James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

Moja ya watu wagumu,alikataa kukir hali akijua hana kosa.Mwenzake alikir hivi sasa analipa mihela kwa kesi ya kubambikiwa.Haya maisha bhana,anarud uraian adui wake alishajifia na watu wameshasahau.
 
Ushahidi wa kubumba hata ukae ndani miaka 100 hauwezi patikana.
Rejea wazee wa uhamsho,wazee wa escrow ni kesi za kubandika tu.
Hata Mbowe watahangaika wee mwisho watamuachia.
Huwezi ukabuni ushahidi wa uongo
 
Hapana mkuu!
..
Chadema ya sasa inamuona Ruge malaika. Lakini kumbuka kina Ruge walikomaliwa sana na kina Lisu kipindi kile cha Jk.

Sijaona chadema hii ya sasa ikitaka hao uliowataja waunganishwe na Ruge ila tunaona wakifurahia sana Ruge kutoka wakidai alionewa!

Tangu Gwajima awe mshenga wa kumleta EL pale chadema ndio ukawa mwisho mwema wa mapamabano dhidi mafisadi uliasisiwa na kina Slaa.

Ndio maana nasema nikiona mtu yeyote kwenye nafasi alafu akapiga mihela yake ntamsifu sana.

Kurajiribu kuwapigania watz ni kujichosha bure. Ndio sababu juzi nilisema Mbowe anahangaikia kitu gani? Anapata tabu kwa ajili ya mijitu isiyojielewa? Au labda ananufaika na harakati zake?

Soma hiyo thread ndio utaelewa kwanini wanaona Rugemalira sio tu ameonewa ila ametolewa kafara kuwalinda mafisadi papa yaliyopo serikalini na chamani. Mfano chenge, Muhongo, Ngeleja n.k
 

Soma hiyo thread ndio utaelewa kwanini wanaona Rugemalira sio tu ameonewa ila ametolewa kafara kuwalinda mafisadi papa yaliyopo serikalini na chamani. Mfano chenge, Muhongo, Ngeleja n.k
Kwanini waone kaonewa?

Kwanini wasipiganie hao uliowataja nao washitakiwe badala ya kushangilia Ruge kutoka?
 
Salaam Wakuu,

Leo nimepita maeneo ya Mahakama ya Kisutu, Nikakuta Mkurugenzi wa kampuni ya VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira anatabasamu akiwa na ndugu zake wakipeana hugs na kuchumiana. Inaashilia kuna dalili nzuri leo Mzee wa Henken akaliona jua. Langu Dua.

_MG_0435.JPG
James Rugemalila(Kulia) na mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh(Kushoto), wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi kabla ya kupanda kizimbani Mahakamani Kisutu Jijini Dar.

Tarehe 19 Jun, 2017 TAKUKURU wawafikisha mahakamani Seth Na Rugemalila kwa uhujumi uchumi. walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu wakishtakiwa kwa makosa sita ya uhujumu uchumi, likiwamo la kuisababisha Serikali hasara ya jumla ya takriban Sh358 bilioni.

Wakili wa Serikali, Paul Kadushi aliyataja mashtaka mengine yanayowakabili wawili hao kuwa ni kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kuisababishia hasara Serikali.

Zaidi Soma:

1). TAKUKURU yawafikisha mahakamani Harbinder Sethi na James Rugemalira kwa kosa la Uhujumu uchumi

UPDATE:

Rugemalila yupo huru!

Mashtaka yake yameondolewa chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwanendo wa Makosa ya Jinai

HAYA NI MAMBO YA MUNGU TU. SIKUTEGEMEA RUGEMALIRA ANGETOKA MAHABUSI AKIWA MZIMA. MWENYEZI MUNGU AMPE FARAJA KWA MATESO ALIYOYAPATA KWA KOSA LA KUUZA HISA ZAKE!
 
Kwanini waone kaonewa?

Kwanini wasipiganie hao uliowataja nao washitakiwe badala ya kushangilia Ruge kutoka?
Kina seth wamelipwa so wao ni wanufaika tu ila issue ni nani aliyewalipa? Nani aliyekubali malipo wanayodai ya kifisadi kutolewa? BOT na wizara ya fedha wanaponaje? Vipi TRA ambao hawakuona hta capital gain tax ya kukata??

Walishinikiza sana kina Lissu toka siku ya kwanza Seth anakamatwa ila kimyaa watu wakadai anapinga kila kitu. Leo yakwapi sasa? Wameshindwa leta ushahidi mwaka wa 5 huu maana mafisadi ya kweli yapo CCM na serikalini na ndio yaligawana pesa kwenye masandarusi!!

