Kama kawaida yao, ukishazoea kuua utaendelea kuua tu.
Wale wanaoitwa Taifa teule wameendelea na kazi yao ya kufanya wanachoweza kwa ufanisi mkubwa. Leo wameua wapalestina masikini 100, wasio na silaha, ambao wana njaa wakati wakisubiri msaada wa chakula. Wanajeshi wa Israel limefyatulia kundi la watu risasi na kuua wapalestina 100.
Haya yakiwa yanafanyika kuna watu wanafurahi, wanapenda, wanachekelea na wanatamani hawa wapalestina wasio na hatia wanedelee kuuawa
Taarifa za hilo tukio unaweza kuipata hapa:
hii ni hasara kubwa kwa Mungu, watu wanapokufa. nimekoma, sitaki tena majibizano kuhusiana na huu mjadala wa Israel na Gaza, hata pale nilipochangia Mungu anisamehe kabisa na yeyote aliyekwazika. Mungu hafurahii kifo cha mwenye dhambi hata angekuwa ni gaidi au mwizi.
ajabu ni kwamba, wengi wa hao wanaoua wenzao, na hao wanaouawa, wote hawamwamini Mungu kwa njia sahihi. Waisrael ndio kabisa wamepoteza hata ile imani yao ya zamani ya kumwabudu mungu wa kweli, wamebaki kufurahia hata ushoga, nchi imejaa ushoga, wakati sodoma na gomorah miji iliyoteketezwa kwasababu ya ushoga hata haipo mbali na Israel, ni maeneo ya Jordan hapo. wapalestina nao wanaabudu wasichokijua na kisichookoa. Tunaomba Mungu asaidie hii vita iishe, kwasababu sio watoto na wanawake tu, bali watu wengi pande zote mbili wanakufa, mno.
Tukijikita kwenye maandiko, miaka hii ni miaka ambayo maarifa yameongezeka sana hata vita vimepiganwa kwa maarifa ya sayansi ya juu. Uonapo mambo hayo jua wakati wa Bwana kurudi umekaribia, kwa mtini jifunzeni tawi likishakuwanyauka na kuchipua mnajua wakati wa mavuno u karibu, walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, yeye atakuja kama mwivi, ila mambo ya vita kama hizi, mashariki ya kati, urusi, afrika n.k ni ishara tosha.
mfalme wa kazkazini atakuja kuungana na mfalme wa mashariki dhidi ya Israel (mfalme wa kazkazini ni Urisi na Uturuki, wakati mfalme wa mashariki ni Iran, china n.k), na ukiangalia, kuna tension hizo sana kuonyesha kuan siku hawa wote watakuja kuungana kwenye zile vita vilivyotabiriwa ambavyo ndio siku za mwisho. Mwenye sikio na asikie.