Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Ndugu maneno ya wanasiasa sio ya kuyaamini asilimia 100 hasa wakati wanatafuta kura. Mwanasiasa akikwambia sasahivi ni usiku,toka nje uthibitishe.
Kuna video niliiona Youtube kuna mchambuzi fulani jina limenitoka, ni raia wa Marekani kijana mdogo sio maarufu sana. Baada tu ya Trump kuchagua mawaziri wake,alisema kabisa Trump kachagua watu wapenda "damu" na utawala wake utakuwa na vita nyingi tu na alisema kabisa Trump ataishambulia Iran kwa sababu watu aliowaweka kwenye cabinet yake ni Anti- Iran hasa waziri wa Ulinzi Pete Hesgeth. Kwa wakati ule ilionekana kama utani maana Trump alikuwa hana hata miezi mingi madarakani lakini kwa sasa utabiri wa yule mchambuzi unatimia.
 
Vita ya Ukraine na Russia alisema ataimaliza ndani ya siku 2
 
Hivi hayo makombora hayawapati wale waandamanaji vipenzi wa Nchi za magharib? Maana isiwe unasema inawatetea huku inawaua
 
Hii vita ya nchi na nchi madhara hayatakua makubwa kama yale ya Israel na Hamas, Hii vita target itakua Miundombinu ya kijeshi, nishati, pro regime wa Ayatollah Khamenei, wakubwa wa jeshini na njia za kiuchumi.
Ubaya wa vita ni kwamba inaanzaga hivi hivi mmoja anapiga vituo muhimu tu kama jeshini au viwanda vya silaha....ila mwingne yeye anavurumisha bomu litue popote ilimladi litue ardhi ya mpinzani.

Sasa hapo ndo ubaya unaanzaga mwisho wa siku kila mmoja anaanza kuvurumisha mabomu kwa raia wa mwenzake ilimladi tu mmoja a surrender.
 
CDF wa Iran ameliwa kichwa. Sasa sijui nani atatoa komandi?


View: https://www.instagram.com/p/DVS4FVelTrK/?igsh=MTEyMnM2Nnk5bWw2bA==
Hata kwenye ile vita ya siku 12 Israel walipita na CDF na baadae aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya CDF Israel walimuua. Israel wamefanikiwa kuwa na taarifa za kijasusi zinazowawezesha kuwaua viongozi wa juu wa kijeshi wa Iran. Huu ndio mfupa ambao Iran umemshinda hadi sasa,kuwalinda viongozi wake wa juu dhidi ya mashambulizi ya Israel.Hata Rais wa Iran alijeruhiwa wakati wa vita ya siku 12 na inasemekana yule rais wao aliyekufa kwenye ajali ya ndege ni Israel walihusika
 
Nilichobaini ni kwamba Marekani wana maadui wao ambao hawawezi kugeuzwa marafiki kupitia power ya uraisi.
 
Hata kwenye haya mashambulio ya leo kuna raia wamekufa, hakuna vita ambayo raia wasio na hatia watanusurika. Hata wakati wa kukamatwa Maduro kuna maiti za raia zilitapakaa barabarani. Vita haina macho. Ni vile tu wahusika watasema walilenga maeneo fulani lakini hakuna namna raia wasidhurike,hiyo haipo
 
Anaeilinda ni Mungu au US?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…