Iringa: Kanisa Katoliki lawazuia waumini walioshiriki kongamano la Mwamposa kutopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu mpaka watakapoungama

Wapo sahihi zaidi ya asilimia 90000. Kanisa katoliki hali entertain, ushirikina, mazingaumbwe na miujiza ya kimagumashi. Hata hivyo hao watu walishaliasi kanisa katoliki kwa kufanya ibada tofauti na mifumo ya kanisa, kukataa baadhi ya mambo ambayo ni msingi wa kanisa katoliki, sasa muumini ukashiriki hizo ibada halafu urudi tena. Kama wamevutiwa waende huko huko wakaongeze idadi. Kanisa katoliki ni tajiri wa waamini halibembelezi waamini, halifanyi promotion za kuvutia watu kujiunga kwa kuwashawishi kwa fedha, au kuwaoza wake wengi kama wengine wafanyafyo. Kanisa katoliki ni kuwajibika na sio kudekeza
 
Kanisa la Roman Catholic Iringa limefukuza na kutoa onyo kali kwa washirika wake waliohudhuria kongamano la Mwamposa na wengine walionunua maji na mafuta kwenye mkutano wake

View attachment 2236071
View attachment 2236072
mbona wanagombania waumini sasa haileti picha nzuri ikiwa wote wana hubiri neno la Mungu na kuanza kuonesha kama kwamba wao ni wakamilifu kuliko wahubiri wengine
 
Unamaanisha baada ya yesu hakuna mkiristo anayeweza omba na akakubaliwa maombi!?
Kwani tunaongelea maombi, au miujiza? Miujiza ya utajiri! Ghafla tu kwenye mpesa inaingia milioni 10, baadaye zinaingia milioni 7 nyngine!

Eti hazijulikani zilipotoka! Na baada ya hapo unaanza kuzitumia! Na hii ni baada ya kutoa laki kwa Nabii! 🤔 Ni wajinga pekee ndiyo watakao amini huu utapeli.
 
Katoliki na walokole wote so no wa yesu!?
Wengi watakuja na kusema tulitoa people kwa jina lako na kwa jina lako kufanya miujiza mingi ndipo atakaposema ondokeni kwangu maana sikuwajua kamwe.Ni kama kwenye mpira kuna wanachama na mashabiki huwezi kuwatofautisha.Hivyo kuna mashabiki wa Yesu na Mwili wa Yesu.
 
Unamaanisha kuwa dhehebu jingine la kikristo, nje ya ukatoliki ni dhambi ?
Kanisa Katoliki halina shida na madhehebu mengine! Ila lina shida tu na waumini baridi na wale vuguvugu.

Waumini baridi ni wale wasio enda kanisani, wasioshiriki kwenye Jumuiya na pia wasioshiriki sakramenti mbalimbali za Kanisa!

Waumini vuguvugu ni wale bendera fuata upepo! Mguu mmoja nje, mguu mmoja ndani! Wale wanao amini maji ya Mwamposa yana upako, wanao enda kwa waganga wa kienyeji na kupewa mahirizi, wale ambao wanafanya matambiko, nk. Halafu wakati huo huo bado wanajitambulisha kama Wakatoliki.
 
You people are conservatives.
 
Sasa kama wanapotoshwa wanafundishwa MBENGO ZEMEFONGOLEWA si wapigwe pin
 
Shida hiyo miujiza au pesa wanazolipa!?
 
Walokoke mashabiki wa yesu,wakatoliki mwili wa yesu!?
 
Mwaposa anahudumia watu kiroha Zaid ya elf kumina tano kwa siku wew Ni Nani useme muhuni subiri utupiwe uchawi utatumia Yale maji taka usitake
Watu elfu kumi na tano ni nini mbele ya watu bilioni na zaidi??
 
Haisaidii, wakitaka kwenda kwa hiyari yao wataenda tu.
Inasaidia. Mkatoliki hukatazwi na Kanisa kwenda dini nyingine kama umeamua hivyo. Wanachokuambia ni kwamba usiwe mguu mmoja huku na mwingine kule. Kama wana nia ya kuhamia huko, waende tu ila wasirudi huku kupokea Sakramenti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…