Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki?

CDM imempatia OFA ya kuendelea kusalia madarakani kwa miaka 3 zaidi ili atuletee KATIBA MPYA, ngoja tuone kama ataendelea KUSHUPAZA SHINGO.
 
Wanabodi,



Hili ni bandiko la swali.
============
  1. Muda uliopo unatosha,kufanya minimum reforms za katiba kwa hati ya dharura,kuucholopoa huo ubatili uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu na kuifanya iwe ni katiba safi na halalii
Naunga mkono hoja.
Mada inajieleza hata bila ya muktadha.

Mkulu Pascal Mayalla , heshima yako.

Kuh angalizo:

Mzee wetu ninaelewa fika unyeti wa wa suala hili. Nonetheless, kwasababu swala hili linajadiliwa "Where we dare speak openly" naamini ingenifaa na mm Nkaburu kuwa na uthubutu na nikatia neno😁, kujibu swali, na kutoa maoni, bila ya kuwakwaza wazee wangu.

Itifaki imezingatiwa.

Tukizingatia swali la msingi katika mada, (subject matter) naomba kujibu ifuatavyo.

Nafikiri itakuwa sahihi kusema swali linauliza hivi:


Ukizingatia kama mtu anaweza kuwa na kiburi au yupo bize, unawezaje kutathmini tabia na matendo yake? Je, unadhani wasaidizi wana jukumu gani katika kumfahamisha kuhusu masuala muhimu kamavile katiba na Sheria ya Uchaguz? Hatimaye, ni hatua gani zichukuliwe kutafuta haki katika suala hili nyeti na gumu?

Changanuzi

Swali #1

  • Je ana kiburi, jeuri au yupo busy?
  • Nauliza, Je , ana sifa za kuwa Jeuri na Kiburi au yuko busy?
Jibu la haraka linaweza kupatikana hapo chini. Ni makala ya Pascal(nimelifupisha for clarity) ikijibu sifa zake na Ubize wake.
hiyo inatuambia ni msikivu na yupo bize na vipaumbele vya uchumi kwanza na hivyo basi tunaweza watupia lawama wasaidizi?

Swali #2
  • Je, Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi
  • Nauliza, Je, wasaidizi wake wamemwelezea kuhusu ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?
  • Zingatia, wasaidizi wake hawaishii magogoni peke yake, Wabunge nao, wanahusika pia.
Kwa msingi huo, Jibu la haraka linaweza jibiwa hapa chini kwenye makala ya Pascal
Binafsi naona Bunge linahusika kwa kiasi kikubwa na ubatili huo wa Katiba na mapungufu yaliyomo kwenye sheria ya Uchaguzi, hivyo lawama zilekezwe huko?

Swali #3
  • Je, tufanye nini kutafuta haki?
  • Nauliza, Je, tuchuke hatua gani kutafuta haki?
Nadhani jibu sahihi lipo, ukizingatia Chama kimoja kishasema na kupendekeza, No Reforms, No Elections, ikiwa ina maana, bila ya marekebisho muhimu ya katiba na sheria ya uchaguzi, Uchaguzi hautofanyika, piga ua?

Halikadhalika, napingana na hilo juu, kwani mabadiliko haya yanapaswa kuwa na faida kwa Watanzania wote ni sio kwa ajili ya chama kimoja tyu.

Tuchukue hatua gani?

Binafsi sishiki bunduki, nchale, fyekeo, chepeto, kuyalazimisha marekebisho/mabadiliko🤭

Napendekeza, kauli iseme "Together, For Truth and Justice" itushirikishe Wananchi wote

Maoni:Bunge Liwajibishwe🏌‍♂️
 
Mkuu Asumani, othuman dan fodio , sio uoga, nafundisha watu kujadiki hoja na sio kujadili watu!.
Hapa swali ni tufanye nini?.
P
Pascally hata kama unafundisha watu kujadili hoja lkn kwa mtu unayemzungumzia code zipo wazi kulikuwa hakuna haja ya kuficha kwa kiwango hicho.

Imagine wewe ni mwanasheria by proffesional ambapo jamii inajua sio watu waoga itakuaje kwa mwalimu wa upe?
 
Mkuu Asu, othuman dan fodio , lengo la kuepuka kutaja majina ni kingio la kutunza staha za watu, ningemtaja kwa jina, saa hizi angeisha ogeshwa kwa ... ya kutosha!.
P
 
Vikibadilika tutapoteza our greenish Pascal Mayalla
 
Mambo ni mengi sana hasa mvutano wa kisiasa katika kukwamishana kisiasa,, lakini nijikite kwenye swali lako la mwisho...Watanzania tunapaswa kwa umoja wetu kuipazia serikali kuwa tunataka haki yetu ya kikatiba sambamba na kupata katiba mpya nasio wakuwaachia viongozi pekee walisemee hilo,, mfano. sehemu sahihi ya watanzania kufikisha ujumbe ni kwenye matamasha,mikutano, miyaliko mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, kwenye ziara za viongozi sio kiongozi anakuja eneo lenu kazi kuwasema wanaioba pesa za serikali tu na kusuasua kwa miradi lazima kuchombeza na swala la haki yetu sisi kama watanzania lakini kama watanzania wenyewe hawajaona umuhimu wa haki yao kikatiba pengine kwa sababu wanazoziona wao hawatoliwekea mkazo hvo litabakia kwa viongozi tu wakiumana meno na iwe hvo na sio njia ya kuandamana tena kusisitiza kabisa kama havitofanyika hvo sisi raia hatwendi kupiga kura yoyote...changamoto inayokuja hapo nikuwa kunakundi kubwa la watanzania wanalamba asali na wengine hawalambi asali...mambo ni mengi.
 
Yeye na serikali yake wasipokuwa sikivu nchi hii tutakuwa kama congo, ni swala la muda tu.
 
Mama Samia huyo

Hacha kujidanganya kwamba watz awaoni umuhimu wa katiba mpya wanajuwa sana ila tukubaligi tu ukweli watz ni mazwazwa el mapong'ole
 
Kama kawaida yenu watz uwa mnakamtindo ka usahaulifu mshasahau aliwaambia yeye ni CHURA KIZIWI 😀. Mana yake mshapuuzwa mnaonekana Si lolote SI chochote
 
Paskali, wakati huu umekuwa mkweli kwa taaluma na nchi yako, hongera kwa bandiko bora tangu mwaka uanze.

Vv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…