IRAN IMESHAMBULIWA KWA UZITO
Toka asubuhi na mapema nimekuwa nikifuatilia kwa makini na utaratibu ili nije kuwapa taarifa za kina na zenye uthibisho. Masaa manne yaliyopita, Israeli imefanya mashambulizi makubwa ndani ya ardhi ya Iran, Siria na Iraq na wakati huo huo ikifanya mashambulizi ya anga ndani ya Lebanon na Gasa. Vituo vya kijeshi vya mamluki wa Iran ndani ya Siria na Iraq vimeshambuliwa. Na ndani ya Iran Israeli imeshambulia maeneo 20 katika mijimbo matatu.
Ndani ya Iran
Asubuhi na mapema ndani ya Tehran na majimbo mengine vilisikika vishindo vizito vya makombora. Serikali ya Iran ilikuwa kimya na haikuruhusu vyombo vyake vya habari virushe matukio ya mashambulizi pamoja na hilo ilifunga anga lake. Lakini taarifa za vyombo binafsi (wale wabishi) ndani ya Iran vimeripoti matukio ambayo yameilazimisha serikali ya Iran kukiri kwamba kuna uharibifu mkubwa umefanyika katika miji yake mitatu katika maeneo maalum ya kijeshi. Mamlaka ya Iran, imetangaza bayana kwamba nayo itayajibu mashambulizi ya Israeli.
Israeli baada ya shambulio la Iran la october 1 ambalo liligusa vituo vitatu vya kijeshi vya Israel na sehemu kadhaa za makazi ya raia, nayo ilipanga kujibu shambulio hilo na imejibu baada ya siku 25. Huku Iran ilitumia miezi miwili kujibu kwa kulipiza kisasi cha mauaji ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh aliyeuawa 31 July pamoja na maofisa wengine wa Hezbollah na Iran waliouawa baada ya hapo. Hii inaonesha dhahiri kuwa intelijensia ya Israeli ni kubwa zaidi.
Mpango wa Israeli
Kabla ya shambulio la leo, balozi wa Israeli kwa UN, alitoa taarifa kwa UN iliyoikataza Israeli isijibu, alijibu kwa kusema Israeli lazima ijibu ili kuonesha dunia uwezo wake. Na waziri mkuu wa Israeli hapo nyuma alikuwa ametangulia kusema kuwa atajibu shambulio la Iran kwajili ya maslahi ya Israeli. UN na nchi kadha wa kadha zilionya kwamba aache ili kuepusha machafuko ya kikanda. Israeli ilikataa na Marekani wao wakaiunga mkono. Lakini Marekani haikuunga mkono mpango wa Netanyahu wa kuharibu vinu vya nyuklia na visima vya mafuta vya Iran kwa kile ambacho kwamba sumu ya nyuklia ingeleta sio tu uharibifu kwa raia wa Iran bali na kwa majirani zake na kwamba kama visima vya mafuta vingelipuliwa ingeleta shida ya upungufu wa mafuta duniani. Inasemekana Marekani ilivujisha mpango huu wa Israeli wa kushambulia sehemu hizo. Iran nayo ika respond kwamba kama Israeli inataka kuishambulia Iran basi nayo ijibu kwa kupiga vituo vya kijeshi kama walivyofanya wao. Wachambuzi wengine wanadai mpango huo kuvuja ulikuwa ni mpango wa kijasusi wa kuizubaisha Iran.
Hofu ya siku 24 ndani ya Iran
Ndani ya siku 24 kabla ya mashambulizi ya leo, wananchi wa Iran walikuwa wamejawa na hofu kuu. Hawakujua nini kitawakuta, wengi wao waliukimbia mji wa Tehran ili kujiepusha na mashambulizi ya Israeli. Serikali ya kislamu ya Iran, iliwatoa hofu wananchi wake kwamba wamejiandaa kuzuia mashambulizi ya Israeli.
Kujipanga kwa Iran dhidi ya mashambulizi ya Israeli
Urusi ambaye ni mshirika wa Iran, aliipa Iran betri za S 400 ili kuongeza nguvu kwa S 300 ambazo zipo Iran ambazo pia ni za Urusi. Hivyo betri za Iran na zile za Urusi zilifungwa katika mji wa Tehran na sehemu maalum za kijeshi na miundo mbinu muhimu.
Mashambulizi ya Israeli
Israeli kuanzia saa 10 usiku, ilituma ndege zake za F35 pamoja na makombora kadha wa kadha kwenda Iran. Mifumo ya anga ya Iran ikiwemo S 400 ilishindwa kuziona ndege hizo ambazo zilishambulia sehemu muhimu na kutoka. Pia makombora nayo yakalenga kwenye malengo yaliyopangwa na kuleteleza uharibifu katika maeneo makuu matatu ya kijeshi na sehemu zingine 20 ambazo nazo zoliguswa na makombora na mabomu ya ndege.
Hapa kuna sasisho (update) za hivi punde kutoka Aljazeera:
Jeshi la Israel limefanya mashambulizi dhidi ya Iran na kushambulia maeneo 20 kwa saa kadhaa kujibu shambulio la kombora la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tarehe 1 Oktoba.
Msemaji wa jeshi la Israel alisema shambulio hilo ambalo sasa limekamilika, ambalo alilitaja kama operesheni ya "Days of Reckoning of" yaani Siku za hesabu", lilishambulia "zana za kutengeneza makombora" ya Iran, pamoja na mifumo ya makombora ya kutoka ardhini hadi angani na uwezo mwingine wa ulinzi wa anga.
Jeshi la Iran limethibitisha kuwa mashambulizi hayo ya Israel yalilenga vituo vya kijeshi katika majimbo ya Ilam, Khuzestan na Tehran, na kusema yalisababisha "uharibifu mdogo".
Israel imeionya Iran dhidi ya kulipiza kisasi, ikisema "italazimika kujibu" tena, na kuongeza kuwa ina "malengo ya ziada" ambayo inaweza kushambulia ikiwa hilo litatokea.
Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa la Marekani alisema Washington inafahamu kuhusu mashambulizi ya mshirika wake, lakini haikushiriki, akielezea operesheni hiyo kama "zoezi la kujilinda".
Baada ya mashambulizi ya Israeli
Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari amethibitisha kuwa mashambulio ya kulipiza kisasi ya Israel dhidi ya Iran yamekamilika.
"Tulifanya mashambulizi yaliyolengwa na sahihi dhidi ya malengo ya kijeshi nchini Iran - na kuzuia vitisho vya mara moja kwa Taifa la Israeli," alisema.
hagari aliionya serikali ya Iran kwamba Israel iko tayari kulenga shabaha zaidi nchini humo ikihitajika.
"Tutajua jinsi ya kuchagua shabaha za ziada ... na kuzipiga ikihitajika. Huu ni ujumbe ulio wazi, yeyote atakayeitishia Israel atalipa gharama kubwa,” alisema.
Karibu kwa maoni
Na Jeff Massawe
0757722557