Naipendatz
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 5,096
- 8,234
Tukutane 2025 na utabiri wenu fakeJK ni bingwa wa spinning politics, anatafuta angle ya kuhamisha mjadala wa utawala wa mama kudorora, na anajua fika siku za mama kuendelea kukaa madarakani zinahesabika sana, maana kinachoendelea nyuma ya pazia ni kitu kizito na taarifa tetesi zimeshaanza kuvuja.
WanaCCM wanasema Mama hatoboi, iwe jua iwe mvua!
Rais mstaafu J. Kikwete akihojiwa amesema nchi inakwenda vizuri chini ya Samia na changamoto mbalimbali zinaondolewa ikiwemo uongezaji wa huduma za dharura kwenye sekta ya afya.
Kikwete amesisitiza Samia analeta matumaini kwa watanzania kwa manufaa ya leo na kesho.
My take. Hii inaweza kuwa ni njia ya kumsafisha Samia na madhaifu yanayoonekana kwenye utawala wake, amejitokeza kubadilisha upepo hasa baada ya uteuzi wa juzi wa mawaziri na lile jina moja linalojirudia kila awamu.
----
Rais mstaafu wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete leo amemsifia Rais Samia Suluhu Hassan na kusema anaendesha Nchi vizuri na kwamba changamoto hazikosekani, Dr. Kikwete ameyasema haya leo mbele ya Naibu Waziri wa Afya Dr. Godwin Mollel wakati walipotembelea eneo kutakakojengwa mradi wa jengo la matibabu ya dharura kwenye Hospitali ya Wilaya ya Chalinze iliyopo Msoga ukiwa ni mradi unaofadhiliwa na ABBOTT FUND ya Marekani kwa gharama ya Bilioni 1.2
Rais Mstaafu Kikwete amesema haya
"Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu, anayo dhamana kubwa... sio kazi rahisi... ina mawimbi mengi na pengine kwenye kazi ile unapata siku za furaha ni kidogo kuliko siku za maudhi lakini cha umuhimu ni wewe kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu, mpaka sasa anaendesha Nchi vizuri changamoto hazikosekani, nilisema wakati mmoja kwamba Babu yangu alinisumulia kwamba Nchi haipoi kama ugali, ugali ukichelewa kuula unapoa wote"
"Nchi siku zote haiwi hivyo, hapa pakipoa mara kunaibuka hili mara lile lakini katika yote hayo mpaka sasa analiongoza Taifa vizuri, Uongozi atapata moyo zaidi akiona sisi ambao tupo pamoja nae tunaendelea kumuunga mkono kumuonesha kwamba tupo pamoja, ukiwa pamoja na wenzako unapata moyo wa kukabiliana na changamoto kubwa zilizopo ofisini"
unampenda wewe na nani?Ombi lenu wewe na nani?semea nafsi yako Mama KMama kaleta matumaini, Mama chaguo la Mungu, tunakupenda sana, waongeaji wapo tu usiwasikilize.....piga Kazi.
Ombi letu tukikupa 2025 tunaomba tuachie katiba mpya...tena tunaiomba Ile ya Warioba sio Ile iliyochezewa na wanasiasa......Tunaomba Tundu Lisu na Prof Assad waongoze mchakato.
Tunakupenda sana mama la mama
Atoboe wali tena. Keshakua Raisi, cheo cha juu kabisa Tanzaniahatoboi??
Kumweka Mbowe ndani na kuzuia mikutano halali ya ndani ya Chadema.Anamsafisha kwani kachafuka na nini?
Maza asipompa unaibu before 2025 nitashangaa sana.Wanajuana hawa na wana agenda zao.
Rizimoja uwaziri uko njiani.
Inaendaje vizuri wakati muhusika alisema hakujiandaa?
if you fail to prepare, you are preparing to fail.
Yuko kwenye failure state ! Simple as that
Chaguo la Mungu? Shame on you!
Mungu alimchagua huyu lini na kwenda kufanya kitu gani?
Hebu weka hapa uthibitisho tuuone?
Duh embu dadavua hizo siku mkuu?JK ni bingwa wa spinning politics, anatafuta angle ya kuhamisha mjadala wa utawala wa mama kudorora, na anajua fika siku za mama kuendelea kukaa madarakani zinahesabika sana, maana kinachoendelea nyuma ya pazia ni kitu kizito na taarifa tetesi zimeshaanza kuvuja.
WanaCCM wanasema Mama hatoboi, iwe jua iwe mvua!
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni ssh , teuzi na mikutano. Kwani hamuoni akituwawakilisha Watanzania sawia kabisa ππππSamia zaidi ya kuvaa ushungi hakuna anachodeliver kwenye nchi!
Aisee umesema kweli kabisa, vijana wanavuta bangi hadharani, sijui ndo nchi gani inakwenda vizuri?Huku mjini tunachokiona ni mateja kuongezeka sana, pesa halali hakuna.
Halafu unaambiwa nchi inaenda vizuri. Haya Bwana. Mungu sio wa chalinze.
Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app