Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki?

Unajua umuhimu wa Mgombea binafsi katika Demokrasia ya Ukweli?
 
Unapambana sana mkuu. Bob Marley aliwahi kusema "You Will never find Justice in the world where criminals make the rules"
 
asiependa kuoga wala kufua pekee kama wewe ndie anaweza kusingizia kwamba Tanzania tuna shida ya maji ili abaki kua mchafu hivyo hivyo,

alalalamika hakuna maji huku ana mchupa mkubwa wa maji ya kudawnload, alaaa!

katiba si muhimu na kwakwli si kipaumbele cha waTanzania kabsa 🐒
 
Hakika akisoma hili bandiko lako atapata mwanga mzuri wa nini cha kufanya kabla ya oktoba, kama anajali lakini
 
Umeongea vyema kabisa
 
Kama hujui umuhimu wa Mgombea Binafsi, kwa hapo siwezi kukusaidia maana hujitambui
Gentleman,
wananchi wa Tanzania hawana haja na huo ushirikina na hayupo wa kubabaika nao

ni muhimu kufahamu kwamba Uchaguzi mkuu wa kihistoria Tanzania ni Oct mwaka huu 2025🐒
 
Kaka paskali leo umeonyesha uwezo mkubwa na siku zoteee huyu ndie paskali tunae mjua ambae alimuuliza mwendazake swali tata/ gumu ambalo mwendazake alikwepa kulijibu.

Mambo kama haya ntapenda nisome maoni ya Hawa rafiki zangu wawili then ntapata muda wa kuchangia Nini kifanyike.
Tlaatlaah
Lucas Mwashambwa
 
Mkuu,
Mayala aliposema usitaje jina wakati wakati wa kuchangia hoja yako ,siyo kwamba anamuhofia huyo uliyemsema kwa nini asimtaje.
Lengo lake lilikuwa WEWE ujikite katika kuchangia hoja nzito ambayo itatufanya sisi wadau wa nchi tuchukue hatua stahiki ili kulazimisha mabadiliko ya katiba kuhusu chaguzi zetu kama alivyoyaainisha.
Mfano halisi ni hicho ukichokiandika kumjibu mleta mada.....,umemshambulia as a person kiasi kwamba mashambulizi yako yakafanya usahau kuchangia hoja iliyoyoko mezani..kwamba tufanyeje ili marekebish yafanyike?
Chadema kama chama cha siasa wamekuja na slogan kuhusu hilo....,No Reform,No Election....,Pasipokuwa na mabadilko, Kusifanyike uchaguzi.
Lakini hapa mleta mada akataka michango wako na wangu na wa watu wengine pia kuhusu hilo.

Binafsi rai yangu kuhusu nini kifanyike,nashauri tuunge mkono mapendekezo ya Chadema kuhusu kauli mbiu yao hiyo ya kulazimisha mabadiliko kwanza ndipo uchaguzi ufuate. Kuunga mkono kauli mbiu hii haina maana ni lazima uwe mwanachama wa Chadema. Umuhimu wa kuunga mkono unatokana na ukweli kwamba chaguzi zinazofanyika katika uwanja ulioinama katika nchi mbalimbali,ndizo zimekuwa chanzo cha vuruguna machafuko. Kwa hasira ya Watanzania inayotokana na kuchezewa rafu katika chaguzi,hasira ambayo inachemka chinichini kama volcano, ipo siku itakuja kulipuka.
Sasa tusisubiri tufike huko ndipo tuamini. Tuchukue hatua sasa.
Wewe unashauri nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…