Iran ni nchi ya maajabu sana

Kumbe Israel wanapewa fedha za kujilinda na America?😎 Kweli wachovu
Mkuu si umeona jinsi Marekani imeahidi kuwasaidia tena mamilioni ya dola waisrael na pia kutuma meli na ndege za kivita, baada ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu kuwaomba ili waweze kufanikisha vita vyao na Hamas.

Sasa kama Hamas tu kikundi kidogo kisichokuwa hata na askari elf 40, tena watumia silaha za kienyeji inawafanya waombe msaada mungine zaidi kutoka Marekani, je nchi hiyo inaweza kuwa na nguvu au ubavu wa kupambana na nchi yenye historia ya kupambana vita zaidi ya miaka elf 2 iliyopita na haijawahi kumsujudia Mmarekani au nchi yoyote ile?
 
Israel sasa inalipua chochote kilichopo Gaza. Haijalishi iwe shule, kambi au Hospital ya UN au mtu binafsi. Wamarekani na maseneta wao wote ni wanafiki wakubwa. Na hii ndio sababu ya Israel kufanya chochote bila kufanywa kitu na Marekani wala nchi yoyote yenye nguvu au ushawishi.
 
Hao vijana wengi wao wanaongelea ushabiki tu, lakin uhalisia hawaujui.

Israel leo inatolewa kamasi hata na kikundi kidogo kisichokuwa na askari hata elf 40 (hamas) tena chenye silaha za kienyeji kama rocket na mizinga ya kurusha.

Sasa huo ubavu wa kupambana na Iran watautoa wapi?
 
Wanaweza kutoboa kwasababu yuko jirani na nchi ambazo hazifungamani upande wowote na zile zinazopingana na magharibi, kama Urusi, Uturuki, China, Azerbaijan, Armenia etc
Hili ndilo jibu la yote. Kwa hiyo ni kama hajawekewa vikwazo vile. Huduma zote anazipata vizuri tu kwa hizo nchi
 
Hili ndilo jibu la yote. Kwa hiyo ni kama hajawekewa vikwazo vile. Huduma zote anazipata vizuri tu kwa hizo nchi
Israel ni sawa na katoto kadogo kanakojaribu kuchokoza watu wakubwa (Iran) ili kakiguswa kakimbilie kwa baba yake (Marekani) na wajomba zake (Umoja wa nchi za Ulaya) waje kumsaidia kupambana.

Bila udhamini wa Marekani na kuungwa mkono na Ulaya kiukweli Israel ingekuwa nchi nyepesi na ya hovyo sana kama walivyokuwa miaka ya nyuma kabla ya kushikwa mkono na wanaojifanya wababe wa Dunia.
 
Siri ya iran kufanikiwa ni kujitambua wao na mahitaji yao. Wengine hata mkifunguliwa milango mkaingia kila kona bila viza mtabakia kuwa vilaza tu. Mnapokea misaada hadi ya pedi mna akili kweli?
 
ulitaka Marekan wahamishe kambi?
 
Siri ya iran kufanikiwa ni kujitambua wao na mahitaji yao. Wengine hata mkifunguliwa milango mkaingia kila kona bila viza mtabakia kuwa vilaza tu. Mnapokea misaada hadi ya pedi mna akili kweli?
Jamaa wako vizuri mno kichwani. Miaka zaidi ya 2000 iliyopita waliowahi kuwa na Empire ambayo ilidumu kwa muda mrefu.

Sasa leo hii kanatokea kanchi kenye miaka Mia tatu tu toka kaanzishwe, eti kanakuja kuwatishia nyau na kujaribu kuwapangia jinsi ya kuishi watu wazima wenye akili zao.
 
ulitaka Marekan wahamishe kambi?
Nazungumzia ujasiri na uwezo waliokuwa nao Iran kwa Marekani. Ingekuwa nchi nyingine zingeigwaya Marekani.

Sana sana zingeishia kulalamika tu na kuliacha jambo lipite bila wao kuchukua hatua yoyote. Hii tunaona hata kwa Iraq yenyewe, ingawa hawahitaji tena jeshi la Marekani kuendelea kuwa katika ardhi yao lakini hawana uwezo wa kuwatoa au kuwalazimisha waondoke.
 
Ila sidhanii kama Americant ataendelea kukaa iraq
Acha tuone ila Americant anaondoka Iraq ni suala la muda tuuu
 
Ila sidhanii kama Americant ataendelea kukaa iraq
Acha tuone ila Americant anaondoka Iraq ni suala la muda tuuu
Marekani kuondoka Iraq sio rahisi mkuu, ukizingatia pale kuna masilahi yao muhimu wanayapata kwa bure kupitia kile anachodai kupambana na magaidi.

Labda kama Iraq itataka kushirikiana kwa njia ya siri na Iran kupitia yale makundi ya wapiganaji yanayodhaminiwa na Iran. Yani Iraq iwe inatoa mchongo wa njia, silaha za kimya kimya (sio mpaka wasubiri zivuke kutoka Iran) washiriki kuwapa wapiganaji hao siri ya kile kinachoendelea katika kambi hizo.

Hapo kwa namna fulan wataweza kuwafanya Marekani wakimbie kama Afghanstan maana itakuwa ni mashambulizi ya usiku na mchana bila kupumzika.
 
Do akili hizi za walokole bana

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 

Siku nyingine uwe unaongea kwa takwimu sio insha nyingi
msaada ambao israel inapokea n 2B sasa unasemaje mabilion ya fedha kutoka US
si hivo tu US inawapa palestina,Rwanda,n nchi mbali mbali misaada tofauti ni kuwa wanafanyia nn!

