Jamaa yangu ananitesa kisa alinitafutia kazi, ni haki?

Niliwahi kupitia changamoto inayoelekea kufanana na hiyo.

Kwa kweli nilipitia maumivu mpaka siku nilipoamua kumuambia ukweli
 

Mchane ukweli mwambie tenda wema nenda zako atakae kulipa Mungu
 
Wadogo zetu tukiwapa connection za kazi mkumbuke japo fadhila japo sio haki Kuna muda tunawaitaji hata mtutembelee nyie mnakua busy mnasahau mlikua mnashinda sebuleni kugombea remote na watoto wetu...
 
Mimi jamaa yangu alikua ananiconnect kwenye kazi yenye mshahara mkubwa kuliko wake, yaani ningemzidi mara 2. Bahati mbaya tu sikupata ikabidi anikonektie kwenye kitengo chake.

Nilipokuja kujua ile kazi alokua ananitumia link several times akisisitiza niapply ina ujira mkubwa kuliko wake, niliona jamaa ana roho nzuri sana.
 
Mwambie amshukuru mungu maana duniani kila binadamu kaletwa ili amuinue mwezake au amvushe mwezake kwa hiyo usiumie sana kichwa kwa hilo.
 
Pole sana. Muombe Mungu kwa imani yako, kua mvumilivu kuna siku utafanya maamuzi bila wewe kutarajia. Makazini kuna mambo ya ajabu sana. Nilipitia hii hali ilinitesa sana ila Mungu mwema sikudumu kwenye ile ajira.
 
Cha kukushauri hapo, tanua mianya ya kukuingizia kipato mf fungua biashara, chukua hata bajaji za mkopo ndani ya muda mfupi chombo kinakuwa chako 100% .

Ukitegemea kazi basi jua fika jamaa hashindwi kukuharibia muda wowote.
 
Cha kukushauri hapo, tanua mianya ya kukuingizia kipato mf fungua biashara, chukua hata bajaji za mkopo ndani ya muda mfupi chombo kinakuwa chako 100% .

Ukitegemea kazi basi jua fika jamaa hashindwi kukuharibia muda wowote.
Hii ya bajaji naomba mchanganuo zaidi mkuu...Yani nakopaje, riba shingapi na itanifaidisha vipi hiyo bajaji?
 
Kwanza Mimi skumuomba kazi, yeye ndo alinitafuta from the blue...afu saiv ndo imekuwa kama deni
Kwa jibu hili japo sijasikiliza upande wa pili ila inaonesha wazi mwenye matatizo ni wewe pia wewe ni mchoyo wa fadhila kuna vitu unavificha ficha.

Maana ulivyoandika kana kwamba shobo zake jamaa ndio zimepelekea kukufanyia connection.
 
Kwa jinsi nilivyosoma replies zake nimegundua tatizo lipo kwake na sio kwa huyo mshikaji wake.

Huyu mleta mada ndio dizaini ya wale watu unaowasaidia wakifanikiwa wanakupiga majungu na kutaka kushindana na wewe uliyewasaidia na kukushusha kabisa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…