Jamii za Pwani malezi ya watoto yamewashinda. Dini imeshindwa kuwasaidia pia

Sio tu wanafaa kuwa wake/kuolewa, Wanafaa pia kuwa viongozi wa chama na serikali si wameshakua? Tuwapambania waingie kwenye uongozi wataleta mabadiliko makubwa sana.

🤡🤡

Zamani binti wa umri huo anakuwa malkia. Kijana wa miaka 23 anakuwa mfalme anayeweza kutawala dunia nzima. Ninyi mnazungumzia nini?

Uongozi sio umri.
Uongozi ni kipaji kama vipaji vingine
 
Siwezi wahukumu hao watoto,wapo huru kuonyesha hisia zao kama binadamu haijalishi utavyozipokea .

Pia maneno yao yamechagizwa Na furaha ya kumaliza elimu ya secondary ambayo imeendana Na kukua kiumri hivyo kujiona wanakuwa huru ktk maamuzi yao.

Pia sitegemei wao wawe malaika in this world of 'wicked and adulterous generation'
 
Wewe mbona hutolewi mahari kama ni heshima?
Mwanaume ndio anaenda kuomba kwa mwanamke.
Iko hivyo.

Mahari ni kununua mwanamke.
Ninyi ndio mnafuata mila msizozijua.
Nimekutolea mfano wa watu ambao hawana mahari kwenye kuachana inakuwaje.

ukiangalia kwa undan utajua ishu sio mahari.
Ww mwanao akiolewa awe ametolewa mahari au hajatolewa.
Mwisho wa siku wakitengana bado process ni zile zile.

Mwisho wa siku akifariki bado familia ya mwanaume ndio inapewa kipaumbele.

Kwahiyo uwe umechukua hela ya mahari au haujachukua.
Mwisho wa siku namna ya kushughulikia masuala haya ya mwanamke ambaye yuko kwa mwanaume ni the same.

Mm nina sapport mahari kwa sababu naona ni heshima kwa wazazi na ndugu wa Mwanamke na siichukulii kama kununua mwanamke.

Na ofcoz nataman mwanangu akikua , basi mwanaume wake afuate taratibu zote na nipate wasaa wa kuongea nae ana kwa ana na nimkabidhi binti yangu kwake.
 
Kuna vitu vingine mnabisha bur tu, mimi Dada yangu amesoma University akiwa kwenye ndoa, haya ni makubaliano muowaji anatakiwa ayafahamu tangu awali tunakuzoezesha lakini kwa sharti binti aendelee na elimu, mengine ni nia ya binti mwenyewe kusoma, maana kusoma nako ni wito.

Mimi binafsi pia wife amegraduate tuna watoto, chabmsingi ni watu kujitambuwa.
 
Najifunza aisee!
Mkuu
Hata kanda ya ziwa tunatukanwa sana sijawahi ona reaction, nyinyi sijui kwann mnawahi kuchukia mkiguswa!
hapana mimi sijawahi comment nimeishi mwanza almost 9 years na nimetembea kanda ya ziwa karibia mikoa yote nimeishi na watu vizuri kila jamii ina mazuri na mabaya yake.

Mimi huwezi nikuta na beza jamii bila kunigusa mimi mhusika.
 
Mm kama binti yangu shule imemshinda yupo tu nyumbani na akaja kijana akamposa kama huyo mtu anatoka kwenye familia nzuri,na kijana mwenyewe mienendo yake ni mizuri nini naruhusu akaolewe tu.
Akienda ndoa ikamshinda atarudi nyumbani akae kama wengine maana kuna watu wanaolewa wakiwa na miaka mpaka 40 na ndoa zinawashinda.
Kama ataendelea na masomo akisha fika chuo yeye mwenyewe akaniletea mchumba na nikajilidhisha kuwa anafaa siwezi kumkataza kuolewa.
 
Si ndo furaha yenu.Mnataka utandawazi uislam na sharia zake hamuutaki.mnalaumu nini?
Unazungumzia uislamu wa kutoa talaka ya maneno kwa ndoa ya miaka 15.!?

Uislamu ni utahila wenye heshima
 
Zamani binti wa umri huo anakuwa malkia. Kijana wa miaka 23 anakuwa mfalme anayeweza kutawala dunia nzima. Ninyi mnazungumzia nini?

Uongozi sio umri.
Uongozi ni kipaji kama vipaji vingine
Ndio maana yake kuwa kwanini likija suala la mabinti mnawasukumizia tu kwenye kuoa/kuolewa tu? Wameshakuwa wanafaa kabisa kuwa viongozi wa chama na serikali na makanisa.
 
Ni kama unapoint hivi. Kuna binti alioelewa alipo maliza tu kidato cha nne. Ingawa yeye binti alikuwa hataki kuolewa lakini mama yake aliforce aolewe tu na pia matokeo ya form 4 hayakuwa vizuri. Leo hii huyo binti akili imekomaa na anajivunia familia yake .

Ili ndoa kudumu na mabinti kukomaa kiakili pole pole ni muhimu mabitinti wadogo waolewe na wanaume waliokomaa na sio wanyoa viduku.
 
Mkuu

hapana mimi sijawahi comment nimeishi mwanza almost 9 years na nimetembea kanda ya ziwa karibia mikoa yote nimeishi na watu vizuri kila jamii ina mazuri na mabaya yake.
Vizuri umeona vyote, wengine wananote mabaya tu, mimba malaya mashoga wako kila sehemu tunazidiana kwa takwimu tu! Sasa unakuta mtu anashadadia ili tu apate unafuu duh!
Mimi huwezi nikuta na beza jamii bila kunigusa mimi mhusika.
Mimi hata nigusweje ntajibu kama kuchangia mada ila sio niibebe kama mi ndo RC
 
Ninao ishi kuna vitoto vina mazoea ya kijinga, yaani ni wanataka kabisa mashine. Na ndo ukanda huu huu wa pwani Dar..

