Jaji Warioba: Dkt. Bashiru ajibiwe kwa hoja, hajafanya kosa lolote acheni kumshambulia

Hata mimi kosa la Bashiru sijaliona.

Watanzania sijui tuna pepo gani aisee, sifia sifia hii sijui itaisha lini.

Huku kusifia kila kitu, kule kupinga kila kitu. Mzani haubalance yani.

Wa huku akienda kule nae anaadopt tabia za kule vivyo hivyo sa kule akenda huku nae anasifia kila kitu.

Ni unafiki na ubinafsi tu.
 
Umekosea mkuu hawakosoi maoni bali wanamuattack mtoa maoni.

Bora basi hata yajadiliwe maoni, cha ajabu anajadiliwa mtu.
Mara hana kadi
Sijui kadi hakurudisha , yote hayo yanatoka wapi.?? Ulikua wapi kuyasema kabla?? kwanini hukusema wakati anateuliwa.??
 
Una uhakika kua maisha yamempika kuliko wewe yalivyokupiga?

Acha uroporopo, Acheni watu watoe maoni yao kwa uhuru, Kama ninyi mnavosifu na kuabudu
 
Ni kosa kutoa mawazo ya kinafiki kwa sababu mwenyekiti wake aliyetwaliwa alipenda sifa sana na hakuweza kumshauri haya anayosema hii inamaana angepata nafasi ya kuwa Rais kwa ticket ya ccm,angetaka sifa pia .Ni mfumo
 

..Nadhani uko kinadharia zaidi.

..You are dealing with human beings, not stones.

..kwamba watu wana kumbukumbu, wana hisia, na wana akili zinazofanya tafakuri.

..Wanamkumbuka Dr.Bashiru jinsi alivyokuwa fedhuli na mwenye kiburi cha madaraka wakati akiwa Katibu Mkuu wa Ccm.

..Leo amefikwa na nini kiasi cha kiasi cha kuanza kuwazodoa watawala, na kutetea wanyonge?

..Je, tumuamini tu bila ya kumdadisi? Je, atetewe tu bila kwanza kukiri makosa yake, na kuwaomba radhi waliodhulumiwa wakati akiwa sehemu ya genge la watawala?

..Kuielewa hoja yangu labda nitoe mfano huu mdogo. Hivi mtu ambaye anajulikana kwa kumkashifu Mtume Muhammad, je ana uhalali siku yoyote ile atakayoamua aingie Msikitini?

..Je, waumini hawana haki ya kumhoji kama ame Silimu? Je, hatakiwi kuulizwa kama ametawadha kabla hajaingia Msikitini? Je, aachwe tu aingie Msikitini na viatu?

..Narudia tena, Dr.Bashiru atubu, aombe radhi, ajitenge na ufedhuli na unyanyasaji wa awamu ya 5. Baada ya hapo atakuwa na uhalali wa kutetea uhuru wa maoni.
 
Kwa kuwa alikuwa fedhuli akiongea ukweli unageuka kuwa uongo!?
Mbona kabla ya kuwa ccm hamsemi kuwa alikuwa sio fedhuli mnayoangalia ni hayo ya miaka miwili ambayo hayakuwa furahisha.
Machawa jibuni hoja zake
 
Bashiru kajibiwa, Kajibiwa na Kigwangala kuhusu masuala ya serikali kuongeza bajeti ya kilimo, ruzuku ya mbolea, kufungua masoko n.k
Kama hujaridhika na majibu Hilo ni lingine, Ila Kajibiwa
 
..nakubali Bashiru atetewe.

..lakini itapendeza kama Bashiru atawaomba radhi wale waliodhalilishwa na kuteswa wakati akiwa Katibu Mkuu wa Ccm.
Ninani aliyezalilishwa wakati wa Bashiru?Bashe na Nape ndio walikuwa wakosoaji sana kipindi cha Magufuli, pamoja na ukosoaji Bashe alipewa unaibu Waziri wa kilimo tena Magufuli alimwambia hadharani kuwa kuwa yote uliyokuwa unayakosoa nenda kayafanye,Makamba na Nape Kinana na Ngereja walinaswa wakimtukana Magufuli, lakini aliwapotezea utukusikia kelele za kuwavua ubunge au wanachama.Bashiru kutoa maoni tu kuwa watawala inabidi kutimiza wajibu wao na Sio hisani kwasababu ni waajiliwa wetu nayo imekuwa nongwa,harafu wanasema Samia karudisha democrasia kwenye chama,watu wanatoa maoni yao bila wasiwasi,hiki ni kichekesho kingine.
 
Nasubiri siku Maza atakapopata jukwaa kama atamshambuli ile design ya Ndugai. Hapo ndipo nitajua hizo sifa za kupiga mwingi huwa anazipokeaje moyoni.
Kawatuma au wanajipendekeza?
 
Na linapoteza Kweli !! Tumuombe Mungu sana. !!
 
Watu wanakaripia unafiki wake maana yeye alimtukuza magufuli kuzidi Mungu, aliwa master mind wa ukatili dhidi ya binadamu alioufanya magufuli, halafu leo anageuka kukemea maovu aliyoyaasisis wakati wa magufuli ambaye naye alimpambia kama haa wanavyompambia samia
LAKINI ANAYOSEMA YAKO SAHIHI!
 
Kule mahala vile vichwa vyenye uwezo wa kupangua hoja havipo tena kuanzia mwaka 2010 mwanzoni
 
95 % jamaa ni Selfish !!
 
Kwa kuwa alikuwa fedhuli akiongea ukweli unageuka kuwa uongo!?
Mbona kabla ya kuwa ccm hamsemi kuwa alikuwa sio fedhuli mnayoangalia ni hayo ya miaka miwili ambayo hayakuwa furahisha.
Machawa jibuni hoja zake

..tatizo la Dr.Bashiru ni uongo, ufedhuli, na ukatili, aliokuwa akiuunga mkono wakati akiwa Katibu Mkuu wa Ccm.

..kuna watu walifungwa, wametiwa ulemavu, wamepotezwa, kwa kuwa walikuwa wakosoaji wa Ccm na serikali yake wakati Bashiru akiwa Katibu Mkuu wa chama.

..sikuwahi kumsikia Dr.Bashiru akiwasemea au kuwatetea hao. Sanasana nilimsikia akiwabeza na kutetea watawala wakati wote.

..Dr.Bashiru alipaswa kutubu kwamba alikosea. Kwamba aliunga mkono utawala dhalimu wa awamu ya 5. Akifanya hivyo itakuwa rahisi zaidi kutetewa na wapenda haki, demokrasia, na uhuru wa mawazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…