Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

Interview ya Tundu Lissu yasitishwa Wasafi FM. Mwenyewe ang'ang'ania ofisi za Wasafi. Wakubaliana kuifanya wakati mwingine

Kwani anashare pale wasafi hadi aelezwe sababu?
Unaelewa unachouliza? Yani watu mmewasialna zaidi ya wiki mbili na kukubali. Halafu masaa machache unapigiwa simu kuharisha mahojiano bila sababu za msingi. Kuna mambo mangapi umehairisha?. Tuwe wakweli
 
Boss wa wasafi ni chawa wa ccm unategenea nini? Ati matatizo ya kiufundi ati ubora wa kipindi? Hovyo kabisa🚮
 
Hawa Watu waliosoma shule za Vipaji usiwachukulie poa au kihunihuni ndio Sababu huwa namuheshimu sana tu mwanabodi Pascal Mayalla

Unaweza kukuta sasa Tundu Antipas Lisu anajadiliwa zaidi huko mitaani na mitandaoni kuliko hata kama angeruhusiwa kushiriki kile kipindi cha radio

Akili kubwa ni kubwa tu hata kama ni Made Darasani 😄
 
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba interview ya Mh. Tundu Lissu pale Wasafi FM imefutwa.

Awali ilielezwa kwamba Tundu Lissu angefanya mahojiano katika kituo cha Wasafi. Taarifa zisizowekwa wazi ni kwamba mahojiano hayo yamefutwa kufuatia maelekezo ya CCM

---
Taarifa kutoka ukurasa rasmi wa CHADEMA mtandao wa X

Leo tarehe 07 Februari 2024 Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. Tundu Lissu alipata mwaliko wa kufanya mahojiano maalum na kituo cha Luninga cha Wasafi Tv katika kupindi cha Good Morning kinachoanza saa 11 alfajiri mpaka saa mbili asubuhi. Jana usiku moja ya watangazaji wa kipindi hicho alimpigia Mhe. Lissu na kumjuza kuwa mahojiano hayo yameahirishwa kutokana na maelekezo kutoka juu.

Aidha, asubuhi ya leo Mhe. Tundu Lissu amefika Wasafi Tv kujua sababu za kuahirishwa kwa mahojiano hayo. Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea muda huu katika ofisi za Wasafi Tv.

Updates

Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi.

View attachment 2896687
Picha: Tundu Lissu akiwa ofisi za Wasafi

View attachment 2896880
Kitenge yupo sahihi. Ameelezea vyema kabisa, dawa ni kutoganya nao interview tena.
 
Yawezekana alizi-cancell baadhi ya ratiba zake kutokana na mwaliko wa kipindi,hivyo kwa leo ratiba zake unakuta zimevurugika,yaani ratiba yake imemfanya yeye kuathirika.
sasa ikitokea ivo si anajiformat na kujimodify chap anaendelea na nyingine 🐒

huyo hamna kitu bana anaforce kisichowezekana kutafuta huruma na kuwaonyesha mabwenyenye wanaomfadhili kwamba anaonewa na kudhulumiwa 🐒
 
Huyu mtu anasemaga uongo na kueneza falsafa isiyofaa ya uliberali tanzania. Eti kila kitu ruksa na kushindana. Wanaruhusu ushoga umalaya eti ni uhuru wa mtu. Asante wasafi kufuta mahojiano na hii kibaraka wa sera za sisi kunyonywa na wageni.
Leta clip moja inayosema hayo. Tusipende kuropoka vitu kisa chuki ya kisiasa
 
Ndio muone sasa umuhimu wa kuwa na VYOMBO vyenu vya HABARI... mnaweza kusema ohoo havitosajiliwa, sawa ILA mlishajaribu kuomba kwa kufuata TARATIBU zote?..

Ombeni kwa kufuata taratibu zote, wakikataa, NJOONI kwa Wananchi
Huzijui figisu za MCC wewe.
 
Nadhani aliyemwalika hakufanya risk analysis

Anyway Tundu Lisu angepotezea tu unless alikuwa na hidden agenda ya kuyabwaga kuhakikisha akimaliza interview TCRA wanafuifingia hiyo TV

Asitangaze vita na TV hawatatangaza chochote chake Wala Cha Chadema mbeleni huko

Awe future focussed akiwatubua asahau habari zake kurushwa zitabakia BBC swahili huko

Yaani wasirushe habari zake Wala hawezi kuwabembeleza, hata Wakati wa kampeni za 2020 kwenye kampeni hiyo hujuma ilikuwepo, hivyo sio jambo jipya. Ila tumejua ule utapeli wa uhuru wa vyombo vya habari umerudi ni utapeli kama utapeli mwingine. Mitandao ya kijamii inatutosha maana Dunia ya Sasa kwenye upande wa habari uko juu ya mbinu za kizee za ccm.
 
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba interview ya Mh. Tundu Lissu pale Wasafi FM imefutwa.

Awali ilielezwa kwamba Tundu Lissu angefanya mahojiano katika kituo cha Wasafi. Taarifa zisizowekwa wazi ni kwamba mahojiano hayo yamefutwa kufuatia maelekezo ya CCM

---
Taarifa kutoka ukurasa rasmi wa CHADEMA mtandao wa X

Leo tarehe 07 Februari 2024 Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. Tundu Lissu alipata mwaliko wa kufanya mahojiano maalum na kituo cha Luninga cha Wasafi Tv katika kupindi cha Good Morning kinachoanza saa 11 alfajiri mpaka saa mbili asubuhi. Jana usiku moja ya watangazaji wa kipindi hicho alimpigia Mhe. Lissu na kumjuza kuwa mahojiano hayo yameahirishwa kutokana na maelekezo kutoka juu.

Aidha, asubuhi ya leo Mhe. Tundu Lissu amefika Wasafi Tv kujua sababu za kuahirishwa kwa mahojiano hayo. Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea muda huu katika ofisi za Wasafi Tv.

Updates

Tundu Lissu sasa yupo Wasafi FM kupata sababu za msingi za kufutwa kwa mahojiano. Licha ya kupewa taarifa kwa njia ya simu, Lissu hakuridhika na badala yake amekuja mwenyewe Wasafi. Uongozi wa Wasafi umeomba radhi bila kueleza sababu za msingi.

View attachment 2896687
Picha: Tundu Lissu akiwa ofisi za Wasafi

View attachment 2896880
Mlisema wamekatazwa vipi tena nyie Punda?

View: https://twitter.com/clickHabari/status/1755141018964336921?t=k06mHdM-v4SWyhaMwMr1BQ&s=19

Mahakamani mnaenda lini? 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom