Uchaguzi 2020 Itokee Lissu akashinda Urais, akakupa nafasi ya kutoa pendekezo, ni kitu gani alichofanya Magufuli utamwomba akiondoe mara moja?

Uchaguzi 2020 Itokee Lissu akashinda Urais, akakupa nafasi ya kutoa pendekezo, ni kitu gani alichofanya Magufuli utamwomba akiondoe mara moja?

Mifuko ya hifadhi za jamii
Nilisikia kwenye Fao la kujitoa NSSF (private sector) Magufuli ameongeza muda hadi 2023 badala ya July 2021 iliyokuwepo mwanzo, ni kweli au ni stori tu za vijiweni maana sina source ya kuaminika kuhusu hilo, kama kuna mwenye source ya kuaminika anijuze
 
Wengi nasikia tu mnasema ooh Magufuli hajafanya lolote, ooh katupiga sana nk. Lakini pale ninapouliza baadhi ya watu kwamba ni kitu gani ambacho amefanya Magufuli ambacho unaona hakifai, wengi wanashindwa kutoa jibu la haraka.

Sasa leo ningependa kuwauliza katika mtandao wa JF, kwamba ikitokea Tundu Lissu anashinda kiti cha uraisi, na akakuambia toa pendekezo ni kitu gani ambacho Magufuli alikifanya nikiondoe au kukikomesha mara moja, utapendekeza nini?
Katiba mbovu,kuukuu ya kijima iliyo jaa viraka,jeshi la polisi la kikoloni lifumuliwe,mageuzi ya mfumo mzima wa elimu yetu toka wa kinadharia hadi wa kivitendo,wizara ya elimu iwekwe kikatiba ili wanasiasa wasiichezee,yapo mengi sana
 
Arejeshe fao la kujitoa. Fao hili ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi wa nchi. Kijana akiacha kazi,au akiachishwa au kampuni yake ikifunga biashara akipewa fedha yake aliyoichanga kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii,Kijana huyu ataanzisha biashara, ataendelea kjlipa kodi,ataweza kuajiri watu wawili au watatu.
Well said, haina haja ya serikali kung'ang'ania fedha za watu ambao wamechanga wenyewe
 
arejeshe utangamano haraka sana. sisi na maCCM tushazoea kuishi side by side peacefully.
Kweli hata kumsabahai mtu wa Chadema inakuwa mtihani,hata mademu zetu ambao wapo chadema imekuwa shida kukutana nao,hata kula mizigo imekuwa shidaaaaa wakati zile papuchi hazina nembo ya ccm au chadema
 
Umesahau Jasusi Membe yupo busy akipanga list ya mawaziri, kasema ataishangaza Tanzania atakavyofunga goli la ushindi dakika ya 89 kutokea impossible angle.
 
Kufuta Sheria zote alizozishape kwa interest zake

Kurudisha Uhuru wa habari,
Kupitia watu kukukosoa unapata muongozo wa kuongoza nchi changamoto nyingi za watu unazipata na kuzifanyia kazi lakini ukiongoza kwa akili zako tu
Matokeo ndiyo haya yanayomkuta bwana yule anajaribu kufanyia kazi baadhi ya mambo anayoambiwa akiwa kwenye jukwaa la kampeni wapi na wapi Sasa

Mahospitali naskia operesheni ni laki mbili Sasa hivi kwa wamama wanaojifungua hii imepelekea kutaka kufanyia operation kila mama aneyetaka kujifungua hata Kama ana uwezo wa kutumia njia ya kawaida

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wengi nasikia tu mnasema ooh Magufuli hajafanya lolote, ooh katupiga sana nk. Lakini pale ninapouliza baadhi ya watu kwamba ni kitu gani ambacho amefanya Magufuli ambacho unaona hakifai, wengi wanashindwa kutoa jibu la haraka.

Sasa leo ningependa kuwauliza katika mtandao wa JF, kwamba ikitokea Tundu Lissu anashinda kiti cha uraisi, na akakuambia toa pendekezo ni kitu gani ambacho Magufuli alikifanya nikiondoe au kukikomesha mara moja, utapendekeza nini?
Hatutaki kusikia watu wanaoitwa wasiojulikana. Hatupendi kuishi kwa hofu na kutoaminiana
 
Kunyimana dhamana kwasababu wewe humpendi Magufuli na ccm.

