Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

Tatizo Lisu Hana self control hazingatii kanuni za TCRA akiongea vyombo vya habari

Ni mtu risk Kwa vyombo vya habari vyaweza fungiwa na TCRA labda mahojiano yafanyike Private wahariri ndio warushe Lakini akiongea Live Kuna uwezekano mkubwa chombo Cha habari kufungiwa na TCRA Kwa kukiuka maadili
Ni lini lisu aliongea na media ikafungiwa
Hakuna mwanasiasa ambaye yupo makini na anachoongea kama lisu sababu anajua sheria
 
Tatizo Lisu Hana self control hazingatii kanuni za TCRA akiongea vyombo vya habari

Ni mtu risk Kwa vyombo vya habari vyaweza fungiwa na TCRA labda mahojiano yafanyike Private wahariri ndio warushe Lakini akiongea Live Kuna uwezekano mkubwa chombo Cha habari kufungiwa na TCRA Kwa kukiuka maadili
Umeongea vzr tena vzr sana
 
Hata sijui mnashangaa kitu gani hapo, kwangu hata kama mahojiano yangefanyika, naona hizo ni siasa tamu za muda mfupi tu

Diamond = CCM.

Kitenge = CCM.

Hayo mambo ni kuyazoea na kuachana nayo, tazameni njia nyingine zenye maana zaidi na uzito, zenye kuleta mabadiliko kiuhalisia, sio kwa maneno.

Hata Lissu sioni maana kwake kwenda huko kupata maelezo, hao jamaa wanatumiwa na CCM, ndio wanaowapa leseni, lakini pia, mambo mengine ni maamuzi yao kwani kituo ni chao.

Kama wameamua kuhairisha au kufuta, muhimu wamuombe radhi Lissu kwa usumbufu, biashara iishe, lakini sio kila siku tuendelee kushangaa hadaa zile zile za miaka yote, ni ujinga.

Lissu nae kama anaona amepotezewa muda, aende mahakamani kudai fidia, lakini sio kugomea kwenye ofisi za watu, ataonekana msumbufu mwishowe aje kuondolewa hapo na polisi, now what is that..!!
Kuwa CCM siyo sababu ya Kuchoka na Mfumo m'bovu unaoendelea.

Inafikia Wakati watu wanachoka
 
kwa uongeaji wa puppet haipo media house itakubali kupoteza viewers na followers wake kwa kumkaribisha mropokaji asie na staha kama huyo kibaraka.

hiyo media house haipo Tanzania na kama kuna media itampa platform bass hasara na madhara yake kwenye media hiyo kwenye industry yatakua ni makubwa mno 🐒

Kwan kule space na YouTube hapatoshi 🤣

Kama ni kupoteza viewers na followers ungeipambania TBC1 maana hiyo ndio ya ccm, pilipili usiyoila inakuwashia Nini? Hiyo Wasafi viewers wake ni vijana na sio wazee kama TBC, na vijana wanataka kumsilikiliza Lisu, itapotezaje viewers, na hata ikipoteza kwa ajili ya Lisu shida yako ni Nini, kwani ww ni afisa masoko wa Wasafi?

Huu ujinga wa kuandaa mafuriko fake ndio ulimponza Magufuli, akaamini anakubalika na wapinzani wake wamepotea kisa alitisha vyombo vya habari vikawa vinamtukuza yeye tu. Ilipofika wakati ww kampeni akafanya hila zote, lakini Bado wapinzani walipata nyomi la ukweli, akaishia kupora uchaguzi. Ujinga ule ule naona Bado mnatembea nao. Nasema hivi, acheni kuharibu biashahara za wanaume, kama mmechoka kubalini tu hakuna kinachodumu milele.
 
Lissu aliitwa kwenye interview WASAFI nakugfanya kila mtu kuwa makini kutaka kujua atakacho zungumza. , ghafla wakamchelewesha na kutomjuza kinachoendelea.
Uongozi wa WASAFI FM Watamueleza Lissu, na wasipotaka waache vile vile na ikiwezekana akitoka hapo achapishe tweet/post moja nzito sana kueleza huo upumbavu wao.

Kwa kuwa mtaji wa mwanasiasa ni watu, Tundu Lissu anao hao watu, awaeleze watu wake huo mchezo wa WASAFI kwa kushirikiana na dola katili la CCM.

Wasafi walitumia jina la Tundu Lissu kuvuta wasikilizaji katika kipindi chao leo. Wameuza maudhui kupitia jina la Tundu Lissu.

Watu wengi leo wamewasha radio wamsikilize Tundu Lissu (watu ambao siyo wasikilizaji wa WASAFI FM). Wameishia kulishwa habari za Bashite na matangazo ya kubeti.

Mwanasiasa makini lazima alinde hisia za watu wake ambao waliwasha radio tangu saa 11 alfajiri ili wamsikilize na wameishia kuambiwa mahojiano yamehairishwa kutoka juu.

