Jaji Eliezer Mbuki Feleshi anafaa kuwa AG

Tumuachie MH Rais atamchagua mtu mzuri mwenye busara lkn tukubali tukatae rushwa ipo pale pale
 

Naomba nikukumbushe kuwa si watu wote hupoteza kumbukumbu. Huyu Felesh si ndio yule DDP alificha mafaili ya uchunguzi wa kesi ya wizi wa EPA na KAGODA AGRICULTURE? Kisha akajifanya eti yamepotea ili kuficha ushahidi na kulinda mafisadi walioifisidi nchi. Leo hii unakuja hapa ukihema kwamba anafaa kuwa AG? Kwa vigezo gani wakati ni mmoja kati ya maCCM yanayolinda wezi nchi hii. Usiendelee kutufanya kuwa sisi wote ni wajinga.
 

Hiyo ni perception yako kwa maslahi yako binafsi!; uzoefu wako na Feleshi sio authoritative wala recorded!! sisi wenzio tunampima Feleshi wako kutokana na rekodi yake alipokuwa DPP; wachana na mambo ya lambalamba huko sukari!
Je Feleshi wako ana ubavu wa kusimama kidete akatoa maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa katika maswala ambayo "the oligarchs na grand mafia" wa nchi hii wana maslahi??!! Feleshi anaweza kuivimbia Ikulu kwa maslahi ya Umma? Feleshi ana ujasiri wa kujiuzulu ikiwa ushauri wake utapindishwa kwa maslahi ya mafisadi!!
Akiwa DPP aliachieve nini kama sio kufanya kazi ya kuatamia mafaili ya kesi nzito nzito mpaka kupelekea kutofautiana in public na Edward Hosea wa PCCB!! hilo liko wazi hata katika threads za weakleaks! man; no research no right to speak!

Ofisi ya AG ni nzito sana na ya hatari kubwa sana kwa sababu AG strong atapata maadui wengi sana wenye nguvu za kiuchumi na kisiasa kwa maslahi binafsi; Andrea Chenge alipotamka kwamba hivi ni vijisenti tu! hakuwa na maana kwamba hizo pesa zilikuwa kidogo bali alikuwa na maana kwamba "Eti ninyi mnashangaa hii dola millioni moja wakati kuna watu wamekomba zaidi ya hizo?" (my own take); Political entrepreneurship na the new mafia haviwezi kumuacha salama Feleshi; na Feleshi wako alishathibitisha udhaifu huo akiwa DPP; hana ubavu wa kusukumana na mafisadi; akipewa na apewe; sio jukumu langu na sina uwezo wa kukataa; it will be "fait accompli"! akagange njaa yake lakini sio kwamba ni mtu anayeweza kusimamia maslahi ya taifa come rain or sun!!
 

Vipi kuhusu alivyowabambikia kesi za ugaidi akina Lwakatare na wale vijana wa Igunga, ushahidi ulijitosheleza kuliko ule wa UDA?

Riziwani alimbeba Sana huyu fisadi sijui hata kama anapewa kesi huko mahakama kuu maana anapenda Sana njuruku. Vipi hili gorofa lenu hapa Mwanza mnapangisha dola ngapi kwa square mita?
 
Mleta mada umevurugwa. George Masaju ndiye ayestahili hiyo post na siyo fisadi Feleshi mchumia tumbo na kilaza
 
Usiendelee kutufanya sisi hatuna kumbukumbu. Huyu jamaa si ndio alificha yale mafaili ya kesi ya wizi wa EPA na KAGODA AGRICULTURE na kujifanya eti yamepotea kwenye mazingira ya kutatanisha. Mpaka leo hajatuambia mafaili yako wapi na wale wezi walioiba zile fedha za umma wamefanywa nini. Wanaendelea kupeta mitaani na hata wengine wameiba tena kwenye ESCROW kwa sababu DPP aliwalinda kwenye suala la EPA NA KAGODA. Acha kuendelea kutufanya wajinga.
 
