Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Usinilishe ambacho sijaongea, umezungumzia Ndege comments kibao zilizopita, hayo ya Silaha umeyatunga sasa hivi.
Cyprus na huko kwingineko ni marekani ndio amefanya hivyo.. Mimi naongelea ndege za Israel sio marekani

hakuna airbase ya Israel iliyopigwa na Iran, picha za satellite za base zilizopigwa zipo ila hakuna ya Israel kama ipo leta hapa

F-35i adir,F-15i raam na F-16 sufa zote zinatoka Israel mzee
 
Cyprus na huko kwingineko ni marekani ndio amefanya hivyo.. Mimi naongelea ndege za Israel sio marekani

hakuna airbase ya Israel iliyopigwa na Iran, picha za satellite za base zilizopigwa zipo ila hakuna ya Israel kama ipo leta hapa

F-35i adir,F-15i raam na F-16 sufa zote zinatoka Israel mzee
Hakuna Ndege za Israel zote ni za Marekani, kuna Ndege za Marekani za Israel na za Marekani za Marekani, zote zikitoka ni Amri moja.

Lete ushahidi hizo Ndege zinatokea Israel kuja kupiga Iran na kurudi Israel.
 
Iran kazi anayo🔥
 

Attachments

  • TEHRAN___Mashambulizi ya anga Jijini Tehran-Iran.__UWANJA WA MAONI UKO WAZI_ ___israel _us _ir...mp4
    1.4 MB
Ayatollah alikataa special protection.
Tofauti na viongozi wa nchi za mgharibi ambapo kiongozi huonekana kama rasilimali na inapaswa kulindwa kwa gharama yeyote ile, kitu ambacho humuweka kiongozi mbali na watu wake.
Hii inapelekea kiongozi kulindwa kwa ulinzi maalumu, kulindwa kwa mifumo ya kijasusi, kuwekwa nyuma amachini ya saruji imara ambapo anakuwa mbali hata watu wake kumfikia.

Kwa mujibu wa Ayatollah aliona jambo hilo ni kama kuweka tabaka na mgawanyo usio sawa baina ya watu wake anao waongoza na yeye ambae ni kiongozi.

Khamenei aliamini kwamba kama kiongozi na mfano wa kuigwa unapaswa kuishi sambamba na maisha ya watu na mateso wanayopitia.

Khameni hata kwenye vita ya miaka minane baina ya Iran na Iraq. Licha ya kuwepo tishio la wazi dhidi ya maisha yake, aliendelea kubaki katika mji mkuu uliokuwa ukishambuliwa kwa mabomu na makombora, akiishi katika makazi yake ya kawaida huko Jamaran, ili watu waelewe kuwa kiongozi hayuko tayari kujihifadhi katika hifadhi maalumu na zisizo za kawaida wakati watu wake hawana fursa hiyo.

Tabia hii ilikuwa ujumbe rahisi lakini wenye maana kubwa ya kwamba kiongozi asipojiweka katika kiwango cha walio dhaifu zaidi na wasio na fursa katika jamii, hawezi kudai kuwa anaelewa maumivu na mateso ya makundi mbalimbali ya jamii, na hivyo hukosa sifa za uongozi.

Hivyo ndivyo Ayatollah alivyokuwa na alitekeleza azimio hili la kimaadili kwa uzito kamili.

Kuna muda wakati vyombo vya usalama vya Iran walikuwa wanapata intel za vitisho vya kijasusi na kumuasa Ayatollah afanyiwe ulinzi maalumu, Ayatollah alijibu na alisisitiza kuwa mtindo wake wa maisha lazima ulingane na wa watu na uwe katika kiwango chao.

Hivyo hata viongozi wa ngazi za juu wa Iran jeshini na serikalini walifuata falsafa yake hio kama kiongozi wao.

Hivyo inashangaza watu kuona kuuawa kwa Ayatollah ni kama Israel na US walifanya ujasusi wa hali ya juu sana, na wengine wakishangaa kwanini viongozi wa Iran na wakubwa jeshini wanauawa sana, ni kwa sababu wanaishi katika falsafa hio. hivyo wao ni easy target.

Kama Hamas walificha mateka 200 ndani ya Gaza, eneo dogo ukubwa wa wilaya, wakawaficha mateka wale, Kutoka Israel kwenda Gaza unafika kwa baiskeli, lakini licha ya intelligence ya Israel inayosifika na nguvu za jeshi lao, na jinsi walivyofunga mipaka ya Gaza na walivyoipiga Gaza ikawa magofu, bado hawakuweza kupata mateka.

Israel ikaona ikubali imeshindwa na kuamua kubadilishana mateka kitu ambacho waliona wamefeli, mateka wakaachiwa wengine walikuwa wana afya, you can imagine baada ya miaka miwili na kikundi ambacho hata kifaru hawana.

