Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Ni sawa mwanaume aliwe tundu aseme nimeliwa kidogo.
Aibu na jambo hilo halikutegemewa..Wataandaman ila jibu ni moja aibu...aliyeuliwa ukiangalia kauli zake zilikuwa za kibabe amekkufa kiboya boya sana...potea na mawazo hayo utakufa na presha.
Hao wajiite Dunia nzima..wahuni watapagonga hapo kama Syria..pataisha mtakuja kulia lia humu free Iran free Iran..Wazungu ni wahuni hawana hizo stori zenu za kelele nyingi.
 
Tupe namba ya kukutumia rambirambi bosi.
 

Haaa! Aiseeh
Mkuu wewe hujui mambo ya kijeshi na medani za kivita.

Na pengine huenda hujui kadiri kiongozi wa kijeshi anavyokuwa na cheo kwanini ulinzi wake unaongezwa.
Ungejua hivyo ungeelewa Kwa nini Israel na USA na wafuasi wao kwao huo ni ushindi mkubwa

Vita Siku zote ni mpige Mchungaji na kondoo watatawanyika wenyewe. Hiyo Kanuni inatumiwa na Majeshi yote yenye nguvu.

Sasa Hiyo Iran anachofanya ni kuhadaa walimwengu na pengine kujitetea maskini.

Unarusha rusha mabomu hovyo, hata uchome Ikulu, au mji mzima kama kuna watu wakubwa hujawaua hiyo vita haijaisha.

Wewe anapigwa mkuu wa majeshi na Ayatollah sasa nani aliyebaki kwenye nchi??
Majeshi yapi? Kama yameshindwa kulinda viongozi wao wataweza kujilinda wao wenyewe?

Iran sasa hivi ipo kwenye mfumo, inatagemea tuu utashi wa Trump
 
Alikufa Nyerere na Tanzania bado ipo na mamluki wanaotaka kuleta vita kina Kittima wanashughulikiwa ipasavyo na wagalatia wenzake, Tena sasaivi ndio Tz haicheki na nyau kabisa .....hata Iran kufa kwa huyo babu sio ndio mwisho wa Taifa lao.

Huyo Babu hajafa. Sema ameuawa kikatili na kama Mbwa mwizi.

Tofautisha Kufa NAA kuuawa.

Hiyo ni Vita Mzee.
 
Iran kashambulia Cyprus, Iran anaamini anaweza kuanzisha vita ya Dunia🤣
Mbona taarifa yako imelalia upande mmoja? Kwamba kakurupuka kuishambulia cyprus? Nikufungue hicho kichwa ipo hivi USA/IDF wameona ni threat assets zao zikibaki middle east kheri kuzihamisha haraka wakataka kuzipeleka uturuki wakakataliwa ndio kuzipeleka cyprus kwa hiyo Iran kuishambulia cyprus kuna ubaya gani kama yeye amewapokea USA/IDF
 
Mbona sijasikia popote kuwa Russia na China wanam-backup Iran?

Russia anawezaje kutoa msaada hali ya kuwa naye anauhitaji wa msaada?

Huyu mchina nadhani ni mtu ambaye hataki kuwa involved na vita yeyote, hata kwa Urusi sidhani kama Mchina alimsapoti Russia.
 
Utamfichaje kiongozi kama hakuna vita. Wanaanzisha vita kwa njia ya kustukiza kwa kuuwa viongozi. Na hiyo inaweza kutokea ktk nchi yoyote ile kama adui yako anataka kuanzisha vita kwa njia hiyo
 
Hio mbinu ya kuua makamanda wa kijeshi kwa Iran imeshaonyesha haifanyi kazi..
Mwanzoni Israel alifanya sana covert ops za kuua wanasayansi kwa kudhani kwamba kuua wanasayans wale vichwa wa sayansi ya atomic wangefanikiwa kabisa kusimamisha projects zao kitu ambacho waliona ni kupaka rangi upepo.

Ndipo wakaanza mashambulizi ya moja kwa moja na hadi US kushambulia vinu vya nuclear, na hapo hawajafanikiwa, sasa wamerudi tena...

Na hili hawatofanikiwa maana dalili zote zinaonyesha Israel hii vita anakwenda kuomba ceasefire. Maana wamejaribu kuwatafuta top commanders wawaue lakini hawajafanikiwa sana.

Vita iliyopita waliua top commanders karibu 30, hivi sasa top commanders wamekuwa makini sana. Wapo mahala wanatoa maelekezo, na nafasi zote zipo replaced kazi inaendelea. Na waliuawa kwa kusthukizwa kwa mbinu chafu ya Trump kusema wanafanya mazungumzo kumbe wanaandaa kuivamia Iran.

Iran hairushi mabomu hovyo, ni vile medias zinawadanganya, Iran inapiga kwenye mshono.. ndio kwanza masaa 48 hayajapita lakini Tel Aviv imechakaa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…