Inawezekana tuna watu wasio na uwezo katika nafasi wanazozitumikia?

Yeye mwenyewe anasemaje
Yeye mwenyewe anaujua mchezo wa siasa vizuri kiasi cha kukaa kimya kwenye hili, na kuwaachia expendables wake kina January Makamba wamsemee kwamba "Makamu wa Rais alitengwa sana".

Samia might be dumb enough to tout albadiri solutions in a secular state, I will give you that. She may not be the brightest bulb in the room.

But she is not so dumb to walk on a political minefield for no reason right before an election year.
 
Mkuu focus zaidi on what mabeyo didn't want to say! Because he said what people wanted to hear!
 
Hayo anayoongea huyo CDF ni matokeo ya Magufuli kutawla bila kufuata Sheria, na kwa bahati mbaya hata hao wateule wake walikuwa wanafuata chochote anachoagiza bila kujali Sheria inasema Nini. Huyo CDF alikuwa anacheka kwenye kamisheni ya Jeshi huko Arusha wakati Magufuli anapokea wanaccm kwenye hafla ya kijeshi, wakati kikatiba jeshi limetengwa kabisa na siasa. Sikushangaa akimuagiza CDF aagize apelekwe kwao akafie nyumbani.

Hayo ndio yalikuwa maagizo yake kwenye mambo mengi. Ni nani hakuona jeshi likitumika kuvamia maduka ya kubadilishia fedha na kupora wafanyabiashara fedha zao? Nani hakuna jeshi likitumika kununua korosho za wakulima kwa shuruti? Katika mazingira hayo kwanini wahuni wasitumie mazingira hayo kufanya kinyume na katiba, maana tayari ilishazoeleka na huyo CDF alikuwa anakaa kimya.
 
Mimi najiuliza mpaka sasa je Mabeyo alikuwa na haja gani ya kuyasema haya ?

Je nj kitu gani kipo nyuma ya pazia kimemfanya aseme hivyo ?

Je kunyamaza haikuwa best option kwake ?
 
Upo sahihi kwa kila ulichokiandika.

Tatizo la msingi na swali la kujiuliza ni kwa nini waliokuwa na taarifa ya hali tete ya JPM (kama walikuwa briefed) walikuwa kimya kututaarifu Watanzania ili tumuombee kama ambavyo yeye mwenyewe alikuwa akituomba tumuombee!!?

Ilikuwaje kwenye" chain of command" na kwenye "succesion plan" kwa mujibu wa katiba, VP na PM wasiwe na taarifa ya hali halisi ya Rais ila "CS" na "CDF" wawe na taarifa!!???

Rais akiwa hai,kisheria na kikatiba, ni nani huwa anaweza kumshirikisha kutoa pesa hazina kwa niaba yake!!??

Ni nani aliye na mamlaka ya kutoa hela BOT kama Rais hayupo!!???

Inawezekana kabisa tukawa tunatafuta mchawi wa the dark days between "12th/03/2021" na "19th/03/2021, lakini wachawi hao tunao, na tunaishi nao katikati yetu, na tuna kula nao na kusaza, huku tukiendelea kulalamika "as if" hatuna uwezo wa kuwafanya chochote cha kuwa funzo kwa wengine.

Nafikiri ni wakati wa Watanzania kuamka na kufanya jambo ambalo hawa ambao inasemekana kuwa tumewachagua kidemokrasia tunaowaita "viongozi" japokuwa ni "watawala" , wataelewa kuwa sasa Watanzania halisi tumechoka.

Rais Samia anavyoendelea kuwachekea hao anaofikiri kuwa ni wenzake, aangalie kile kinachotokea kwa JPM kwa wale waliokuwa wakionekana kama ni waumini wake.
 
Mimi najiuliza mpaka sasa je mabeyo alikuwa na haja gani ya kuyasema haya ?

Je nj kitu gani kipo nyuma ya pazia kimemfanya aseme hivyo ?

Je kunyamaza haikuwa best option kwake ?
Mabeyo hakuamua kuyasema yeye kama yeye hadharani.
Kama CDF, aliambiwa ayaseme hayo ili kuwatisha wengine wote ambao walikuwa ama watakuwa wanaamini kuwa wapo salama katika kuyapanga mambo yao dhidi ya "SSH".
 
ujuaji wa kipumbavu tunao watanzania

aliye kuwa na mgonjwa ni mabeyo

makamu yuko tanga

waziri yuko dodoma, ko ulitaka aliye na mgonjwa (aliye eneo la tukio ) asifahamu hali ya mgonjwa afahamu aliye tanga na dodoma

acheni ujuaji wa kipumbavu
Hata hujui unaongelea kitu gani walah
 
Wewe ni mbumbumbu na hujui lolote kuhusu mamlaka ya CDF ki protocal ila kwa kukutoa ujinga jua tu mamlaka ya CDF ni makubwa kuliko makamu wa rais, usisahau rais ni amir jesh mkuu, na CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama na ndiye mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya nchi.
 
Usifananishe rais na takataka zingine,we hata ukitaka kufia porini sawa tu sio rahisi,uhai wake unapiganiwa kwa gharama zote na kuna watu wanakuwa responsible ikitokea uzembe wowote ule,rais hupangiwa mambo mengi maana ni taasisi
Mbona JPM urais wake haukipiganiwa kwa gharama zozote!!??

Mbona hakuna watu waliokuwa "responsible" wakati tunaambiwa ni uzembe ndio umepelekea kifo chake!!??
 
Ilipaswa CDF atii agizo la Rais,kwani ni amri,angemletea usafiri akafie kwake tu mbona simple kuliko watu wasubirie muda wako ufike.
 
Hakuna anayekataa kuwa CDF ni zaidi ya makamu wa rais, je katibu mkuu kiongozi na waziri mkuu nao vyeo vyao ni zaidi ya makamu wa rais? Kwanini wapewe wao taarifa ya hali ya rais kwanza Hadi kuitwa, huku akiachwa makamu wa rais? Punguza jazba jibu hoja kwa utulivu.
 
Wewe umecreate assumption zako sijui wewe ndo January aunmkwe WA Samia.Naona unamshambulia indirect CDF msitaafu bure
 
Nadhani utaraibu ingekuwa kuhakikisha karibu na mgonjwa kunamwanafamilai anayeona Kila kitu kinachotokea na siyo kuambia Rais amefariki.
 
Wewe umecreate assumption zako sijui wewe ndo January aunmkwe WA Samia.Naona unamshambulia indirect CDF msitaafu bure
CDF ana pengi pa kushambuliwa na nikitaka kumshambulia naweza, na wewe huwezi kumtetea.

Ila sijaanza kumshambulia.

Ni wewe tu hujui kusoma kwa ufahamu.

Ukibisha, niambie nimemshambulia CDF hapa, na hapa, kwa sababu hii na hii.

Tuchambue mambo kwa kina, si kwa shutuma za jumlajumla tu za "wewe umemshambulia CDF" ambazo mjinga yeyote mwenye mahaba na jeshi anaweza kuzisema bila kuweza kuzielezea kimantiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…