James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

Asamehe na kusahau maana tayari mwenye vita yake ameshaipigana na kuishinda.
 
Mimi nimemkubali, mzee ameona potelea Kwa mbali afie gerezani watoto wabaki na utajiri, hiyo ndio Tafsiri ya Kufa kiume
vijana tijifunze kupata hela ni jambo moja na kuilinda ni jambo jingine linahitaji uwe kauzu na roho ngumu
Kuna kipindi alilegea akaiomba mahakama imruhusu ataje wahusika wa escrow ili aachiwe jaji akakataa. Huu mlungula ulipita Hadi kwa majaji, maaskofu, mawaziri na mmmmh.
 
[/QUOTE]
Watoto wake wajifunze jinsi baba yao alivyojitoa kutetea mali yake kwa kukubali kuteseka miaka 4 akiamini ktk nguvu zake..
Ili kesho wajue thamani ya mali hiyo kuisimamia....

Na jinsi ya kufanya ibada ya kufeast kila mwaka na kusafisha makaburi yaliyo uani pale makongo.
 
Ameteseka lakini alibakia imara dhidi ya mdhurumaji. Siku zote ushindi wa mwenye haki uko mikononi mwa Mungu.

Hukumu ya Mungu haikawii wala kichelewa bali huja kwa wakati ulio sahihi.

Pole sana Mzee Rugemarila, kayafurahie maisha yako ya uzeeni baada ya wakala yule wa ibilisi kukupitisha kwenye tanuru.
 
Besti kufa kufaana. Ila najiuliza Jiwe alishindwa kweli kumpora hela zake hadi yeye akubali? Kama TRA tu walipora hela st jude account bila ridhaa yao Jiwe angeshindwa kwa rugee kweli?
Pesa za Ruge zilikua na mkono wa tatu, nadhani unafahamu hilo. Huo mkono wa tatu ndio uliosema "pesa sio za serikali"
 
Salaam Wakuu,

Leo nimepita maeneo ya Mahakama ya Kisutu, Nikakuta Mkurugenzi wa kampuni ya VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira anatabasamu akiwa na ndugu zake wakipeana hugs na kuchumiana. Inaashilia kuna dalili nzuri leo Mzee wa Henken akaliona jua. Langu Dua.

_MG_0435.JPG
James Rugemalila(Kulia) na mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh(Kushoto), wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi kabla ya kupanda kizimbani Mahakamani Kisutu Jijini Dar.

Tarehe 19 Jun, 2017 TAKUKURU wawafikisha mahakamani Seth Na Rugemalila kwa uhujumi uchumi. walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu wakishtakiwa kwa makosa sita ya uhujumu uchumi, likiwamo la kuisababisha Serikali hasara ya jumla ya takriban Sh358 bilioni.

Wakili wa Serikali, Paul Kadushi aliyataja mashtaka mengine yanayowakabili wawili hao kuwa ni kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kuisababishia hasara Serikali.

Zaidi Soma:

1). TAKUKURU yawafikisha mahakamani Harbinder Sethi na James Rugemalira kwa kosa la Uhujumu uchumi

UPDATE:

Rugemalila yupo huru!

Mashtaka yake yameondolewa chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwanendo wa Makosa ya Jinai

Inasikitisha kama kweli alibambikiziwa kesi basi Mungu atawalipa waliofanya hivyo sawia na matendo yao
 
Back
Top Bottom