Kuna mgahawa huwa naenda kula, siku moja kuna wuhudumu alimwambia mteja mmoja mwenye mazoea naye, "yaani wewe, mimi ningelikuwa mwanaume ningelikufira"

Na hakuna mtu akiyeshtuka, as if matusi kwao ni kuinganishi

Pia katika harakati zangu mkoa wa lindi, kule watoto wa miaka 16,17,18 tayari wanajiuhisha na ngono nzembe. Kule yaani wanaona fahari kumiliki mabwana
 
Ndio maana yake kuwa kwanini likija suala la mabinti mnawasukumizia tu kwenye kuoa/kuolewa tu? Wameshakuwa wanafaa kabisa kuwa viongozi wa chama na serikali na makanisa.
Kwani wao kuolewa Kuna wazuia kuwa viongozi wa chama na serikali?
Ya kwamba ukitaka kuwa kiongozi wa chama au serikali ni usiolewe ndo kigezo?
 

Kuachana sio kugumu kama unavyotaka kuzungumza hapa.

Ugumu unaletwa na mambo kadhaa. Mojawapo ni hilo la nani kamuoa mwenzake. Kwamba mmoja anamamlaka juu ya mwingine jambo ambalo ni mila potofu.

Pili, suala la mali. Hili ndio huwa gumu zaidi. Mgawanyo wa mali na maslahi ya mtoto huongeza mchakato wa kuachana kuwa mrefu.

Kwa watu wanaojitegemea kiuchumi, kiakilia na kihisia. Kuachana ni jambo rahisi na lisilo na mambo mengi.

Mnaongea kwamba mmefikia mwisho kisha mnajadiliana nani anabaki na kipi na nani anabaki na kipi. Au mnafuata haki kwamba kila mtu aondoke na alichochuma. Ni simple sana.

Ubinafsi ndio chanzo cha kuona kuachana ni kugumu.

Mahari,
Huwezi kuja kwangu alafu tujadiliane kuhusu kiasi gani unipe ili umchukue binti yangu. Hiyo haiwezekaniki.

Yaani Mtibeli na ndevu zangu nijadili binti yangu hatoki bila milioni tatu. Ati na ninyi mnashusha na kubagaini huo ujinga siwezi mfanyia binti yangu.

Njoo na zawadi ulizonazo. Na binti yetu akija kwenu atakuja na zawadi alizonazo. Simple.
 
Unazungumzia uislamu wa kutoa talaka ya maneno kwa ndoa ya miaka 15.!?

Uislamu ni utahila wenye heshima
Sasa nani amekwambia talaka ni kosa kutoa?
tumia akili yako vizuri.
Talaka ipo hata kwenye ukristo sema haumjui dini yenu
 
Single parenting ni janga, tunajitoa akili tu lakini kukea mtoto mwenyewe ni janga kwa asilimia kubwa sana.

Kujali elimu ya dini kuliko elimu ya kidunia pia ni janga, mtoto aende shule kuondoa ujinga, mtoto asimamiwe kuanzia shuleni hadi nyumbani.

Ndoa za utotoni ni janga, bjnti miaka 15-18 analea ndoa badala ya kusoma(hata kama sheria zinaruhusu).

Wazazi kuwa busy kusaka pesa, janga lingine na bomb kubwa.
 
Ndio maana yake kuwa kwanini likija suala la mabinti mnawasukumizia tu kwenye kuoa/kuolewa tu? Wameshakuwa wanafaa kabisa kuwa viongozi wa chama na serikali na makanisa.

Kwani hakuna vijana waliooa wakiwa na miaka 18 - 20?

Kwa nini useme tunawasukuma wakati wao wametaka kwa hiyari yao?

Hakuna force marriage hapo. Ni wao wenyewe.

Force marriage ni ile binti anataka kuolewa sasa hivi anamiaka 19 ninyi mnamlazimisha aolewe akimaliza chuo. Ujinga mtupu. Dhulma
 
Wanaouishi Wokovu katika Kristo Yesu ndio wanaweza kuelewa nilichokiandika hapo kinajipambanua vipi.

Mkuu,kuna dini,tena nyingi tu,zinajiita "Za Kikristo" lakini hazina Wokovu wa Kristo ndani yake.

Kwa kifupi ni kwamba kuna namna Shetani amefanikiwa sana kuwachanganya na kuwakanganya watu wengi wasione kwamba wanachohitaji kwenye maisha yao ni Wokovu katika Kristo Yesu sio Dini.
 

Uko sahihi kabisa. 100%
 
Hata kanda ya ziwa tunatukanwa sana sijawahi ona reaction, nyinyi sijui kwann mnawahi kuchukia mkiguswa!
kiufupi
Vizuri umeona vyote, wengine wananote mabaya tu, mimba malaya mashoga wako kila sehemu tunazidiana kwa takwimu tu! Sasa unakuta mtu anashadadia ili tu apate unafuu duh!

Mimi hata nigusweje ntajibu kama kuchangia mada ila sio niibebe kama mi ndoo RC
Mkuu

Nimezunguka mikoa yote Tanzania tabia za wabantu zinafanana kwa kiasi kikubwa.

Nilichotambua kuna watu hawana furaha ya maisha kwaio JF ndio pakutua mzigo.

Mimi nilikua natumia fake ID but nikajitathmini kua sina ugomvi na mtu kwaio natumia jina langu halisi kwa sasa.

Pia kama mtu anajiamni akaposti kusema kabila au dini au atumie ID kama paschal mayala na wengineo.

Mimi si bora kuliko wanadamu wenzangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…