Kuwekwa lumande indefinitely bila kufunguliwa kesi mahakamani.

Kuingia na pesa za kigeni uwanja wa ndege bila kubughudhiwa.

Kupunguza ushuru na tozo bandarini.

Kuondoa mtu mmoja kufanya maamuzi bila kufuata taratibu na ushauri wa kitaalamu.

Kuondoa kuamyabudu rais, ambaye alipaswa awe kiongozi wa wananchi.

Kuondoa kutekana au kutekwa na vyombo vya dola, ili kukutisha utoe pesa.

Kufokea raia wenye nchi yao, kusababisha kumuogopa rais anayejifanya ni Mungu.
 
Katiba mpya.

Fao la kujitoa lirejeshwe.

Nyongeza ya mshahara kwa mujibu wa sheria izingatiwe na waliotakiwa kupanda madaraja na mishahara miaka 5 iliyopita wapewe haki yao.

Wastaafu ambao bado hawajalipwa pesa zao wapewe haki yao.

Kinga ya kutowashitaki baadhi ya viongozi iondolewe.

Wakulima wawe huru kuuza mazao yao (hasa ya chakula) nchi jirani bila kikwazo ikiwa nchi haina upungufu wa chakula.

Iundwe tume huru ya kimahakama kuchunguza matukio yaliyotokea kati ya 2016-2017 ikiwemo utekaji wa raia, kupotea kwa watu na mashambulizi kwa wanasiasa (Tundu Lissu) na raia wa kawaida ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
 
1
Wengi nasikia tu mnasema ooh Magufuli hajafanya lolote, ooh katupiga sana nk. Lakini pale ninapouliza baadhi ya watu kwamba ni kitu gani ambacho amefanya Magufuli ambacho unaona hakifai, wengi wanashindwa kutoa jibu la haraka.

Sasa leo ningependa kuwauliza katika mtandao wa JF, kwamba ikitokea Tundu Lissu anashinda kiti cha uraisi, na akakuambia toa pendekezo ni kitu gani ambacho Magufuli alikifanya nikiondoe au kukikomesha mara moja, utapendekeza nini?
1. Kuifuta katiba iliyopo
2. Kuifuta tume ya uchaguzi
3. Kuifuta bodi ya mikopo ya elimu ya juu
4. Kuifuta / kuliunda upya jeshi la polisi
5. Kuunda majimbo mara moja
6. Kurejesha nyumba zote za serikali zilizouzwa kiholelela
7. Kuifuta Bima ya afya na kuiunda upya
 
Wengi nasikia tu mnasema ooh Magufuli hajafanya lolote, ooh katupiga sana nk. Lakini pale ninapouliza baadhi ya watu kwamba ni kitu gani ambacho amefanya Magufuli ambacho unaona hakifai, wengi wanashindwa kutoa jibu la haraka.

Sasa leo ningependa kuwauliza katika mtandao wa JF, kwamba ikitokea Tundu Lissu anashinda kiti cha uraisi, na akakuambia toa pendekezo ni kitu gani ambacho Magufuli alikifanya nikiondoe au kukikomesha mara moja, utapendekeza nini?
1. Aache mpango wa kujenga uwanja mkubwa wa Mpira Chato
2. Amrudishe Prof. ASSAD na wengine woote walionewa kazini na walipwe mafao yao
3. Arusdishe fao la kujitoa
4. Apunguze saana kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu na awekeze zaidi kwenye maendeleo ya watu kama elimu bora, afya bora na kutengeneza zaidi nafasi za ajira
 
Naona Lisu kaishiwa sasa anatafuta alishwe maneno ya kuongea kwenye kampeni za lala salama baada ya kugundua kuwa mikutano yote aliyofanya hajawagusa wananchi na kitu cha kueleweka

LISU ni mgombea pekee wa uraisi ambaye anamaliza ngwe yake bila kunadi sera za CHAMA CHAKE
 
Back
Top Bottom