Uchaguzi 2020 Jaji Kaijage: Baada ya uhakiki, sasa tuna jumla ya wapiga kura 29,188,347. Vyombo vya Habari vitende haki kwa vyama vyote

Uchaguzi 2020 Jaji Kaijage: Baada ya uhakiki, sasa tuna jumla ya wapiga kura 29,188,347. Vyombo vya Habari vitende haki kwa vyama vyote

View attachment 1541030

Hata hivyo hakusema kama vile ambavyo vitakaidi agizo lake vitachukuliwa hatua gani , na wala haifahamiki kama anayo mamlaka ya kushughulikia vyombo vya habari vitakavyotoa habari za upendeleo , maana tayari hapa kibindoni ninayo orodha ya vyombo vya habari vinavyopendelea mgombea mmoja na kutelekeza wengine
Huyu kaijage kama ana akili sawasawa angeita mkurugenzi wa TBC amwambie lazima itanga LIVe uzinduzi wa kampeni wa chama cha demokrasia na maendeleo siku hiyo ya kwanza.
 
Katika hao wapiga kura waliojiqndikisha
Milion 27 ni kwa Magu
Milio 2 kwa Lisu
Zilizobaki ni kwa Membe na wengineo

Huna ujualo zaidi ya kupiga propaganda mfu hapa jukwaani. Haijawahi na haitakaa itokee wapiga kura wa nchi hii kujitokeza kupiga kura kwa 100%. Kwa taarifa yako kutokana na ushenzi uliofanywa na awamu hii ya tano kwenye chaguzi zetu, hakuna uwezekano wa wapiga kura kufika 20m.

Na hata hiyo 20m nimesema iwapo Lissu hatakatwa kutokana na maagizo ya Magufuli kwa tume ya uchaguzi. Ni iwapo tume ya uchaguzi itatekeleza maagizo ya Magufuli ya kumkata Lisu, wapiga kura hawatavuka 5m. Take it or leave it, that's the story.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ( NEC) mh Jaji Kaijage amesema baada ya kuhakiki daftari na kuondoa majina yanayojirudia sasa wamebakia wapiga kura 29,188,347

Pia ameongeza kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania inafanya uchaguzi Mkuu wa kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais kwa kutumia fedha za ndani. Kiasi kilichotengwa ni zaidi ya Bilioni 331.

My take; Kumbe nyomi ya Tundu Lissu si chochote si lolote.

Maendeleo hayana vyama!
Kura zenu mmeshapiga?
 
Kaijage.jpg
My take; Kumbe nyomi ya Tundu Lissu si chochote si lolote.
Acha bange, Lissu anaingiaje sasa hapo??
 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ( NEC) mh Jaji Kaijage amesema baada ya kuhakiki daftari na kuondoa majina yanayojirudia sasa wamebakia wapiga kura 29,188,347

Pia ameongeza kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania inafanya uchaguzi Mkuu wa kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais kwa kutumia fedha za ndani. Kiasi kilichotengwa ni zaidi ya Bilioni 331.

My take; Kumbe nyomi ya Tundu Lissu si chochote si lolote.

Maendeleo hayana vyama!

kwanini ujiulizi wale wanaojitapa kuwa wana wanachama 6Mil. ?
 
UKichukua wapiga kura 29,188,347 ukagawanya kwa idadi ya vituo 80,155 unapata wapiga kura 364 Kila kituo.
Kila mpiga kura akitumia dakika 5 kuiga kura, hizo ni 364x 5 sawa na dakika 1,820 amabzo ni sawa na masaha 30. Ni ishara kwamba hatutamaliza kupiga kura mpaka baada ya siku mbili. otherwise waje waseme kila kituo tena kiwe na A, b. c,d.. nakuendela.
 
Nijuavyo Mimi ni kuwa wengi hawakujitokeza kujiandikisha sababu ya figisu za chaguzi za marudio na S/M. Sasa sijajua hii 29M inatoka wako,isijekuwa kuna kiasi kikubwa cha hii namba itaongezwa kwenye kura za mgombea urais chama tawala ili ionekane kapata kura nyingi na kufikisha adhma ya 90% ya kura.

Anyway,sisi tutadeal na primary votes za kutoka vituoni,huko ndo namba huwa haidanganyi.
Hawakujitokeza kujiandikisha waishio mitandaoni pekee, mkuu umesahau vipi watu wa mitandaoni wenye kuonyesha vipisi vya laini ya voda vilivyochanwachanwa, kumbe mtu mwenyewe ndio mtumiaji mkubwa wa mtandao wa voda!?
 
Back
Top Bottom