Iringa: Polisi yakana madai ya kada wa CHADEMA, Vitus Nkuna kushambuliwa na wasiojulikana barabarani, yasema alisababisha ajali kutokana na ulevi


Kwani hao ndugu walishaacha kubambikizia watu kesi?
 
Tena hawakumpiga vizuri vizuri.ilitakiwa afundishwe na kushikishwa adabu mpaka pombe imtoke kichwani mwake.
 
Pele limempata mkunaji 🤣🤣hapo lucas kafurahi kweli kweli anabubujika machozi ya furaha kuona kada wa CDM alikua tungi kama vile CCM hakuna walevi 🤣🤣🤣🤣
 
Your browser is not able to display this video.
Baada ya kujisambazia taarifa kwenye ukurasa wake wa X kuwa ameshambuliwa na kupigwa na watu Wasiojulikana aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana chadema (BAVICHA) Kanda ya Nyasa Vitus Nkuna amekamatwa na polisi .

Imeelezwa kuwa Nkuna alikuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa na kusababisha ajali na kushambuliwa na wenye gari aliloligonga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa SACZP Alan Bukumbi akitoa aarifa kuhusu kukamatwa kwa kada wa Chadema mkoa wa Iringa Vitus Nkuna kwa kosa la kutoa taarifa za upotoshaji mtandaoni ya kuwa amevamiwa na kushambuliwa na watu wasiojulikana.

SACP Bukumbi amesema kada huyo wa Chadema Vitus Nkuna mnamo Tarehe 30 Septemba 2024 katika eneo la Mgongo kata ya Nduli Barabara ya Iringa-Dodoma akiwa anaendesha gari aina ya Volkswagen Touareg yenye rangi nyeusi na mamba za usajili T 797 DYC alisababisha ajali kwa kuligonga gari aina ya TOYOTA Probox yenye namba za usajili T 975 EDC mali ya kampuni ya KINGS.

Aidha baada ya ajali hiyo mtuhumiwa Vitus Nkuna alipimwa kipimo cha ulevi na kukutwa ana kiwango kikubwa cha kilevi katika damu yake kiwango ambacho hakikubaliki.


Chanzo: matukiodaimamedia
 
SOKOMOKO kazua balaa!!
 
alipimwa akakutwa yupo chakari huyu Nkuna sio wa kumtetea si ndo yy alieiba uchaguz alafu kamat kuu ikatengua ushindi wake
Una ushahidi alipimwa na nani na hicho kipimo kimethibitishwa na nani? ubora na usalama wake ukoje? kina hifadhiwa na nani? kibali cha kupima kilitolewa na mahakama ipi?
 
CHADEMA na ulevi wamefunga ndoa. Wapiga kura hawawezi ruhusu kuongozwa na walevi.
 
Una ushahidi alipimwa na nani na hicho kipimo kimethibitishwa na nani? ubora na usalama wake ukoje? kina hifadhiwa na nani? kibali cha kupima kilitolewa na mahakama ipi?
Maswali ya kijinga- Nkuna anakula mvua jiandaeni kumchangia mke wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…