Rais mstaafu J. Kikwete akihojiwa amesema nchi inakwenda vizuri chini ya Samia na changamoto mbalimbali zinaondolewa ikiwemo uongezaji wa huduma za dharura kwenye sekta ya afya.
Kikwete amesisitiza Samia analeta matumaini kwa watanzania kwa manufaa ya leo na kesho.
My take. Hii inaweza kuwa ni njia ya kumsafisha Samia na madhaifu yanayoonekana kwenye utawala wake, amejitokeza kubadilisha upepo hasa baada ya uteuzi wa juzi wa mawaziri na lile jina moja linalojirudia kila awamu.
----
Rais mstaafu wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete leo amemsifia Rais Samia Suluhu Hassan na kusema anaendesha Nchi vizuri na kwamba changamoto hazikosekani, Dr. Kikwete ameyasema haya leo mbele ya Naibu Waziri wa Afya Dr. Godwin Mollel wakati walipotembelea eneo kutakakojengwa mradi wa jengo la matibabu ya dharura kwenye Hospitali ya Wilaya ya Chalinze iliyopo Msoga ukiwa ni mradi unaofadhiliwa na ABBOTT FUND ya Marekani kwa gharama ya Bilioni 1.2
Rais Mstaafu Kikwete amesema haya
"Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu, anayo dhamana kubwa... sio kazi rahisi... ina mawimbi mengi na pengine kwenye kazi ile unapata siku za furaha ni kidogo kuliko siku za maudhi lakini cha umuhimu ni wewe kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu, mpaka sasa anaendesha Nchi vizuri changamoto hazikosekani, nilisema wakati mmoja kwamba Babu yangu alinisumulia kwamba Nchi haipoi kama ugali, ugali ukichelewa kuula unapoa wote"
"Nchi siku zote haiwi hivyo, hapa pakipoa mara kunaibuka hili mara lile lakini katika yote hayo mpaka sasa analiongoza Taifa vizuri, Uongozi atapata moyo zaidi akiona sisi ambao tupo pamoja nae tunaendelea kumuunga mkono kumuonesha kwamba tupo pamoja, ukiwa pamoja na wenzako unapata moyo wa kukabiliana na changamoto kubwa zilizopo ofisini"