Jakaya Kikwete: Lowassa alipopata changamoto na kukaa pembeni, tuliendelea kuwa Marafiki

Jakaya Kikwete: Lowassa alipopata changamoto na kukaa pembeni, tuliendelea kuwa Marafiki

Hivi nyie mnaongea nini? Sasa Richmond ilivyobumbuluka, mlitaka Jakaya ndio ang'atuke? Ofcoz ilikuwa lazima Waziri Mkuu ndio asepe. Mnamuonea huruma ya nini? Kwani alivyokubali uwaziri mkuu si alijua consequences zake? Hiyo ndio siasa. Asingetaka siasa angebakia kwao Monduli kuchunga ng'ombe
 
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete ametoa kauli hiyo baada ya kufika kutoa pole ya Msiba nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa aliyefariki dunia Februari 10, 2024 wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Moyo (JKCI).

Akizungumzia kiongozi huyo, Kikwete amesema Mwaka 2005 tulipoteuliwa kugombea Urais, mwenzangu akaja kuwa Waziri Mkuu tukapata changamoto katikati mwenzangu ikabidi akae pembeni, tukaendelea kuwa pamoja kuwa marafiki na kushirikiana kwa kila linalowezekana"

Kikwete ameongeza kuwa Lowassa ametoa mchango mkubwa katika taifa na yaliyotokea ni changamoto katika maisha lakini hayafuti mema na mazuri aliyofanya kwaajili ya nchi.

there is no permanent enemy in politics..

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
Yeye alivyomaliza miaka kumi yake kulikuwa na shida gani yeye akae pembeni amwachie Lowassa apambane?

Makubaliano huwa yanakuwepo. Kama Blair na Brown, Ruto na Uhuru, JK na Lowassa. Uhuru na JK ni ubinafsi, wivu, husuda uliwaongoza.
Acha mambo ya kitoto, yaani uondoke madarakani kisha urithishe urais kwa rafiki yako?
Wakarithishane mali zao siyo nchi ya watu milioni 60.
Kama ulikuwa na kiu ya kutawaliwa na Lowassa ungempigia kura.
 
Hivi nyie mnaongea nini? Sasa Richmond ilivyobumbuluka, mlitaka Jakaya ndio ang'atuke? Ofcoz ilikuwa lazima Waziri Mkuu ndio asepe. Mnamuonea huruma ya nini? Kwani alivyokubali uwaziri mkuu si alijua consequences zake? Hiyo ndio siasa. Asingetaka siasa angebakia kwao Monduli kuchunga ng'ombe
Na ukiangalia ile kashfa hakuna mahali ambapo kamati ya bunge ilimlazimisha ajiuzulu.
Alihamaki kwa kuwa kamati ya Bunge hakumuhoji.
Jiulize kama kamati haikuona haja ya kumhoji nani aliyemlazimisha kujiuzulu?

Marehemu hakuwa na kifua cha kukabili mikiki mikiki ya kisiasa.
Angetulia aone rais atachukua hatua gani dhidi yake.
 
Q
Acha mambo ya kitoto, yaani uondoke madarakani kisha urithishe urais kwa rafiki yako?
Wakarithishane mali zao siyo nchi ya watu milioni 60.
Kama ulikuwa na kiu ya kutawaliwa na Lowassa ungempigia kura.
Una akili za kitoto sana. Viongozi wengi wa Tanzania ni washikaji, watoto, ndugu wa viongozi wa zamani Nape, Makamba, Mhagama, Ridhwani na wengine. Mimi sipendi huo ujinga, ila usaliti ni usaliti. Uwe kwa uhuru na Ruto au JK na lowassa. Siwaungi mkono wote.

Ina naheshimu makubaliano, urafiki, kauli thabiti.
 
Na ukiangalia ile kashfa hakuna mahali ambapo kamati ya bunge ilimlazimisha ajiuzulu.
Alihamaki kwa kuwa kamati ya Bunge hakumuhoji.
Jiulize kama kamati haikuona haja ya kumhoji nani aliyemlazimisha kujiuzulu?

Marehemu hakuwa na kifua cha kukabili mikiki mikiki ya kisiasa.
Angetulia aone rais atachukua hatua gani dhidi yake.
Kazi yako ni kumtetea JK aliifikisha nchi pabaya. Madawa ya kulevya, rushwa, maji, umeme, vyote vilikuwa changamoto JPM akaoa jahazi.
 
Ule ni msiba wa kitaifa.
Na yeye hakwenda pale ili awe msemaji wa serikali, waandishi walitaka aseme chochote namna alivyokuwa anamjua marehemu.

kwa nini mtu asiye mwajiriwa wa serikali awe msemaji wa serikali ?
 
Kama unakumbuka vizuri jk wakati raisi huyu ndugu yake alikuwa anasuka timu ya kumtoa kwa term ya kwanza , wewe unaona ilikuwa sawa? Kwenye siasa alichokipata lowasa ni ajali za kisiasa mmoja akishinda mwingine lazima ashindwe

Kwanini alikuwa anasuka timu kama unavyosema? Watu wamejuana toka huko UDSM, jeshini? Nani alimsaliti mwenzake kwanza hadi asuke timu? Ruto na Uhuru nani alimsaliti mwenzake kwanza?

Ni hivi mara nyingi binadamu flani wakipata nafasi wanasahau walipotoka, nani waliowasaidia kufika hapo.

Usaliti mara nyingi unaanzia kwa mwenye madaraka kwa kulewa madaraka.
 
Back
Top Bottom