2019
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 3,130
- 4,735
Toka Gaza ikumbwe na mashambulizi ya Israel hakuna nchi ya Kiislamu iliyothubutu kukemea unyanyasaji huyo kwa raia lakini 🇮🇷 imethubutu mara kadhaa kusema huenda ikaingia na kusababisha mzozo kuwa mkubwa zaidi.
Saudia iko wap na uwezo wake?
Qatar je kwann wasitoe hata vifaa?
Misri jirani kabisa lakini kimya?
Ni aibu kubwa sana kuona ndugu yako akionewa na ww huchujui hatua yeyote
Uislamu ni undugu undugu wao kwa Palestina uko wapi zaidi ya unafiki.
--
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian ameionya Israel kwamba eneo la Mashariki ya Kati linaweza kudorora ikiwa haitasitisha mashambulizi dhidi ya Gaza.
Alisema Marekani pia ndiyo "ya kulaumiwa" kwa kutoa msaada wa kijeshi kwa Israel.
Saa chache baadaye, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwatahadharisha wanajeshi wake kuwa katika vita vya kuokoa maisha yao na kusema vita dhidi ya Hamas ni "fanya au ufe".
Iran inaunga mkono Hamas, ambayo ilishambulia Israel wiki mbili zilizopita na kuua watu 1,400, na Hezbollah ya Lebanon.
Zaidi ya Wapalestina 4,600 wameuawa katika muda wa wiki mbili zilizopita huko Gaza, kwa mujibu wa wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas, na Israel ilitangaza siku ya Jumamosi kuwa inazidisha mashambulizi ya anga.
"Ninaionya Marekani na wakala wake Israel kwamba ikiwa hawatakomesha mara moja uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya halaiki huko Gaza, lolote linawezekana wakati wowote na eneo hilo halitaweza kudhibitika tena," Bw Amir-Abdollahian alisema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran.
Alisema kuwa matokeo yanaweza kuwa "makali, machungu" na "kuwa na athari kubwa", kikanda na kwa wale wanaotetea vita.
Waziri huyo wa mambo ya nje aliongeza kuwa uungaji mkono wa kijeshi wa Marekani kwa Israel ni ushahidi kwamba mzozo unaoendelea Gaza ni "vita vya uwakilishi vinavyofanywa na Israel kwa niaba ya Marekani".
Maafisa wakuu wa Marekani pia wanaonya kwamba mzozo huo unaweza kuenea.