Watu wanaoshabikia sana hii vita ya Hammas dhidi ya Israel,lakini ukweli ni kwamba,Sio Hammas wala IDF atakayepoteza baada ya vita hii bali ni wananchi wa Palestina. Kwanini? Angalia sababu hizi:
1.Kwani baada ya Vita Hammas hapotezi chochote? Ni kwamba,Hammas ambao majengo yao rasmi pale Gazza hayajulikani wao kazi yao ni kuvurumisha makombora kuelekea Israel tu,Makombora baadhi hutunguliwa na mifumo ya Ulinzi ya Israel,Mengine huangukia Maeneo ya Wazi na Machache huweza Ku-HIT Target na kusababisha Madhara kwa Wananchi wa Israel. Baada ya kurusha Makombora Hammas hujificha na hivyo kuwa vigumu kwa Israel kujua walipo.
2.Kwanini Israel Haipotezi baada ya Vita? Ukweli ni kwamba,vita nyingi kati ya Israel na Hammas husababishwa na POLITICAL TENSION huko Israel. Netanyahu amekalia kuti Kavu huko Israel,kupunguza TENSION ya kisiasa huko Nyumbani,huamua kuzusha Msala wowote ule wa Kivita dhidi ya Hammas. Mfano,yaani vita hii imetokana na Mpango wa Israel kuondoa Makazi 6 ya Wapalestina yaliyobaki huko Jerusalem Mashariki kitu ambacho hakina Mantiki kabisa.
3. Kwanini raia wa Palestina ndio wanaopoteza mwisho wa Vita hii? Kwasababu,Baada ya Hammas kushambulia Israel kwa Makombora na kujificha kusiko julikana na hivyo kumpa ugumu Israel jinsi ya Kutarget kambi za Hammas. Kwa kuona hilo,Israel hana Chaguo zaidi ya kutuma Makombora ya ndege na Drones kwenye Majengo yenye rais wa Palestina na kutangaza kwamba amelipua kambi za Hammas ili kuwaridhisha raia wa Israel waone kwamba serikali yao iko inalipa kwa kile kilichofanywa na Hammas. Mwisho wa Siku raia wengi wa Palestina hufa,wengine kuachwa Vilema na wengine bila Makazi.
Mfano Mzuri ni hili ghorofa ambalo limeangushwa na Israel huko Gazza katika harakati za kujibu mashambulizi ya Hammas. Wapalestina wengi hapo mwisho wa vita wataachwa bila Makazi huku raia wa Israel waliobomolewa paa zao na Makombora ya Hammas wakijengewa Nyumba nzuri zaidi kabisa.
View attachment 1782197