Jakaya Kikwete: Rais Samia anaendesha nchi vizuri, tuendelee kumuunga mkono

Jakaya Kikwete: Rais Samia anaendesha nchi vizuri, tuendelee kumuunga mkono

JK ni bingwa wa spinning politics, anatafuta angle ya kuhamisha mjadala wa utawala wa mama kudorora, na anajua fika siku za mama kuendelea kukaa madarakani zinahesabika sana, maana kinachoendelea nyuma ya pazia ni kitu kizito na taarifa tetesi zimeshaanza kuvuja.

WanaCCM wanasema Mama hatoboi, iwe jua iwe mvua!
Tukutane 2025 na utabiri wenu fake
 
Rais mstaafu J. Kikwete akihojiwa amesema nchi inakwenda vizuri chini ya Samia na changamoto mbalimbali zinaondolewa ikiwemo uongezaji wa huduma za dharura kwenye sekta ya afya.

Kikwete amesisitiza Samia analeta matumaini kwa watanzania kwa manufaa ya leo na kesho.

My take. Hii inaweza kuwa ni njia ya kumsafisha Samia na madhaifu yanayoonekana kwenye utawala wake, amejitokeza kubadilisha upepo hasa baada ya uteuzi wa juzi wa mawaziri na lile jina moja linalojirudia kila awamu.

----
Rais mstaafu wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete leo amemsifia Rais Samia Suluhu Hassan na kusema anaendesha Nchi vizuri na kwamba changamoto hazikosekani, Dr. Kikwete ameyasema haya leo mbele ya Naibu Waziri wa Afya Dr. Godwin Mollel wakati walipotembelea eneo kutakakojengwa mradi wa jengo la matibabu ya dharura kwenye Hospitali ya Wilaya ya Chalinze iliyopo Msoga ukiwa ni mradi unaofadhiliwa na ABBOTT FUND ya Marekani kwa gharama ya Bilioni 1.2

Rais Mstaafu Kikwete amesema haya

"Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu, anayo dhamana kubwa... sio kazi rahisi... ina mawimbi mengi na pengine kwenye kazi ile unapata siku za furaha ni kidogo kuliko siku za maudhi lakini cha umuhimu ni wewe kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu, mpaka sasa anaendesha Nchi vizuri changamoto hazikosekani, nilisema wakati mmoja kwamba Babu yangu alinisumulia kwamba Nchi haipoi kama ugali, ugali ukichelewa kuula unapoa wote"

"Nchi siku zote haiwi hivyo, hapa pakipoa mara kunaibuka hili mara lile lakini katika yote hayo mpaka sasa analiongoza Taifa vizuri, Uongozi atapata moyo zaidi akiona sisi ambao tupo pamoja nae tunaendelea kumuunga mkono kumuonesha kwamba tupo pamoja, ukiwa pamoja na wenzako unapata moyo wa kukabiliana na changamoto kubwa zilizopo ofisini"

2921908_IMG-20210910-WA0137.jpg
 
Kijana wake mwandishi wa hotuba karudi kwenye kabineti.........

Ila sijawahi mchukia Jeikei,amenisaidia mengi ambayo binafsi nisingetoboa
 
Ukarimu wote anaompa ndo leo asimsifie kweli, hawa wote wezi tu na huyo mpuuzi angejua kitaani anavyochukiwa laiti angekaa kimya. Hakuna anayeomba kifo ila huyu dalali akifa nitamtolea Mungu sadaka nono sana
 
Mama kaleta matumaini, Mama chaguo la Mungu, tunakupenda sana, waongeaji wapo tu usiwasikilize.....piga Kazi.
Ombi letu tukikupa 2025 tunaomba tuachie katiba mpya...tena tunaiomba Ile ya Warioba sio Ile iliyochezewa na wanasiasa......Tunaomba Tundu Lisu na Prof Assad waongoze mchakato.
Tunakupenda sana mama la mama
unampenda wewe na nani?Ombi lenu wewe na nani?semea nafsi yako Mama K
 
Nimeamini watu wana roho mbaya, nyie Sukuma gang tulieni dawa iwaingie. JK yupo sana hata mumwombee kifo. Yaani mtu asiteuliwe kwa sababu ya chuki zenu...., Mbona Mwendazake alikua anatengua watu na hamkuwatetea, acheni vijana waliolelewa na Chama wapewe nafasi na bado wapo wengi watateuliwa kama Nape, Ridhiwani na wengine wengi
 
Chama lake lote liko njiani kurudi kwenye system, bado wawili tu so ni lazima amsifie ili pia kubadili hali ya story za huku mitaani baada ya teuzi mbili zenye utata
 
Hata mimi ningekuwa nanufaika na utawala wake iwe halali au haramu pia ningesema hivyo hivyo. Mafuta ya kula lita 20 sh. 89,000/= sukari kilo 2,900/= tozo za miamala ya simu, tozo za mita za nyumba, ugaidi wa kusingiziana!!! Mhh kweli alieshiba hamjui mwenye njaa.
 
Inaendaje vizuri wakati muhusika alisema hakujiandaa?

if you fail to prepare, you are preparing to fail.

Yuko kwenye failure state ! Simple as that

Hata mwenda zake alitwambia alikua ana bip urasi au umesahau
 
Chaguo la Mungu? Shame on you!

Mungu alimchagua huyu lini na kwenda kufanya kitu gani?

Hebu weka hapa uthibitisho tuuone?

Umepagawa nini wewe [emoji15] hukuona kura ya Mungu iliompa Samia urasi ? Weka kwenye akili yako na uzingatie Mungu huwa anamuondoa mtu ili mwingine achukue nafasi.
 
Jk bana, yaani anajiongeza yeye mwenyewe kwa kuendesha nchi vizuri.
JK acha kuzuga kumpongeza mama Samia, wewe ndio dereva
 
JK ni bingwa wa spinning politics, anatafuta angle ya kuhamisha mjadala wa utawala wa mama kudorora, na anajua fika siku za mama kuendelea kukaa madarakani zinahesabika sana, maana kinachoendelea nyuma ya pazia ni kitu kizito na taarifa tetesi zimeshaanza kuvuja.

WanaCCM wanasema Mama hatoboi, iwe jua iwe mvua!
Duh embu dadavua hizo siku mkuu?
 
Huku mjini tunachokiona ni mateja kuongezeka sana, pesa halali hakuna.
Halafu unaambiwa nchi inaenda vizuri. Haya Bwana. Mungu sio wa chalinze.

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
Aisee umesema kweli kabisa, vijana wanavuta bangi hadharani, sijui ndo nchi gani inakwenda vizuri?
Tatizo hili lisiposhughulikiwa tunakwenda kubaya sana,
Naomba viongozi wa mitaa mpelekee rais taarifa za ukweli, jk anamdanganya rais
 
Back
Top Bottom