Lidafo
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 995
- 2,329
Mkuu KhaibarKwa udogo wa kijiografia wa Israel na anavyochangiwa na hizbollah,sidhani kama Israel ataweza kuhimili vita zaidi. Ukiona Trump anahangaika negotiations jua anayetafta kuokolewa ni Israel kuliko USA mwenyewe.
Unalosema ni kweli kabisa.
Kijiografia Iran inaweza kustahimili vita Vya muda mrefu kuliko Israel kwakuwa Iran ni kubwa kieneo takribani 1.6 milioni Km² Idadi ya watu takribani milioni 85 wakati Israel Ina 22,000 km² na watu takribani milioni 9.7
Hivyo Iran ana advantage kwenye vita Vya muda mrefu maana Wana maeneo mengi ya kuhifadhi silaha na ya kujificha + maeneo mengi ya kijeshi na viwanda Vya silaha.
Kwa upande wa Israel shambulio Moja kubwa Lina athiri miji mikuu na kupelekea athari za uchumi kwa haraka, athari kwa watu na miundombinu kwa haraka zaidi
Iran analijua hili vizuri ndio maana ana mlazimisha Israel waende vita Vya muda mrefu.
Sasa factor Moja ya kijiografia haiwezi kutumika pekee kupima mwenendo wa vita Kuna factor kama za Uchumi na uwezo wa kijeshi, Lakini Bado hizi nazo kitaalamu zina mpa nafasi nzuri zaidi Iran kwenye vita Vya muda mrefu.. Kivipi?
Tukianza na Uwezo wa kijeshi na vifaa Iran Ina makombora ya masafa marefu, drones nyingi na inaweza tumia proxy groups kama Hizbullah, Hashd al-Shaab , Houth n.k lakini pia Iran inatengeneza silaha zake nyingi ndani ya nchi Tena kwa uwezo wa kujitisheleza.
Kwa Upande wa Israel wao Wana teknolojia ya juu ya ulinzi wa anga Iron dome, Arrow-3 + ujasusi wa juu kwenye ku- eliminate + ndege zenye Kasi na uimara F-35 n.k
Lakini changamoto Yao kubwa Israel wanategemea sana misaada ya marekani hasa silaha kubwa , makombora na vipuri.
Hivyo, Kitaalamu Israel ni mzuri kwenye vita Vya muda mfupi lakini akilazimishwa kuingia vita Vya muda mrefu(Kama anavyolazimishwa sasa na Iran) hawezi kustahimili kwa maana mpinzani wake (Iran) ana wigo Mpana wa kupambana muda mrefu kutokana na ukubwa na uzalishaji wa ndani.
Ukija kwenye factor nyingine ya uchumi hapa nitagusia kwa ufupi sana nimechoka ku-type duuh!
Israel ana uchumi wa kisasa lakini mdogo hivyo akishambuliwa bandari, viwanja Vya ndege na sekta ya nishati hatoboi.
Upande wa Iran wana uchumi unaohimili shinikizo kwa kuwa wamezoea vikwazo Vya muda mrefu, Hivyo vita Vya muda mrefu kwao ni Hali ya kawaida.
Kwahiyo mkuu unayosema Israel inaomba ceasefire kupitia marekani nakuunga mkono kabisa kwa maana ni ngumu Israel kutoka hadharani kusema anaomba ceasefire hivyo anatumia marekani kama mlango wa nyuma wa kupunguza mapigano bila kuonekana dhaifu.