Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi tunaomba muingilie hili kwa mustakabali wa haki. Jaji Salma Maghimbi ni mzigo kwa Mahakama

Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi tunaomba muingilie hili kwa mustakabali wa haki. Jaji Salma Maghimbi ni mzigo kwa Mahakama

Mh jaji mama Salma Maghimbi, kuna mashauri umeyatolea uamuzi toka mwezi wa 5 lakini mpaka sasa umeshindwa kutoa nakala ya hukumu, drawn order na proceedings.

Tunakuomba utupatie nakala husika kwa ajili ya hatua nyingine. Hivi kweli Mh Jaji DRAWN ORDER doc ya page moja ni ya kuchukua zaidi ya miezi 4 mteja kupatiwa?

Tunaomba nafasi yako usiitumie kuumiza wateja wa mahakama. Kumbuka wewe ni jaji mfawidhi mahakama kuu ya dar. Unatakiwa kuwa mfano kwa majaji wengine unaowaongoza
 
Jaji SALMA MUSSA MAGHIMBI Jaji Mfawidhi Mahakama kuu Kanda ya Dar amekuwa akichelewesha kutoa nakala za hukumu pamoja na Drawing Order kwa muda mrefu.

Ninavyoongea kuna hukumu alizotoa toka mwezi wa 5 ila mpaka sasa hajaweza kutoa nakala ya hukumu au drawing orders.

Tunaomba Mahakama immulike na kumshinikia kutoa nakala ya hukumu na drawing order kwa kesi ambazo alishazitolea hukumu/uamuzi.
Huyu Mama ni mvivu na mlipua kazi sana. Anafahamika toka akiwa pale Ardhi.
 
Mh Jaji hututendei haki. Kesi umezitolea uamuzi toka mwezi wa 5 lakini hutaki kutoa nakala za hukumu na proceedings. Tatizo ni nini kwani wewe mama?
 
Kumbe majivuno ya mhimili huu kuwa wapo vizuri kuchapisha hukumu sivyo ilivyo katika uhalisia



01 September 2023

Professor Elisante Ole Gabriel on Sustainable Reforms of the Judiciary System in Tanzania


View: https://m.youtube.com/watch?v=fjvZgxDuKk8
The Judiciary review website Tanzll has a viewership of 82 % making it a front runner in the world of ...
Interview hosted by Austin Makani - Monday Agenda on CapitalTV Tanzania.
Source : AMM Investment
 
Jaji SALMA MUSSA MAGHIMBI Jaji Mfawidhi Mahakama kuu Kanda ya Dar amekuwa akichelewesha kutoa nakala za hukumu pamoja na Drawing Order kwa muda mrefu.

Ninavyoongea kuna hukumu alizotoa toka mwezi wa 5 ila mpaka sasa hajaweza kutoa nakala ya hukumu au drawing orders.

Tunaomba Mahakama immulike na kumshinikia kutoa nakala ya hukumu na drawing order kwa kesi ambazo alishazitolea hukumu/uamuzi.
Kwani nakala ya hukumu ni ombi? Au ni takwa la kisheria kwa yeye kuiotoaa? Sheria inatoa Remedy ipi kwa nakala zinazocheleweshwa maliciously?
 
Mkuu mimi nilikuwa nina shida ofisi flani Dodoma... nilizungushwa wiki nzima.. nenda huku rudi huku..

Ambaye anahusika ndiye ananizungusha na ni mkuu wa idara flan yupo serious kuanzia muonekano na hataki mchezo kwa walio chini yake..
Nikapewa siri.. Kwa shida hii tafuta laki 5 mpelekee asubuhi kwenye bahasha.. Mwambie mkuu nimekuletea shukrani fanya wepesi..
Siku mbili suala liliisha nikaondoka..
Dah!... Inatisha
 
Mh msajili, kwa nafasi yako naomba utumie kanuni ya 90 [5] ya kanuni za mahakama ya rufaha zilizofanyiwa marekebisho 2022 kuhakikisha tunapewa nakala za ruling, drawn order na proceedings baada ya kuisha siku 90 toka tulipoandika barua kwako kuomba nakala ya docs husika pia nyongeza ya siku 14 kuisha baada ya siku 90. Tunaomba umtake jaji SALMA MUSSA MAGHIMBI atoke nakala husika. Ucheleweshaji huu unatushawishi kuamini tuhuma kwamba mama Maghimbi ni mla rushwa jambo ambalo linaathiri haki za watu
 
Mh Jaji Maghimbi tupe nakala zetu za kesi ambazo ulishazitolea uamuzi siku nyingi. Au mpaka tukupe rushwa ndo tupate hizo nakala ambazo ni halali yetu?
 
Na kesi za rushwa wanahukumu wao!
Kwanini hii sheria ya rushwa isifutwe ili iwe halali ukitaka huduma ya umma uinunue na anayekuuzia alipe kodi serikalini kutokana na pato hilo la rushwa?

Maana rushwa haiwezi kwisha Tanzania Takukuru na Polisi ndio vinara wa rushwa na nyumba ya kuhukumu wala rushwa inataka rushwa ili ihukumu wala rushwa.
Niliwahi kuandika hayo:

 
Kuna wananchi ambao kesi zao ziliamuliwa August na September wao haraka sana Jaji Maghimbi aliwapatia docs zao zote kwa wakati. Sisi wa toka mwezi wa 5 na 6 mpaka sasa hatujapatiwa nyaraka hizo, na wala hakuna matumaini kuwa ni lini tutapewa nyaraka hizo. Au mpaka tutoe rushwa kama wao ndo tupatee?
 
Back
Top Bottom