Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba interview ya Mh. Tundu Lissu pale Wasafi FM imefutwa.

Awali ilielezwa kwamba Tundu Lissu angefanya mahojiano katika kituo cha Wasafi. Taarifa zisizowekwa wazi ni kwamba mahojiano hayo yamefutwa kufuatia maelekezo ya CCM

---
Taarifa kutoka ukurasa rasmi wa CHADEMA mtandao wa X

Leo tarehe 07 Februari 2024 Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. Tundu Lissu alipata mwaliko wa kufanya mahojiano maalum na kituo cha Luninga cha Wasafi Tv katika kupindi cha Good Morning kinachoanza saa 11 alfajiri mpaka saa mbili asubuhi. Jana usiku moja ya watangazaji wa kipindi hicho alimpigia Mhe. Lissu na kumjuza kuwa mahojiano hayo yameahirishwa kutokana na maelekezo kutoka juu.

Aidha, asubuhi ya leo Mhe. Tundu Lissu amefika Wasafi Tv kujua sababu za kuahirishwa kwa mahojiano hayo. Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea muda huu katika ofisi za Wasafi Tv.

Updates

Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi.

View attachment 2896687
Picha: Tundu Lissu akiwa ofisi za Wasafi​

View: https://twitter.com/clickHabari/status/1755141018964336921?t=k06mHdM-v4SWyhaMwMr1BQ&s=19
 
Tatizo Lisu Hana self control hazingatii kanuni za TCRA akiongea vyombo vya habari

Ni mtu risk Kwa vyombo vya habari vyaweza fungiwa na TCRA labda mahojiano yafanyike Private wahariri ndio warushe Lakini akiongea Live Kuna uwezekano mkubwa chombo Cha habari kufungiwa na TCRA Kwa kukiuka maadili
Acha woga na tcra yako we andazi

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama hawana hiyo haki si mlazimishe basi ahojiwe.Hicho ni kituo binafsi kinachomilikiwa na mtu binafsi.Anachodai Lisu ni kwanini Interview imekuwa cancelled.Apewe maelezo tu aondoke zake.
Ndio maanake maana kaambiwa kituo kimepewa maelekezo toka juu. Huyo wa juu ni nani anayezuia biashahara halali za watu zisifanye kazi? Maana Sheria inataka vyombo vya habari visifanye ubaguzi, Sasa ni nani kawapa maelekezo toka juu? Kama hata ww unamjua au sababu ya msingi ya Lisu kuzuiwa iseme.
 
Bwahaaaa, bwahaaaaa, eti wana haki ya kucancel, hiyo haki waliijua baada ya muda gani? Na walipomualika hawakuwa wanaijua hiyo haki? Ila Leo nina raha ya hatari, pale majizi yanapoamua kuharibu biashahara za wanaume kwa kuhofia upotoshaji wao kuwekwa vizuri.
Haya sasa Lisu kapewa maelezo na ameridhika kwamba hakukuwa na nia ovu wala amri kutoka kokote kuhusu ku cancel hiyo interview.
Wazee wa kukurupuka njooni na lingine.
 
Mbona Wananchi wanamiminika Kwa Makonda kutoa kero zao? Kwa nini wasimiminike huko Chadema?
Huko kote wanakomiminika Kuna viongozi wa ccm, matatizo yao yashindwe kutatuliwa na hao wakazi, Hadi aje muhalifu mpita njia kutatua matatizo yao? Bado Kuna wajinga wa hivyo miaka hii?
 
Ndio maanake maana kaambiwa kituo kimepewa maelekezo toka juu. Huyo wa juu ni nani anayezuia biashahara halali za watu zisifanye kazi? Maana Sheria inataka vyombo vya habari visifanye ubaguzi, Sasa ni nani kawapa maelekezo toka juu? Kama hata ww unamjua au sababu ya msingi ya Lisu kuzuiwa iseme.
Umekurupa na uzushi wako.Haya rejea maelezo ya Tundu Lisu kuhusu hiyo interview.
 
kwa nini alialikwa?
Nadhani aliyemwalika hakufanya risk analysis

Anyway Tundu Lisu angepotezea tu unless alikuwa na hidden agenda ya kuyabwaga kuhakikisha akimaliza interview TCRA wanafuifingia hiyo TV

Asitangaze vita na TV hawatatangaza chochote chake Wala Cha Chadema mbeleni huko

Awe future focussed akiwatibua asahau habari zake kurushwa zitabakia BBC swahili huko
 
Haya sasa Lisu kapewa maelezo na ameridhika kwamba hakukuwa na nia ovu wala amri kutoka kokote kuhusu ku cancel hiyo interview.
Wazee wa kukurupuka njoo na lingine.
Weka ushahidi wa yeye kuridhika kuahirishwa kipindi kwa maagizo toka juu.
 
Ahhh. 😂Kwani pale ni maelezo. Apunguze Udikteta

Akamalizie kombe lake la Uji, aje afanye mahojiano humu basi. T.L aje tu J.F amalize nyongo.
Wao wamemuita, halafu dakika za mwisho wanahairisha mahojiano. Kama Leo alikuwa na ratiba zake, amehairisha kwaajili ya mahojiano?. Ongea uhalisia usipende siasa muda wote
 
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba interview ya Mh. Tundu Lissu pale Wasafi FM imefutwa.

Awali ilielezwa kwamba Tundu Lissu angefanya mahojiano katika kituo cha Wasafi. Taarifa zisizowekwa wazi ni kwamba mahojiano hayo yamefutwa kufuatia maelekezo ya CCM

---
Taarifa kutoka ukurasa rasmi wa CHADEMA mtandao wa X

Leo tarehe 07 Februari 2024 Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. Tundu Lissu alipata mwaliko wa kufanya mahojiano maalum na kituo cha Luninga cha Wasafi Tv katika kupindi cha Good Morning kinachoanza saa 11 alfajiri mpaka saa mbili asubuhi. Jana usiku moja ya watangazaji wa kipindi hicho alimpigia Mhe. Lissu na kumjuza kuwa mahojiano hayo yameahirishwa kutokana na maelekezo kutoka juu.

Aidha, asubuhi ya leo Mhe. Tundu Lissu amefika Wasafi Tv kujua sababu za kuahirishwa kwa mahojiano hayo. Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea muda huu katika ofisi za Wasafi Tv.

Updates

Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi.

View attachment 2896687
Picha: Tundu Lissu akiwa ofisi za Wasafi

View attachment 2896880
R.I.P Thadei Ole Mushi
 
Back
Top Bottom