike.
 
alimpa upofu wa macho kabla sauli aanze kumtumikia.

kifo sio adhabu ya Mungu kwa waovu,jifunzeni mambo basic tu haya katika imani.
Acha kuongopea watu kwa maslahi ya kisiasa. Kifo Ni Moja ya adhabu za Mungu. Mungu alimwambia Adam ukila tunda la mti was katikati Hakika utakufa. Na baada ya Adam kula lile tunda Mungu alimwambia Adam ya kwamba mavumbini ulitoka na mavumbini utarudi. Mungu aliwaadhibu kwa kifo sodomah na ghomorrah, Mungu aliwaadhibu wazaliwa wa Kwanza katika misri kupitia kifo, etc. Kifo Ni Moja ya adhabu anayotumia Mungu ukifanya machukizo yaliyozidi.
 
Huyo Mungu wa kukasirishwa na kuuwawa kwa "lisariti la nchi" sijui ni Mungu gani aisee..
Usikaririshwe. Lissu alimsaliti Nani na lini?. Lissu ana nguvu kubwa nyuma yake ambayo sio ya kibinadamu. Mlimpiga risasi mkashangilia ila hakufa akapona. Mkamwibia kura za urais na kuwapora ushindi wabunge wake Cha kushangaa huo urais mlioiba haukudumu hata miezi mitatu mtu akafa. Leo Rais Ni yule aliyeenda kumpa pole hospotalini. Lazima ujifunze kutafakari Mambo ndio utaujua ukweli. Karma ya Lissu itatusumbua Sana ogopa Sana damu ya mtu inapomwagika ardhini, asipokuwa na hatia.
 
Hapa ndipo uwezo wako wa kufikiria unapoishia? Sio bure; huu ni ugonjwa!

Mungu angekuwa anafanya mambo yake kwa style hii ya kibinadamu, basi hapa duniani asingekuwepo kiumbe yeyote aitwaye shetani; angekuwa ameshamalizana naye kitambo sana!
Shetani alishapewa hukumu ya milele anacho subiria Ni wafuasi wake wanao tenda dhambi ili wakatupwe wote motoni milele. Ndio maana shetani Ni mshitaki wetu mbele za Mungu, ili apate watu wengi wa kuungua naye na kupata mateso pamoja naye. Yule tayari alishakifa maana yupo kuzimu anaposubiria watenda dhambi wanaokufa ili wakateseke naye.
 
Aisee, we mpumbavu mungu yuko busy na mambo ingine limuumize la huyo pimbi mkimbizi?.
We pumbavu sana katika wote niliowasoma mwaka huu.
Mwenzako kaweka hoja ya kufikirika wewe unamwita mpumbavu?. Mpumbavu Hana muda wa kufikiri Jambo la kufikirisha Kama hili. Hoja hujibiwa kwa hoja na sio matusi.
 
Obvious Lisu alipigwa risasi na watu wa serikali ya CCM , sina wasiwasi kuna siku mhusika mmoja atasema kila kitu bila chenga, nina uhakika CIA wana kila kitu na wanajua 100% kilichotokea siku ile
 
Swali gumu hapa ni kuwa gari la Lissu lililoshambuliwa lilikuwa left or right handed?

Kama ni magari yetu haya ambayo bos hukaa kushoto, iweke Lissu aliumia mguu wa kulia badala ya kushoto ili hali dereva wake hakuumia?

Wajuvi wa mambo hebu andikeni kwa vina nipate kuelewa.

Povu si busara wapendwa.
Haya maswali yako yananikumbusha suala la Hamza. Wakati Hamza anapiga risasi na kuwaua polisi, Kuna watu wakawa wanasema ni Kiki tu wala sio ukweli na kwamba imetengenezwa na jeshi la polisi. Lakini baadae ikaja kugundulika Ni tukio la kweli Wala si uongo.

Haya maswali yako ilitakiwa ukamuulize Lissu mwenyewe ndio atakujibu. Halafu pia haya maswali sio genuine maana yamekuwa framed na walioshindwa kumuua Lissu ndio wakaja na hayo maswali. Hivyo wewe unaweza kusaidia upelelezi maana hayo maswali umeyapata wapi wakati hukuwepo kwenye eneo la tukio na umeyajuaje hayo na haukuwa na Lissu wakati anashambuliwa?. Wewe Ni mtuhumiwa.
 
Lakini Mimi naona alichokiandika kina mantiki hata Kama ukweli unaweza kuwa sio asilimia Mia. Hakuna uhusiano Kati alichoandika na njaa, mtu mwenye njaa hawezi kuwa na akili ya kuandika Mambo mazito Kama hayo. Ila yote yaliyotokea mpaka awamu ya tano ikatoka Ni karma ya Lissu. Na karma ya Lissu itaitesa Sana serikali mpaka itubu.
Kaka ake Mbowe nae alikufa kwasababu gani?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa unyama huu hata Mungu anaweza toa machozi. Walaaniwe wote waliopanga, ratibu na kutekeleza unyama huu wao na vizazi vyao hata kizazi cha kumi. Maisha yao yakawe tabu tupu hadi watamke yale waliyomtendea mtu huyu ambaye alitoa maoni yake ambayo yangeweza kujibiwa pingwa kwa hoja na si kwa mtutu wa bunduki.
 
Back
Top Bottom