Israel kutangaza vita na Hezbollah muda wowote kuanzia sasa

Hii ndio itakua vita hasa sio ile ya Hamas na IDF kuviana hii vita Hezbollah wanaitamani sana miaka mingi wanaonekana wamejiandaa kwa muda mrefu sana
Mkuu; Hilo tusiliombee kwa sababu IDF bila shaka anamjua vizuri sana huyo mpinzani tarajiwa(Hezbollah) kuliko Hezbollah anavyojifahamu yy mwenyewe.
Hiyo haitakuwa ni vita bali ni maangamizi. Nani abaki kusimulia kilichotokea - Hezbollah au IDF ????. Tutasubiri kipenga cha mwisho.
 
Si kila ambacho vyombo vya habari vikubwa vinazungumza ikawa ni kweli, maslahi yapo mbele zaidi. Hata mashirika ya kimataifa yanatumika katika unyonyaji.

Vita inayoendelea middle east ni vita dhidi ya waliokataa unyanyasaji na unyonyaji dhidi ya wezi.

Mozambique ni vita ya maslahi.
Congo vita haiishi kwa sababu za kimaslahi, hao hao unaowaita wakubwa ndio wachochezi kuharibu amani nchi za watu.

Palestine wanapambana dhidi ya weI wa ardhi yao. Full Stop.

Hata kwenye bible zilikuwepo dola kubwa zenye nguvu lakini walikua waovu wakubwa.
 
Kuna nchi moja inataka kuiga Israel bahati mbaya amezunguukwa na wanaojitambua na kila akiingiza watu wanachinjwa myakimyaki mpaka anaogopa
Huyo achana naye - ni mchovu ana fumble tu hajui anachokifanya.
 
Sasa kwa hali ilivyo kaskazini mwa israel, Israel anajipanga jinsi ya kulipiza kisasi kwa akili mno wakati Mkuu wa intelijensia anawajua udhaifu wa vikosi vya miguu, anga vya israel pamoja na mifumo miwili ya ulinzi wa anga
 
Hawafahamu Hezbollah wewe unadhani ni Hamas hao 😂

Soma historia Israel alikimbia mwenyewe ajaribu kuipiga Lebanon huone moto wake.
 
Quote:
"Mozambique ni vita ya maslahi.
Congo vita haiishi kwa sababu za kimaslahi, hao hao unaowaita wakubwa ndio wachochezi kuharibu amani nchi za watu."
Hii 👆 👆 👆 nimeipenda mno kwa sababu ndo ukweli wenyewe.

Hiyo ya Palestina siiafiki sana kwa sababu Mpalestina hataki kujifunza kwamba kila akitumia nguvu kupambana anapigwa na ardhi inazidi kutwaliwa i.e. inamegwa.

Kumbe angelitafuta njia nyingine mbadala (alternative B) aone kama atafanikiwa au la. Sio kung'ang'ana tu na matumizi ya ngvu ilhali ameshajua fika kwamba huyo anayepambana naye sio size yake.
 
Hawafahamu Hezbollah wewe unadhani ni Hamas hao 😂

Soma historia Israel alikimbia mwenyewe ajaribu kuipiga Lebanon huone moto wake.
Haya tusubiri. Ila vita sio nzuri kamwe. Tumwombe sana Mungu atuepushe na hilo.
 
Kuzidi zile 300 za Iran?
 
Kwamba Hezbolla itaweza kuhimili mkiki wa mabomu 60 kwa siku za ndege za IDF? au unawatakia matatizo raia wa Lebanoni? Yaani unashangaza sana
Israel imepiga zaidi ya hayo mabomu kwa zaidi ya uzito wa atomic bomb liliopigwa pale Hiroshima kwenye kaeneo kadogo kama Gaza.
Je amewamaliza Hamas?

Toka ww2 Israel imevunja rekodi kwa kutumia uzito mkubwa wa bombs kwenye eneo dogo la Gaza, hadi ICJ kuingilia usifikiri ni mchezo.

Alijitia anawamaliza Hamas, Je wamekwisha, cha ajabu vifaru vyake na IDF soldiers wanauawawa huko Rafah.

Sasa we unazungumzia mabomu 60.

Israel itaweza kuhimili Tel Aviv kushambuliwa kwa mizinga mizito?
 
Unafikilia Israel anaweza akaingia ndani ya Lebanon na kujimwambafai kama anavyofanya Gaza???
 
Kwamba Hezbolla itaweza kuhimili mkiki wa mabomu 60 kwa siku za ndege za IDF? au unawatakia matatizo raia wa Lebanoni? Yaani unashangaza sana
Unajua Jamaa nao wana kitu gani wameficha mpaka siku ya real battle?? Mi sipebdi vita kabisa maana madhara ni makubwa mnoo maana Hezbuollah wana makombora yasiozuilila na mfumo wa ulinzi wa kisrael na pia uwezo wa israel kijeshi ni mkubwa na hapendi kushindwa hapo ndio shida sasa
 
Kupigana na hamas tu, Israel inaomba mksada ya siraha na pesa kila siku. Je, akianzisha muziki na hezibollah hli itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…