..Feleshi alishastaafu.....na hata kama angekua bado hangefaa...kwa kuwa nae amewahi kuwa na tuhuma tele za kushindwa kushughulikia kesi kubwa kubwa za kifisadi....huyu Felessi ni sawa tu na hawa kina werema...ni uzao ule ule wa mapanya....
 
Inasemekana ID ya Tunkamanini ni ya Dr Eliezer Feleshi, kwa hiyo anapima kina cha maji cha wana JF
 

Strong voice echoing from a solid rock!!!
Patriotic tone!!!!
MTK, this says a lot!!!
 
Last edited by a moderator:
Reactions: MTK
Amini nawaambieni hata aje AG kutoka MBINGUNI, kwa mfumo huu tulionao atachafuka tu.

Kwahiyo aidha AG, anakuwa Feleshi, Masanju, etc nothing will change it is business as usual.

Watanzania tuache kushughurika na MATAWI tushughulike na SHINA.

Yaani Watanzania tayari mmesahau kwamba CCM walitupilia mbali mapendekezo ya Warioba ambapo nafasi kama hizi za uteuzi Warioba alipendekeza ziwe zinadhibitiwa na mamlaka nyingine!

Kweli Watanzania mnaangamia kwa kukosa kumbukumbu!
 

Nakubaliana na wewe 100% kabisa huyu Mhe. Fereshi nimchapakazi sana na ni muadirifu sana kwa muda niliyo interact naye.
 

Kwa mm ambaye simjui vizuri nisaidie hapa;

Uadilifu wa Feleshi na kutokujua "ladha ya pombe" unajaribu kusema nn?

Uadilifu wa Feleshi na ucha Mungu unajaribu kusema nn?

Waiting............
 
Ngoja nikupatie mifano kadhaa:
  1. Kesi ya Ugaidi ya Lwakatare mwaka 2013: Hapa DPP alitumia Nolle prosequi kuifuta kesi yao na baadaye kuwafungulia watuhumiwa kesi ile ile.
  2. Rufaa dhidi ya kesi ya Prof. Costa Mahalu: Baada ya mahakama kumwachia huru Prof. Mahalu, DPP alikata rufaa, lakini cha kushangaza, baada ya Rais kumteua Prof. Mahalu kuwa Mjumbe wa Baraza la Kutunga Katiba (CA), DPP aliifuta rufaa hiyo kwa Nolle prosequi.
  3. Kesi kadhaa za Madawa ya Kulevya pia zilifutwa na DPP katika mazingira tata.

Mambo haya Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikwisha kuyaona na kutoa onyo:

 
Kwa mm ambaye simjui vizuri nisaidie hapa;

Uadilifu wa Feleshi na kutokujua "ladha ya pombe" unajaribu kusema nn?

Uadilifu wa Feleshi na ucha Mungu unajaribu kusema nn?

Waiting............

Soma hiyo post ilikuwa ikijibu nini ndo uulize mkuu..
 

Tunkamanini, here goes a whim!!!!
 
Last edited by a moderator:

Tunkamanini, here goes a whim!!!!
 
Last edited by a moderator:
Tunkamanini, here goes a whim!!!!

Wanasahau kama DPP ni taasisi na pale kuna wakurugenzi wasaidizi kila kitengo na bado kuna wanasheria wa kanda ambao malanyingi ndo hufanya hizo kazi baada ya kumshauri DPP umuhimu wa kufanya hivyo, na mala nyingi huwa kuna kuwa na umuhimu wa kitechnique kufanya hivyo au wakati mwingine hakuna ushahidi na hata wakati mwingine kwa usalama wa nchi ambapo ushauri unatoka TISS na kwa Rais mwenyewe ambaye kumbuka ndo mteuzi wake.
 
Last edited by a moderator:
Hafai. Huyu ndiye alishindwa ku-prosecute case nyingi za rushwa ambazo zilipelekwa kwake na PCCB. Hata huo ujaji alipewa kwa fadhila. Nasema tena - HAFAI
 
Huyu sijui Fenesi mbona EPA ilimshinda akabaki kutupiana mpira yeye na Hosea wa Takukuru,hana weledi alipewa kazi hapo mwanzoni ikamshinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…