cassavaleaves
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 1,799
- 2,237
View attachment 2851446
Israel inaishambulia makazi ya watu, inaua watoto, wanawake, wagonjwa, waandishi wa habari, na hata wafanyakazi wa umoja wa mataifa
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anasema kwamba tangu kuanzishwa kwa UN haijawahi kutokea wafanyakazi wake wengi kuuawa kwenye vita kama walivyouawa na Israel
Matamko na maazimio kibao ya umoja wa Mataifa yameitaka Israel kusitisha vita lakini imejibu kwa kiburi kuwa itaendelea na mauaji hayo hata Umoja wa Mataifa usema nini
John : Kuna usemi vita haina macho, lakini kuna mambo mengi katika yanayotokea katika vita, lakini nikitaka kujikita tu katika wigo wa hoja yako, wafanyakazi wa UN Gaza maybe 99% Wako UNRWA ( Unite Nations Relief and Works Agency for Palestine Refugee) Na Waajiriwa wengi wa hilo shirika ni Wapelestina wenyewe wanaoishi hapo hapo Gaza, hivyo tegemea kwa njia moja au nyingine lazima wakumbwe na maafa ya vita kwa njia moja au nyingine, hilo haliepukiki.
Lakini pia kumekuwa na shutuma nyingi mno kwa hilo shirika la UNRWA, kwa vile ndilo linatoa msaada hapo Gaza, wa kujenga Mashule, Hospitali na misaada mingi ya kijamii nk, limekuwa kimya mno Hamas inapotumia infrastructures za UN kama kujenga Mahandaki, kutumia misaada ya vifaa kwa ajili ya vita, na mateka baadhi walioachiliwa wamedai walikuwa wamefichwa katika sehemu za UNRWA.....Kwa kifupi baadhi ya wafanyakazi wa UNRWA moja kwa moja hapo Gaza wameshindwa kuwa neutral, baada ya tu ya tukio la October 7, baadhi ya Wafanyakazi wa UNRWA moja kwa moja walitumia mitandao ya ofisini kupongeza tukio hilo, hii ililetea shida UN na ilishindwa kutoa tamko la wazi kupinga hilo.
Hivyo msimo wa Israel umekuwa kutojali chochote kile kutoka UN kwani wanaona wazi iko biased in favor of Hamas! Matamko mengi yanakuwa kwa upande wao wasimamishe mapigano, lakini haionyeshi Hamas ifanye nini. Usalama wa taifa lao ni muhimu kuliko kitu chochote kile, kama agenda ya UN hawaisadii wanaipuuza tu, na kujua mara nyingi haina meno yoyote yale.