Eti yaani mm katika kitu huwa kinanikera kwa Irani ni hicho tu.
Mfano lile shambulizi la mwanzo lilio uwa khaminei na viongozi wengine, zaidi ya miezi mitatu Marekani na Israel walikuwa wanatangaza kabisa kwenye vyombo vya habari kabisa kuwa wanaweza kuwalenga viongozi na kuwauwa ili kuchochea uasi dhidi ya serikali, ila katika mazingira kama hayo eti unakusana lundo la maafisa wakuu wa usalama unakutana nao ikulu sehemu ambayo kabisa unajua kuwa ni target rahisi kabisa.
Yeye Khamenei kama alikuwa hajali maisha yake kwa sababu ya umri wake vipi kuhusu maafisa wengine?
Mfano huyu Ralijan Israel yenyewe imekili kabisa kuwa kuuawa kwake kumewezeshwa na kuonekana onekana kwake hadharani kila mara licha ya uhatari wa usalama uliyopo.
Sasa kulikuwa na ulazima gani wa yeye kushida kwenye mitaa ya Tehran eti akifanya maandamano?
Mm nadhani pia kuuawa kwao kutasaidia kuondoa hawa wazee wanao leta mitazamo ya kidini hata kwenye mambo yanayo hitaji akili ya kawaida tu kuyatatua.
Mfano huyu Khamenei washauri wake walimuonya sana mwaka 2018 kuwa Iran bila kuwa na silaha za nyuklia Iran haitokuwa salama dhidi ya Nchi za magharibi,
Tena kwa kipindi hicho Iran alikuwa na nafasi kubwa ya kutengeneza silaha za nyuklia kwa sababu kulikuwa na mazingira magumu sana kwa Israel hata Marekani kuishambulia ila yeye akakataa eti uislamu hauruhusu kuwa na slaha za nyuklia hivi suala na kujihakikishia ulinzi na penyewe kunahitaji fatwaa za kidini?