Is the risk worth it ? kununua pikipiki mpya, uitoe kwa mkataba wa faida ya “elf 3 kwa siku”,kisha uigawe bure baada ya miezi 13 ikiwa bado mpya

Daaah poleni vijana mapambano ni mapambano.
 
Pikipiki 10 ni shilingi milioni 28, faida ya miezi 13 ni milioni 11

Ni heri ununue bajaji 2 kwa milioni 17, kabla hujaziachia bure umelamba faida ya milioni 11
Milioni 17 huwezi kupata Bajaji 2.
Bajaji sasa ni 10M na chenchi kidogo
 
Mnapenda kuwananga wasomi wakati wengi ndio mabodaboda huko mtaani ni vile huwezi mjua mwenye degree na asiye nayo.
 
Nilishasema sana,kuwa hizi biashara za boda boda na bajaji ni uwekezaji mbaya sana wa pesa,bajaji nako ndio majanga tu,eti uwekeze milioni 10,harafu kwa siku uingize faida ya kama 7000?!!mwenye kuuza machungwa tu ambaye mtaji hata laki haufiki anaweza ipata hiyo pesa,
 
sasa hapo, mtaani kuna lipi la kujifunza hapo...namba haziongopi bana, kama biashara Haina faida ni Haina faida, usomi unasaidia kukupa mwanga ni biashara Gani uifanye au usifanye, kwa kuangalia projected profit na resources unazotaka ku invest
 
Niliwahi kununua Bajaj mbili na kuwapa Vijana, naijutia kupoteza hela yangu

Vijana wakawa ni wasumbufu, hawaleti kipande baadaye ikawa ni hasara tu

Bora hela yangu ningeenda kuilia Bata tu, maana unaweza kujikuta unaua bila kukusudia
Hapo ilitakiwa bajaj moja uendeshe wewe mwenyewe halafu nyingine ndio umpe kijana. Kinyume na hapo lazima ule za uso.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…