Sasa tujiulize kwa jinsi Iran ilivyo kubwa walishindwa kuficha viongozi wao?


Kwa jinsi Iran walivyo mbali na Israel walishindwa kufanya ulinzi wa viongozi wao kwa siri?

Jibu ni hapana, viongozi wa Iran wana namna yao ya uongozi, kama adui anatuua basi atuue sote nikiwa na watu wangu, siwezi kupewa ulinzi maalumu hali ya kuwa watu wangu wanauawa.

Hivyo ngonjera za humu jamiiforums watu wanakejeli , kucheka na kuwaona Iran ni wajinga, labda niseme wao ndio wajinga.

Iran wana intel nzuri tu iliyo sambaa middle east yote. Hivyo si watu wa kuwachuulia poa.

Ayatollah amekufa kwake akiwa na familia yake licha ya vitish vilivykuwa vikiendelea, ajabu watu wanaisifu US na Israel kwa huo ugaidi.

Shame!!!
 
Hakuna Ndege za Israel zote ni za Marekani, kuna Ndege za Marekani za Israel na za Marekani za Marekani, zote zikitoka ni Amri moja.

Lete ushahidi hizo Ndege zinatokea Israel kuja kupiga Iran na kurudi Israel.
Logical fallacy 😀

siwezi kutoa ushahidi kwenye madai ya uongo, picha za satellite zimezagaa sana nitafutie ya base za Israel ulete hapa
 
Hii kazi sio ya Israel, ni mhuni USA
 

Attachments

  • Strikes on Iran_s capital_ Tehran_ continue after the initial combat operations were jointly l...mp4
    2.8 MB
Hakuna Ndege za Israel zote ni za Marekani, kuna Ndege za Marekani za Israel na za Marekani za Marekani, zote zikitoka ni Amri moja.

Lete ushahidi hizo Ndege zinatokea Israel kuja kupiga Iran na kurudi Israel.
Kuna uongo kuuvumilia ni kazi sana. Israel hana ndege?
Zote zikitoka ni mari moja? Zinazofanya mashambulizi sasa hivi huko Lebanon, amri inatoka marekani?

Ndege zinazoshambulia Iran zinatoka wapi?
 
kwanza mwanzo mlisema ayatola kapelekwa sehem salama, mlivoona ameliwa kichwa msemo ukabadilika, eti anaishi kama alivo wananchi wake, wavaa kobazi hamkubali kuzidiwa hoja nyie. ameuliwa yeye. mke wake hadi na wajukuu wameliwa kichwa. kama hakuna tech yeyote ya kisasa ebu jaribu wewe tukuone... rusha hata kombora moja tuone litatua wapi. kuua vio gozi 48 kwa mpigo unafikiri ni jambo la kawaida sio? hiyo ni akili boss hiyo sio ilimu akhera... ni ilimu dunia hiyoo shehee
Ayatollah alikataa special protection boss, alikataa kabisa.
Intel ya Iran ilimuambia wakamuweke mahala salama akakataa.
Hakuna intel yoyote ya ajabu Israel na US walitumia.

Kama wana intel, ilikuwaje katika mateka 200 waliotekwa na Hamas, wasipate hata mmoja, hali ya kuwa walifanya ground invasion na wakafunga anga la Gaza? unaelewa ukubwa wa Gaza unaingia mara nagpi kwa Iran, unaelewa umbali wa Gaza na Israel?

Hivyo hakuna maajabu yeyote, Ayatolaah alikuwa very easy target.
 
Logical fallacy 😀

siwezi kutoa ushahidi kwenye madai ya uongo, picha za satellite zimezagaa sana nitafutie ya base za Israel ulete hapa
Huyo mtu uongo upo kwenye damu. Sijui anapata raha gani

Kabisa mtu anasema hakuna ndege za Israel?

Ungemuuliza ndege zinazoshambulia Iran zinatokea wapi.? Ungemuuliza pia zinazoshambulia Lebanon muda huu nazo zinatokea wapi
 
Iran inaanza kumfikilia Pakistan. Inasemekana Kambi za kijeshi za marekani zilizoko Pakistan ndio zinazofuatilia na kufanya udukuzi wa movements za kijeshi za Iran zaidi huko Balochinstan. ( Paf base Samungli).

Hawa jamaa kobazi hawaamini, vita vya siku 12 hawa Pakistan walijifanya wako upande wa Iran. Akiishambulia Pakistan wao nao wananyuklia. Lakini ni kama kuwapa haueni India ambao ni machawa wa Israel na Maadui wa Pakistan.

Iran hii kazi peke yake itamshinda mapema, angeongezeka mchina tu au kiduku au Russia peke yake wangetembeza kichapo dunia nzima. Ila akisema apige kila mwarabu lazima aishiwe Pawa.
 
Back
Top Bottom