Kuna quote moja inasema "Serikali huamua nani ni adui wa nchi kulingana na maslahi yake kwa wakati huo" So mnaweza iba 10 ila ukakamatwa mmoja tu sababu hao 9 wana maslahi na serikali so wana haki kuliko wewe!!!

That's politics
 
Mchongo ulifanywa na Kikwete so lazimi wamuachie tu
Ndiyo maana alipotaka kutaja wahusika wa escrow serikali ilimkatalia. Jk oyeeeee. Sasa business as usual Mama keshamwachia nchi Vasco.
 
Kina seth wamelipwa so wao ni wanufaika tu ila issue ni nani aliyewalipa? Nani aliyekubali malipo wanayodai ya kifisadi kutolewa? BOT na wizara ya fedha wanaponaje? Vipi TRA ambao hawakuona hta capital gain tax ya kukata??

Walishinikiza sana kina Lissu toka siku ya kwanza Seth anakamatwa ila kimyaa watu wakadai anapinga kila kitu. Leo yakwapi sasa? Wameshindwa leta ushahidi mwaka wa 5 huu maana mafisadi ya kweli yapo CCM na serikalini na ndio yaligawana pesa kwenye masandarusi!!

Kuna quote moja inasema "Serikali huamua nani ni adui wa nchi kulingana na maslahi yake kwa wakati huo" So mnaweza iba 10 ila ukakamatwa mmoja tu sababu hao 9 wana maslahi na serikali so wana haki kuliko wewe!!!

That's politics
Hiyo haihalalishi mwizi aliekamatwa kuachiwa na nyie kushangilia
 
Kwa Ruge alishindwa hilu nakuthibitishia, walioporwa pesa wote ni wale wakiogoopa kukaa jela na kukubali yaishe.

Huyu ni mwamba aingizwe kwenye orodha ya mashujaa.

Ruge is clean mahakama mpaka leo haihamwingiza hatiani, kwa kanuni za kisheria Mzee Ruge amesafishwa rasmi na serikali.
Swadakta...Ruge ni mwamba

Ova
 
Trial by court of public opinion

Hiyo ndio sababu iliyofanya serikali ilazimishe kesi na mzee wa watu kuteseka bila ya ushahidi wa tuhuma.

Watu wakulaumu Zitto, Kafulila, Lissu, CAG wa muda ule na media; kuwalisha watu uongo.

Rugemalila is no angle na PPP ya IPTL na TANESCO haikupitia mchakato halali, wala uamuzi wa kuipa kazi aukuwa na faida kwa taifa.

But it was all legal na hela zilizokuwa kwenye escrow account zilikuwa ni za IPTL.

Sasa nani alikuwa anamiliki IPTL hapo ndio ilikuwa shida mpaka mahakama ilipoamua.

Hii nchi inabidi uwe makini sana na wanasiasa wanaweza kukutengenezea mazingira siyo kabisa.

JK alishaeleza zile sio hela za serikali ni za IPTL.
 
Mwambieni huku nje kuna hukumu ya COVID-19.

Asifanye mzaha, hukumu hiyo haitenguliwi na yeyote.

Tanzania imekuwa nchi ya kuoneana kwelikweli, sijui tutafika wapi na hali ya namna hii!
 
Sawa ukumbuke hawa ni majizi mazoefu yanajua kuiba nakuondoa ushahidi..

Kuibaa sio tatizo tatizo unaiba je na kiasi gani?

mbona hawajakukamat wewe na kukufanyia upelelezi? Haya mambo ni magumu
Be serious. Wizi huo unahusisha serikali na mkubwa ana mkono mzito kwenye misheni hiyo. Unategemea nini? Kwa serikali ya CCM kusema inapambana na ufisadi ni UNAFIKI wa hali ya juu. Hakuna ufisadi mkubwa wa kiwango hicho unaoweza kufanikiwa bila "signecha" ya mkuu mwenyewe.

Baada ya kushindwa kushughulika na mkuu wa awamu ya iliyopita, mwendazake kavamia kina Ruge akitarajia wamgawie pasenti ya mshiko wa "wizi". Where is the moral high ground with these people? Ndio maana wanaishia kudhalilika kwa roho zao mbaya. Mkuu wa sasa kaondoa "nadhiri" ndio unasikia DPP akidai eti "sina nia"! kirahisi rahisi tu! Sijui wanapata wapi amani ya roho watu hawa?
 
Back
Top Bottom