Iringa: Kanisa Katoliki lawazuia waumini walioshiriki kongamano la Mwamposa kutopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu mpaka watakapoungama

Iringa: Kanisa Katoliki lawazuia waumini walioshiriki kongamano la Mwamposa kutopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu mpaka watakapoungama

Nyakati hizi waumini wanabembelezwa sana maana makanisa ni mengi unaweza ukaenda kusali kanisa lolote tu ila katoliki mapato yatapungua
Wakatoliki hatubembelezi mtu,kwasababu hata Yesu Kristo mwenyewe hakumbembeleza mtu ukikosea anakupa makavu,ukitaka kumfuata au kumuacha ni juu yako mwenyewe.Rejea Injili ya Yohane Sura ya sita,aliposema kuwa "Alaye mwili wake na kuinywa damu yake ana uzima wa milele",Wafuasi wengi walikwazika sana kwa maneno hayo hivyo wakarudi nyuma,yeye hakuwabembeleza zaidi sana aliwahoji wale mitume wake kuwa"Ninyi nanyi mwataka kuondoka??".Kwa hiyo hakuna kubembelezana kwenye hbr za kuutafuta Ufalme wa MUNGU.Hata Petro aliwahi kuambiwa na Yesu "Rudi nyuma yangu shetani",leo hii Padre au mchungaji amwambie hivyo muumini uone kivumbi chake lkn Petro alibaki na Yesu.Hakuna kubembelezana narudia.
 
Daah so sad kanisa limeanza kujishtukia. Ila wale waumini viherehere kila jambo wanaenda kushtaki kwa paroko sijui huwa wanawaza nini
 
1 .Hatutamzika kwa sababu aliendaga kwa mwaposa.....
2 .Hatutamzika kwa sababu tunajua wazi ni changudoa na alitembea na wazee wa kanisa...mara amezaa na mume wa mtu

3 .Hatutamzika kwa sababu hatoi mchango wa jumuiya na tena hatutabatiza watoto wake

Wakatoliki na walutherani tumwogopeni MUNGU
...ikiwa MUNGU aliingia agano na kahaba rahabu...ikiwa MUNGU aliingia agano na kijakazi wa Ibrahim aliyezaa naye kwa kumbariki mwanae leo sisi tumekalia kuwahukumu wenzetu
 
Kuna story moja ndani ya biblia ipo very interesting, inafanana sana na wanachofanya hao mapadre wakatoliki,

Yohana 9: 16...., nakazia mstari wa 22 na 25
Nimeshangaa juu ya tamko lao kuhusu uponyaji wa magojwa, nanukuu:

"Tunakemea na kubeza mafundisho potofu ya uwongo (bandia) kama vile ...kuwaponya wagonjwa, ..."

Yesu mwenyewe alisema:

Yohana 14:12​

Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

Maana ake kama vile Yesu alivyoponya magonjwa, na wafuasi wake wanaponya magonjwa, nk. Sijajua wanatumia maandiko gani kwa hili!!!
 
Unaanzaje kumzuia mtu kumuabudu MUNGU?
He mbona tunaenda kwa waganga na walozi Kisha tunarudi kanisani hatufukuzwi?
Kanisa ni kwa wale tuliowaovu sio wasafi, hata YESU alikuja kwa ajili ya waovu
Umeshasikia mtu kazuiwa kumwabudu MUNGU kisa alifumaniwa?
Ishu hapo ni kuhusu kuchanganya imani,mtu abaki ktk Imani moja.
 
Kama ni kweli wamekosea. Uhuru wa kuabudu ni haki ya kikatiba.
Uhuru wa kuabudu ni haki yao na ndio maana hawazuiliwi kuhamia huko kwa Mwamposa ila kila kanisa lina katiba na miiko yake.
Chagua kubaki RC na uishi kwa kanuni na amri za huko au uondoke ukaishi kwa namna ya huko
 
Back
Top Bottom