Iringa: Polisi yakana madai ya kada wa CHADEMA, Vitus Nkuna kushambuliwa na wasiojulikana barabarani, yasema alisababisha ajali kutokana na ulevi

Iringa: Polisi yakana madai ya kada wa CHADEMA, Vitus Nkuna kushambuliwa na wasiojulikana barabarani, yasema alisababisha ajali kutokana na ulevi

Ndugu zangu Watanzania,

Inaonyesha CHADEMA imejaa walevi wa pombe na wanaopenda sana ulevi na unywaji wa pombe kupita kiasi.inaonyesha wao na Pombe ni damu damu.nazani pia mnakumbuka mchungaji peter Msigwa aliwahi kumtuhumu naibu katibu mkuu Benson Kigaila kuwa alinyweshwa sana Pombe siku moja Kabla ya uchaguzi wa kanda ya Nyasa na kambi ya mpinzani wake.

Pia mnakumbuka kiongozi wao pia mkubwa Alilewa sana pombe akiwa Dodoma mpaka kudondoka na kuumia Mguu wake na kusingizia alivamiwa. Watanzania tusiruhusu hawa watu wakapewa madaraka maana watauza Nchi kwa kupewa Pombe .watasaini na kusainishwa Mikataba Mikubwa wakiwa wamelewa chakali mpaka Taifa lipate aibuView attachment 3112762View attachment 3112763

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Kwani hao ndugu walishaacha kubambikizia watu kesi?
 
Mbali na mienendo na maadili.

Huyu mtu kalewa kagonga gari, anatakanl kusema anajua kila mtu anayeendesha gari?

Ati watu wasiojulikana walimtwanga.

Anajua Road rage?

Yaani unigongee gari langu na ulevi wako halaf? na akaenda polisi baada ya hapo.

Hawa kila kitu wanataka kusema ni kwa sababu za siasa. Ati ni kada wa CHADEMA, so what? Mlevi ni Mlevi tu, haijalishi ametokea chama gani.

Anyways, najua kuna kampeni(ona nyuzi hapa JF) kabambe zinazowaandama polisi.

Wakome huo upumbavu..
Tena hawakumpiga vizuri vizuri.ilitakiwa afundishwe na kushikishwa adabu mpaka pombe imtoke kichwani mwake.
 
Pele limempata mkunaji 🤣🤣hapo lucas kafurahi kweli kweli anabubujika machozi ya furaha kuona kada wa CDM alikua tungi kama vile CCM hakuna walevi 🤣🤣🤣🤣
 
Baada ya kujisambazia taarifa kwenye ukurasa wake wa X kuwa ameshambuliwa na kupigwa na watu Wasiojulikana aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana chadema (BAVICHA) Kanda ya Nyasa Vitus Nkuna amekamatwa na polisi .

Imeelezwa kuwa Nkuna alikuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa na kusababisha ajali na kushambuliwa na wenye gari aliloligonga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa SACZP Alan Bukumbi akitoa aarifa kuhusu kukamatwa kwa kada wa Chadema mkoa wa Iringa Vitus Nkuna kwa kosa la kutoa taarifa za upotoshaji mtandaoni ya kuwa amevamiwa na kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Kada.jpg

-ux277h.jpg
SACP Bukumbi amesema kada huyo wa Chadema Vitus Nkuna mnamo Tarehe 30 Septemba 2024 katika eneo la Mgongo kata ya Nduli Barabara ya Iringa-Dodoma akiwa anaendesha gari aina ya Volkswagen Touareg yenye rangi nyeusi na mamba za usajili T 797 DYC alisababisha ajali kwa kuligonga gari aina ya TOYOTA Probox yenye namba za usajili T 975 EDC mali ya kampuni ya KINGS.

Aidha baada ya ajali hiyo mtuhumiwa Vitus Nkuna alipimwa kipimo cha ulevi na kukutwa ana kiwango kikubwa cha kilevi katika damu yake kiwango ambacho hakikubaliki.


Chanzo: matukiodaimamedia
 
Jeshi la Polisi mkoani Iringa limemkamata kada wa Chadema, Vitus Nkuna kwa kusababisha ajali mnamo Septemba 30, 2024. Kamanda wa Polisi, SACP Allan Bukumbi, ameeleza kuwa Nkuna alikuwa anaendesha gari akiwa na kiwango kikubwa cha ulevi, hali iliyosababisha kugonga gari la kampuni ya KINGS.

Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa Twitter siku ya Jumatatu, Nkuna alidai kushambuliwa na watu wasiojulikana. "Nimeshambuliwa na watu wasiojulikana nikiwa barabarani hapa Iringa," aliandika.

Aliongeza kuwa baada ya kufika kituo cha polisi, viongozi wa Chadema walifika kumuunga mkono.

“Tunatoka Kituo Kikuu cha Polisi Iringa na naelekea kwangu. Kesho tutajua nani alikuwa wanataka kunikamata barabarani usiku huu kwa kunizuia mbele na nyuma. Tutaujuza umma kwa kila hatua”, alisisitiza Nkuna katika chapisho lingine.

Jeshi la Polisi limekanusha madai hayo, likieleza kuwa hakukuwa na shambulio, na tukio hilo lilitokana na ajali iliyosababishwa na Nkuna mwenyewe akiwa amelewa.

SOKOMOKO kazua balaa!!
 
alipimwa akakutwa yupo chakari huyu Nkuna sio wa kumtetea si ndo yy alieiba uchaguz alafu kamat kuu ikatengua ushindi wake
Una ushahidi alipimwa na nani na hicho kipimo kimethibitishwa na nani? ubora na usalama wake ukoje? kina hifadhiwa na nani? kibali cha kupima kilitolewa na mahakama ipi?
 
CHADEMA na ulevi wamefunga ndoa. Wapiga kura hawawezi ruhusu kuongozwa na walevi.
 
Una ushahidi alipimwa na nani na hicho kipimo kimethibitishwa na nani? ubora na usalama wake ukoje? kina hifadhiwa na nani? kibali cha kupima kilitolewa na mahakama ipi?
Maswali ya kijinga- Nkuna anakula mvua jiandaeni kumchangia mke wake
 
Back
Top Bottom