Lakini moreover ni nzuri zaidi kisiasa kwamba Tanzania hakuna uhuru wa vyombo vya habari na kwamba waziri wa habari anaweza kupiga simu kuzuia mahojiano ya mpinzani yasifanyike.

Mwanasiasa mkubwa mwenye sifa na jina la Tundu Lissu anazo ratiba zake za kila siku, unapompa taarifa kwamba kutakuwa na kipindi cha radio, anajianda na kuvunja ratiba nyingine, ghafla asubuhi unahairisha. Ni utovu wa nidhamu.
Hizi Makitu za WASAFI FM zimenitafakarisha sana:

1. Nimekumbuka 1995 RTD ilivyogoma kupiga wimbo wa Dr. Remmy uitwao "MREMA" lakini ikawa inapiga nyimbo za TOT kumsifia MKAPA;

2. Mahakama Kuu, Mhe Barnabas Samatta, kuamua kuwa magazeti ya serikali ie Daily& Sunday News ni lazma yatoe "coverage" sawa kwa vyama vyote na yaache kuegemea kwenye chama tawala;

3. Mhe Waziri Nape alipotaka kuongea na waandishi wa habari Court yard hotel, St. Peter's akaishia kuoneshwa pisto!

4. Watangazaji wa WASAFI FM mfano Maulid Kitenge[Mossad] & Gerald Hando kuonekana kukwazwa sana na kilichojiri leo;

5. Umuhimu wa kusubiri kupewa taarifa rasmi na uongozi wa WASAFI FM juu ya kilichojiri badala ya kuwashutumu masna nimeona Bongolanderz wakidai "WASAFI FM YAWA WACHAFU FM"!
 
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba interview ya Mh. Tundu Lissu pale Wasafi FM imefutwa.

Awali ilielezwa kwamba Tundu Lissu angefanya mahojiano katika kituo cha Wasafi. Taarifa zisizowekwa wazi ni kwamba mahojiano hayo yamefutwa kufuatia maelekezo ya CCM

---
Taarifa kutoka ukurasa rasmi wa CHADEMA mtandao wa X

Leo tarehe 07 Februari 2024 Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. Tundu Lissu alipata mwaliko wa kufanya mahojiano maalum na kituo cha Luninga cha Wasafi Tv katika kupindi cha Good Morning kinachoanza saa 11 alfajiri mpaka saa mbili asubuhi. Jana usiku moja ya watangazaji wa kipindi hicho alimpigia Mhe. Lissu na kumjuza kuwa mahojiano hayo yameahirishwa kutokana na maelekezo kutoka juu.

Aidha, asubuhi ya leo Mhe. Tundu Lissu amefika Wasafi Tv kujua sababu za kuahirishwa kwa mahojiano hayo. Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea muda huu katika ofisi za Wasafi Tv.

Updates

Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi.

View attachment 2896687
Picha: Tundu Lissu akiwa ofisi za Wasafi​
Matumizi mabaya ya vyombo vyetu vya dola.

Nape anaamini uwaziri wake umemmilikisha vyombo vyote vya habari nchini.

Endeleeni kumsifia mama ambaye wateule wake wananyonga na kuua HAKI za kikatiba za watu
 
Watamueleza, na wasipotaka waache vile vile na ikiwezekana akitoka hapo achapishe tweet/post moja nzito sana kueleza huo upumbavu wao.

Kwa kuwa mtaji wa mwanasiasa ni watu, Tundu Lissu anao hao watu, awaeleze watu wake huo mchezo wa WASAFI kwa kushirikiana na dola katili la CCM.

Wasafi walitumia jina la Tundu Lissu kuvuta wasikilizaji katika kipindi chao leo. Wameuza maudhui kupitia jina la Tundu Lissu.

Watu wengi leo wamewasha radio wamsikilize Tundu Lissu (watu ambao siyo wasikilizaji wa WASAFI FM). Wameishia kulishwa habari za Bashite na matangazo ya kubeti.

Mwanasiasa makini lazima alinde hisia za watu wake ambao waliwasha radio tangu saa 11 alfajiri ili wamsikilize na wameishia kuambiwa mahojiano yamehairishwa kutoka juu.

Lakini moreover ni nzuri zaidi kisiasa kwamba Tanzania hakuna uhuru wa vyombo vya habari na kwamba waziri wa habari anaweza kupiga simu kuzuia mahojiano ya mpinzani yasifanyike.

Mwanasiasa mkubwa mwenye sifa na jina la Tundu Lissu anazo ratiba zake za kila siku, unapompa taarifa kwamba kutakuwa na kipindi cha radio, anajianda na kuvunja ratiba nyingine, ghafla asubuhi unahairisha. Ni utovu wa nidhamu.
Wameyatimba wamekutana na kichwa sasa kazi kwa mazoea mazoea ni shida..
 
Back
Top Bottom