Jakaya Kikwete: Nilifundishwa kuishi na viongozi wenzangu, upendo ndio kila kitu

Jakaya Kikwete: Nilifundishwa kuishi na viongozi wenzangu, upendo ndio kila kitu

Haka ni kakikundi ka kumlaghai Mama Samia. Yaani Mama kastukia mchezo sasa wenyewe wanaona asiwanange. Mama shikilia hapo hapo, kumbuka hao wote walioongoza nchi kwa msalahi yao binafsi hawatakumbukwa, historia itawahukumu. Tunataka uzalendo, kumkomboa maskini na kuifanya Tanzania yenye neema
 
WAKUMBUSHANA NYIMBO ZA USHINDI VITA YA UGANDA

LEO Desemba 05,2021 wazee wa CCM walio wanajeshi akiwemo Rais mstaafu wa awamu wa Nne, Jakaya Kikwete Lt. (Colonel mstaafu) na viongozi Abdulrahman Kinana (Colonel mstaafu), Yusuf Makamba (Luteni mstaafu), Capt Ditopile Mzuzuri wengine wa serikali wameshiriki katika kumbukumbu ya kifo cha baba mzazi wa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, Hayati Brigedia Moses Nnauye.. na kutoboa siri ya jinsi walivyoishi kwa ...

Na Ditopile Mzuzuri alikuwapo?
 
Hilo ni genge la mafisadi na wahujumu uchumi.

Wazee wa madawa ya kulevya na meno ya tembo.

Twiga shipping Enterprise.
 
LEO Desemba 05, 2021

NILIFUNDISHWA Kuishi na VIONGOZI Wenzangu, UPENDO Ndio KILA KITU"

LEO Desemba 05, Rais mstaafu wa awamu wa Nne, Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa serikali wameshiriki katika kumbukumbu ya kifo cha baba mzazi wa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, Hayati Brigedia Moses Nnauye..

Hii kitu siyo
 
Hapo wanawambieni hao wazee na familia zao ndo wenye nchi na ukipewa lazima ufuate muongozo wao, mwingine gusa unate. 😀 Hapo wanajipongeza ktk hiyo karamu
Siyo kuwa wanajiandaa kuzama kabisakabisa katika bahari kama wanajeshi wa pharaoh na wapanda farasi wake?

Dunia hii inazunguka kwenye mhimili wake kutupa usiku na mchana, na yenyewe inazungukwa na mwezi kutupa miezi na nyakati katika mwaka, kisha yenyewe inazunguka jua kutupa miaka...

Uumh lets wait and see....God has never been a man to lie nor respector of persons; whoever believeth can root out kingdoms...I guess am there to see nothing absolutely nothing shall go against what was decreed in 2012...Says Ame the voluntary watch guard of this country!
 
Watashindana lakini hawatashinda, kwa mlango moja watakuja kwa milango saba watatawanyika.... I send the spirit of confusion, misunderstanding and suspecions amongst the camp of evil in Jesus name...Njia yao na ikawe giza na utelezi na mipango yote miovu dhidi ya taifa hili, ikawe kamba za kujinyongea wale wote wanaopanga kuhujumu nchi yetu na watu wake wasio na hatia...I decree and declare in Jesus name, Amen!
 
Hata angekuwa bondeni kwa Mandela, angepata kashi kashi sana kwa hujuma aliyoifanyia nchi hii!! Enzi ya Magufuli HOME SHOPPING CENTRE [ GSM] uliwasikia? Huoni ajabu leo wameanza jeuri yao?
leteni ushahidi hapa nn alichofanya kwene home shopping center zisije zikawa story za vijiwe vya kahawa.... Enzi za magufuli mbona GSM walisikika au kusikika kwa namna gani?
 
LEO Desemba 05, 2021

NILIFUNDISHWA Kuishi na VIONGOZI Wenzangu, UPENDO Ndio KILA KITU"

LEO Desemba 05, Rais mstaafu wa awamu wa Nne, Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa serikali wameshiriki katika kumbukumbu ya kifo cha baba mzazi wa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, Hayati Brigedia Moses Nnauye..

Ila pia alifundishwa kuwafanyia wananchi ujambazi sambamba na hilo? Mbona case za ufisadi haongelei kabisa?
 
leteni ushahidi hapa nn alichofanya kwene home shopping center zisije zikawa story za vijiwe vya kahawa.... Enzi za magufuli mbona GSM walisikika au kusikika kwa namna gani?
GSM waliishi kwa adabu sana ujinga waliacha kabisa😅
 
Capt. Ditopile Mzuzuri amefufuka kuja kushiriki kongomano la leo??? Andika vitu unavyovishuhudia na si unavyovifikiria.

..Ni kwasababu Mzee Yussuf Makamba alimtaja Ditopile Mzuzuri kama mmoja wa watu aliokutana nao frontline wakati wa vita vya Kagera.
 
Huu ndio uongozi, kiongozi analelewa na kuandaliwa kuwa kiongozi sio mtu anakuja anaokota watu wa jalalani tu kazi yao kubwatuka, Wana temper ya hali ya juu, hawana uvumilivu wala hekima.

Kuishi na viongozi pia ni kuheshimu waliokupita, kuwapa nafasi ya kuongea na wanapokosea ni kuwasomba majadiliano ya siri ili waelewe misimamo yako na sio kuanza kuwatukana na kuwabeza ingali wao ndio wamekuachia nafasi hiyo ya uongozi.
 
Haka ni kakikundi ka kumlaghai Mama Samia. Yaani Mama kastukia mchezo sasa wenyewe wanaona asiwanange. Mama shikilia hapo hapo, kumbuka hao wote walioongoza nchi kwa msalahi yao binafsi hawatakumbukwa, historia itawahukumu. Tunataka uzalendo, kumkomboa maskini na kuifanya Tanzania yenye neema
Maskini atakombolewa na jitihada zake hakuna Rais atakuja kuwekea watu pesa mfukoni, aliwahi kusema hakuna vya bureee.
 
LEO Desemba 05, 2021

NILIFUNDISHWA Kuishi na VIONGOZI Wenzangu, UPENDO Ndio KILA KITU"

LEO Desemba 05, Rais mstaafu wa awamu wa Nne, Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa serikali wameshiriki katika kumbukumbu ya kifo cha baba mzazi wa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, Hayati Brigedia Moses Nnauye..

Jamaa ni mkweli
 
Back
Top Bottom