Lakini hujaeleza kua Iran pia baada ya sanction ilitegemea bidhaa za magendo,na nchi za Asia

Lakini pia kuna nchi kama North korea ambayo vikwazo vimedunda pia
Ni akili tu za watawala
 

Mkuu mtu akikusikiliza anaweza akasema unaakili kumbe akili zako zinasoma kurudi nyuma[emoji23][emoji23][emoji23]Kweli kuna machizi wenye IQ

Hujaeleza ilikuaje US ikawa inapeleka hizo ela Israel?? na hujui hadi leo kwann?? (so usibwabwaje usichokijua)
Kati ya waarabu na waisrael wapi wapo wengi ulaya na US ?? kwann sasa hzo hela haziendi nchi za kiarabu


Eti kama taifa teule kwann wanashinikiza vikwazo!!?? bado hujui
Adui mwombee njaaa (nadhani hii nayo huijui)

Ushindi upo katka kumdhoofisha adui na si kumuacha akue. Hakikisha unammaliza adui kabisa kabisa (kasome 48rules of power)

Israel inatumia slogan hii

β€œif the enemy want to kill you, wake up and kill him first”

ukielewa hapa hutaandika uo ujinga ulioandika siku nyingine
 
Kwa Middle East Iran ni nchi ya pili kwa kuwa na Wayahudi wengi baada ya Israeli, hivyo usihangae maarifa yao.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Siku nyingine uwe unaongea kwa takwimu sio insha nyingi
msaada ambao israel inapokea n 2B sasa unasemaje mabilion ya fedha kutoka US
Nilijua tu kuwa atatokea myahudi wa kisukuma aje kuwatetea wayahudi wa kizungu bila kuwa na fact ya kile anachotetea.

Umesema siku nyingin niwe naongea kwa takwimu, lakini wewe mwenyewe ulieni quote unashindwa kuweka takwimu ya ulichoandika. Yani wayahudi wa Chato mnachekesha sana mnapoingia kichwa kichwa na mihemko yenu kuwatetea wayahudi wa kizungu ambao nina hakika hawawafahamu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Angalia picha hapo chini ili ujifunze hii fact iliyo katika takwimu kama inafanana na kile ulichotoa kichwani kwako mwenyewe bila ya kutafiti.

si hivo tu US inawapa palestina,Rwanda,n nchi mbali mbali misaada tofauti ni kuwa wanafanyia nn!
Misaada wanayopewa Palestina ni ya kinafiki, hauwezi kufananisha na ile ya kiyahudi kwa sababu kadhaa ambazo wewe myahudi wa kisukuma hauzijui.

A. Misaada wanayopewa wapalestina ni ya masharti maalumu yani hawaruhusiwi kuitumia kununua silaha yoyote ambayo wanaweza kuitumia kujilinda. Ila wanayopewa Israel ni ruhusa kununua silaha au kuitumia kutengeneza silaha zao wenyewe, kuboresha jeshi lao nk.

B. Misaada wanayopewa wapalestina ni kwa ajili ya kununua madawa, chakula na huduma zingine za kawaida. Ila wanayopewa Israel ni ruhusa kuitumia kuimarisha jeshi lake, kuboresha silaha zake kwa ajili ya kupambana na majirani zake na zingine wanazitumia hadi kuwajengea watu wao katika ile ardhi ambayo sio ya kwao na sheria za kimataifa, ikiwepo hiyo Marekani yenyewe haziwaruhusu kujenga.
Lakini hujaeleza kua Iran pia baada ya sanction ilitegemea bidhaa za magendo,na nchi za Asia
Yes kutumia magendo ndo ujanja, ubabe na uwezo wenyewe. Nchi nyingi ziligwaya, zilianguka kiuchumi, kijeshi na kiuongozi baada ya kuwekewa vikwazo na Umoja wa mataifa.

Leo hii Israel achilia mbali kuwekewa vikwazo, hata wakinyima misaada na Marekani kwa muda wa miaka mitano tu. Itakuwa nyang'a nyang'a kama Cuba ambayo leo hii limebaki jina tu ila uchumi wa nchi na jeshi ni hovyo kabisa.
Lakini pia kuna nchi kama North korea ambayo vikwazo vimedunda pia
Ni akili tu za watawala
Vikwazo vya North Korea ni tofauti na vile vya Iran. Inatumika nguvu kubwa zaidi ya vikwazo kwa Iran kwa sababu mbili kubwa.

1. Geography yake ya kuwa karibu na nchi ya Israel, ambayo inaifanya Marekani, USA, UK na umoja wa Ulaya wahofie kwamba Iran isipowekewa vikwazo vya silaha, na uchumi basi kuna uwezekano mkubwa wa siku moja nchi hiyo ikafanya kitu ambacho watu wengi hawatokitegemea kutokea huko Israel na mashariki ya kati kwa ujumla.

2. Historia yake, kama nchi yenye historia ya kuwa na nguvu pamoja na jeshi bora kwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita, hata kama hauipendi Iran na hauna ujuzi wa historia, lakini nakushauri uingie google usome kuhusu persia empires, au uende kwa biblia ukaisome historia ya uajemi.

Ni tofauti na vinchi kama US ambavyo vimeanzishwa miaka mia tatu tu iliyopita na waingereza.
 

Attachments

  • Screenshot_20240112-122650.jpg
    105.1 KB · Views: 2
  • Screenshot_20240112-121127.jpg
    74.3 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…