Mambo mengine bwana! Kwa hiyo kwa maoni yako maeneo ya Jerusaleem na Tela Aviv hayana umuhimu?
Usiku huu nimeangali kwenye TV jinsi Iron Dome zilivyo zidiwa na maroketi ya wapalestina - yaani aibu tupu, mbwembwe zote za kuipigia debe na propaganda uchwara kwamba Iron DOME ndio baba lao kumbe wapi? Nilishangaa zilipo rushwa roketi tano Tela Aviv - Dome ikadhibiti moja tu nne zikapenya - sasa wanakuja na visingizio eti roketi za kipalestina wamezifanyia marekebisho zinaruka parallel na aridhi hazichukui mtindo wa ki-projectile hivyo si rahisi kuonekana kwenye scanning radar ili system ifanye mahesabu ya uhakika wapi pa kuzi-intercept - nilipo sikia kisingizio hicho cha Wayahudi nilicheka sana na kuwasikitikia, nikajua hapo Iran imekwisha wapa mbinu na wafunzo Wapalestina jinsi ya kuwazidi kete Waisrael.
Usiku huu tena nikaona matela yamebeba vifaru kwenda Gaza eti kuwamaliza wapiganaji wa kipalestina wanao rusha roketi, yaani mara hii Israel imekwisha sahau vifaru vyake vilivyo teketezwa huko Lebanon 2016 baada ya kuingia kichwa kichwa huko, hawakuamini macho yao, leo hii tena mjinga huyu Natenyahu anataka Wayahudi wapate balaa nyingine tena kwa kuvamia Gaza - hataki kuondoka madarakani anag'ang'ania kama luba - anaogopa kushtakiwa akiondoka madarakani - vita hii ndio itamumaliza kisiasa - akumbuke kwamba vita hii wapalestina hawapo peke yao huko Gaza,watasaidiana na kundi la Hezibolla,Wairan, Syria, Wa Lebanon na Waturuki,yaani dalili zinaonyesha Wapalestina wamejipanga kweli kweli ku-deal na ujeuri wa Natenyahu na genge lake vilivyo, wamefikia hatua ya kuvurumisha mpaka roketi za masafa marefu yenye uwezo wa kusababisha uharibifu mkubwa sana sana, nimeona kwenye TV live madhara ya makombora hayo si mchezo, Israel hisipo kuwa makini this time around watakuja kuaibika.